Amesilimu Kwa Sababu Ya Kutaka Kuoa lakini anakiri kuwa yeye ni Mkristo, Je, Ndoa Inaswihi?


 

SWALI:

Bismilahi rahmani rahim,, namshukuru alwa kwa neema zake na nguvu zake za kusimamisha mbingu na ardhi..na kuindeleza website ili iidi kuulingania uislam uzidi kusonga mbele..............

Swali, kuna mtu mmoja..Alitokea kumpenda sana binti mmoja alikuwa ndani ya dini ya kiislam...lakini yeye yupo ndani ya ukristu.. sasa akapeleka ujumbe wa kutaka kumuoa  ktk familia ya yule binti..yule  bwana akajibiwa ya kwamba haitowezekana ,,kwa sababu ya dini yako...

alicho kifanya yeye ni kwenda kwa shekh kusilim,,lakini sio kwa kupenda ila ni kama wale wazazi wajue ni kweli amesilim ili wampe mke...na kweli baada ya hapo akapewa mke.. kilicho fuatia mpaka sasa yeye nusu mkristu nusu  mu islam.......kanisani haendi wala masjid..lakini yeye mpaka sasa anakiri kabisa kama yeye ni mkristu.....na kwa mkewe anamwabia yeye ni muislam...lakini ndugu zake wa najua yeye ni mkristu...sasa mtihani unakuja hapa mtu kama huyu akifa azikwa vipi au ktk dini ipi................. wakwe wanajua ni muislam  ..... sasa huu si utata.................................

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'Alayhi Wa Aalihi Wasallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'Anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani kwa swali lako kuhusu jambo hili nyeti. Hakika ni kuwa hili ni tatizo kubwa kwa Waislamu wanaoishi katika Afrika Mashariki na hasa kwa ndoa kama ambazo zinaleta utata mkubwa katika familia. Hivyo, ni nasaha yetu kuwa ikiwa mume si Muislamu na amempenda binti basi apatiwe muda baada ya Kusilimu kabla ya kuozwa binti. Muda utakuwa wa kumsomesha Dini na kumfundisha mpaka jamii ihakikishe kuwa kweli amekuwa Muislamu wa utekelezaji.

Hapa tunakumbuka kisa baina ya Mzungu mmoja aliyekwenda Mombasa wakati Sheikh Muhammad Qaasim Mazrui ndiye Qadhi Mkuu wa Kenya. Huyu bwana alipendana na msichana wa Kiislamu naye akaambiwa kuwa hawezi kumuoa mpaka asilimu, naye akasema kuwa ikiwa ni hivyo basi yu tayari. Wazazi walitaka ushauri kwa Sheikh Muhammad, naye akawaambia wamlete. Sheikh alimwambia ya kwamba wazazi wanaona wapatiwe muda kabla ya harusi hivyo yeye asilimu mwanzo na yule Mzungu akasema kama ni hivyo basi sina haja ya kusilimu.

Katika Uislamu mtu anatakiwa aingie mzima mzima na wala sio nusu nusu

((Enyi mlioamini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala msifuate nyayo za shetani; hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi )) [AL-Baqarah 2: 208]

 

  Hawezi mtu kuwa ni Muislamu na hapo hapo ni Mkristu, ima utakuwa Muislamu au Mkristu na ikiwa yeye aliingia katika Dini kisha akatoka atakuwa ni murtadi na hivyo ndoa ya hao wawili inavunjika. Na ikiwa yeye mwenyewe anakiri si Muislamu basi amejitoa mwenyewe na ni lazima familia ijulishwe na hiyo ndoa ivunjwe kwani sasa wanakuwa wanazini.

Ikiwa yeye mwenyewe anajijua kuwa si Muislamu hilo linakuwa ni jambo sahali kwani akifa atazikwa na watu wake Kikristu.

Tusiwe wepesi kuwaoza watu kama hawa kwani kisha huleta matatizo mengi katika ndoa na familia. Tuwe waangalifu na tahadhari katika mas-ala mazito kama ya ndoa.

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share