Kulea Mtoto Wa Kitendo Cha Zinaa Inafaa?

 

SWALI

Assalam aleikum ndugu zangu.nashukuru sana kwa kunipatia jibu swala langu lilotangulia.Sasa niko na swali: jee kumwangalia na kumlea mwanaharamu wa mumeo inafaa?yaani yule baba kuchukuwa responsibility ya yule mtoto wake wa nje ni dhambi,is it like entertaining what he did in his past?ama si dhambi?kisha huyo mtoto ni wa kike ana ndugu yake kwa mama mwengine wa kiume .

 

 



JIBU:

BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa  aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa ba’ad:

Kwanza tutambue kuwa mtoto aliyesababishwa na zinaa  hana dhambi yoyote ile, bali dhambi ni kwa baba na mama waliyemzaa. Kwa hiyo asiwe ni mtoto wa kudharauliwa au kutupiliwa mbali, au kuonewa kwa aina yoyote au kupewa jina hilo 'mtoto wa haramu'.

Na kumlea mtoto huyo ndivyo inavyompasa mtu baada ya kusababisha kuzaliwa kwake kutokana na kitendo cha zinaa. Na mke kumlea mtoto wa mumewe ikiwa ni mtoto wa zinaa au aliyezaliwa katika ndoa ni jambo jema ambalo litampatia mke huyo thawabu kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى na pia itakuwa ni sababu ya kupata ridha na mapenzi zaidi ya mume.

Na thawabu zitakuwa zaidi pindi atakapomlea mtoto huyo kwa malezi mema yenye mafunzo ya dini hadi akue ili atambue jema na baya na aweze naye kujiepusha na mabaya kama hayo aliyoyatenda baba yake.

Na haina maana kwamba kumlea huyo mtoto ni kama kutia nguvu jambo la zinaa bali unafanya wajibu unaokupasa kufanya kumlea mtoto asiye na dhambi yoyote.

 

Na Allah Anajua zaidi.

Share