Kiza Kinaingia Mapema Mno Msimu Wa Baridi Aswali Vipi Magharibi Na Ishaa

 

 

SWALI:

 

Asalam Aleykum! Ndugu zetu waislamu, Mwenyezimungu awajaze na awape subra na muendele kutusaidia na maswali yetu. Inshallah.
 

Swali langu la pili, mimi naishi ujerumani kwa sasa, na wakati umebadilika, kwa mfano, saa kumi na nusu kumekuwa usiku yaani giza limetanda, je nitaswali magharibi saa ngapi na ishaa saa ngapi?.

 

Tafadhali ningependa munijibu maswali yangu

 

ASANTENI SANA NA JAZA YENU IKO KWA MWENYEEZI MUNGU: 

 


 

 

JIBU: 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa maswali yako, na hapa tunakupatia majibu yako.

 

 

Swalah zote zimewekewa wakati maalumu na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo inatakiwa popote ulipo ufuate mwongozo huo. Swalah ya Magharibi inaingia wakati jua linapozama, hivyo likiwa linazama saa kumi na nusu inabidi uswali wakati huo wala usiwe unangojea ifike wakati ambao watu wa Afrika Mashariki wanaswali.

 

Nchi nyingi ambazo zina mabadiliko ya masika, wakati wa Swalah unabadilika sana. Wakati wa baridi Swalah ya Magharibi inakuwa mapema kama wakati huo uliotaja lakini wakati wa joto mchana unakuwa mrefu na inawezekana mukawa mnaswali magharibi huko hata saa mbili au tatu usiku.

 

Na Allah Anajua zaidi

 

 

 

Share