Kuswali Juu Ya Mazulia Yenye Nembo Za Misalaba Na Eneo Lenye Msalaba Ndani

 

Kuswali Juu Ya Mazulia Yenye Nembo Za Misalaba Na Eneo Lenye Msalaba Ndani

 

 

SWALI:

 

Assalaamu alaykum warahmatullaah,

 

Ni ipi hukumu ya kusali juu ya mazulia au misala ambayo ina alama au nembo za wazi-wazi za misalaba au sehemu ambayo unaielekea misalaba hiyo japo huna nia ya kuiadhimisha au kuikusudia? Nitafurahi kama nitapata rai za wanazuoni mbalimbali, makala zao, mitandao ambayo nitaweza kulipata suala hili kwa undani na kina zaidi.

Wassalaamu.

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Hili ni jambo ambalo halifai kwani nembo hizo kwanza zinawakilisha ushirikina wa ki-Naswaara ambao ni nembo ya utatu wao, na pili kuswali juu yake kutakushughulisha na utakosa unyenyekevu na khushuu.

 

Ama picha za misalaba ni jambo ambalo halifai kabisa kwani nembo hizo kwanza zinawakilisha ushirikina wa ki-Naswaara ambao ni nembo ya utatu wao, na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alichukizwa nayo popote alipoiona aliiondoshelea mbali. 

 

Hadiyth ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)   hakuacha abadan kitu chochote katika nyuma kilichokuwa na alama ya msalaba ila alikifuta”. 

Na katika usimulizi mwingine:  “Alivichanilia mbali” [Al-Bukhaariy]

 

 

Kufanya hivyo ni funzo kwamba misalaba ni vitu ambavyo vinaabudiwa badala ya Allaah na hivyo kuweko nyumbani jambo la kuchukiza na halina budi kuondoshwa. Kwa hiyo haipasi kabisa kuwekwa mahali popote ikiwa katika miswala au kokote kwengineko anapokuweko Muislamu.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share