Kupita Mbele Ya Mtu Anayeswali Ni Dhambi?
SWALI:
Je, mtu anapata dhambi akipita mbele ya mtu anayeswali?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Ni dhambi kupita mbele ya mtu anayeswali kutokana na hadithi nyingi zinazokataza jambo
)) َعنْ أَبِي جُهَيْمِ بْنِ الْحَارِثِ بْنِ الصِّمَّةِ الأَنْصَارِيِّ رضي الله عنهما قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم : لَوْ يَعْلَمُ الْمَارُّ بَيْنَ يَدَيْ الْمُصَلِّي مَاذَا عَلَيْهِ مِنْ الإِثْمِ ، لَكَانَ أَنْ يَقِفَ أَرْبَعِينَ ، خَيْراً لَهُ مِنْ أَنْ يَمُرَّ بَيْنَ يَدَيْهِ)) البخاري ومسلم
((Kutoka kwa Abu Juhaym bin Haarith bin Swummatil-Answaariy رضي الله عنهما ambaye alisema: Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم Angelijua mtu dhambi zake kupita mbele ya mwenye kuswali basi kusubiri kwake (asipite) arubaini ni kheri kwake kuliko kupita mbele yake)) Kasema Abu-Nassr: sijui kasema siku arubaini au miezi au miaka. Al-Bukhari na Muslim
Kwa hivyo utaona kwamba kukatazwa kwake kumetiliwa nguvu mno hata ikawa (kutokana na maelezo ya mpokeaji Hadithi) ni bora mtu kusubiri siku arubaini au miezi arubaini au miaka arubaini asipite mbele ya mtu anayeswali
Na haswa mwanamke ndio kabisa Swalah inakatika kabisa na itabidi irudiwe hiyo Swalah.
((عن أبي ذر رضي الله عنه: عن النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم قال: تُعادُ الصَّلاَةُ مِنْ مَمَرِّ الحِمَارِ، وَالمرْأةِ، وَالكَلْبِ الأسْوَدِ)) رواه ابن خزيمة في صحيحه
((Imetoka kwa Abi Dharr رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم kasema: Swalah irudiwe atakapopita mbele punda, na mwanamke, na mbwa mweusi )) Imepokelewa na Ibn Khuzaiymah katika Sahihi yake.
Kwa hiyo itakuwa dhambi kama mtu akifanya makusudi na kama imebidi apite mbele ya mtu mwenye kuswali basi bora aweke 'Sutra' (partition), kitu cha kutenganisha kikubwa
Na Allaah Anajua zaidi