Kutimiza Swalaah Za Fardhi Kabla Za Sunnah

 

 

SWALI LA KWANZA

inafaa kuunga swala ya magharibi pamoja na ishaa kwa ajili ya tahajjud? 

 

SWALI LA PILI

As salaam alaikum,ndugu zangu waislam alhidaaya,swali langu ninalopenda kuuliza ni kama ifuatavyo       mimi naishi ktk nchi za ulaya magharibi,swala ya magharib huiswali usiku kutokana na kuzama kwa jua,je naweza kuswali na swala ya isha? Baada nikisha swalimaghrib?Nia na madhumuni niamke usiku ili niswali Tahjudd.Ambayo hii swala tumeambiwa tuswali usiku mwingi,kisha wakati huo nikimaliza swala yangu ya Tahjudd Alfajir nayo inakuwa imeingia.Je inawezekana kufanya hivyo?Wabilah taufiq.

 

 


 JIBU:

Sifa zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum)  na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Ibada ya Swalah, ni kati ya ibada zilizowekewa nyakati maaluum,

Anasema Allah, "Hakika ya Swalah kwa Waislam ni faradhi iliyowekewa nyakati makhsusi" (An-Nisaa: 102)

Na anasema Ibnu Mas'uud (radhiya Allahu 'anhu) nilimuuliza Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni jambo gani linalopendwa zaidi na Mwenyeezi Mungu?  Akasema ni kuitekeleza ibada ya Swalah ndani ya wakati wake" Al-Bukhaariy Hadiyth Namba 527 na Muslim Namba 85.

Kwa maana hiyo unatakiwa uiswali kila Swalah katika wakati wake kama ulivyoainishiwa na Qur-aan na mafunzo sahihi ya Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ama sababu za kukusanya Swalah, kuiakhirisha, au kuiqadimisha, zimewekwa wazi katika vitabu vya fiqhi kama vile kuruhusiwa katika safari au wakati wa dhurufu fulani, lakini sio kwa kufanya ni kawaida ya Muislamu kwa ajili ya kufadhilisha Swalah ya Sunnah wakati ya fardhi ndio muhimu zaidi. 

Na Allah Anajua zaidi

 

 

Share