027-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Kila Mtu Ana Jukumu La Kuchunga Atakaloulizwa

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

Hadiyth Ya 27

Kila Mtu Ana Jukumu La Kuchunga Atakaloulizwa

www.alhidaaya.com

 

 

عَنْ ابْنِ عُمَرَ (رضي الله عنهما) عَنْ النَّبِيِّ (صلى الله عليه و آله وسلم) قَالَ:  ((كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ،  وَالأمِيرُ رَاعٍ،  وَالرَّجُلُ رَاعٍ عَلَى أَهْلِ بَيْتِهِ، وَالْمَرْأَةُ رَاعِيَةٌ عَلَى بَيْتِ زَوْجِهَا وَوَلَدِهِ، فَكُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ)) متفق  عليه

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله  عنهما)   kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Nyote ni wachunga na kila mmoja wenu ataulizwa kuhusu alichokichunga. Kiongozi ni mchunga, na mume ni mchunga juu ya mkewe na mke ni mchunga juu ya nyumba ya mumewe na watoto wake. Kwa hivyo nyote ni wachunga na kila mmoja wenu ataulizwa kuhusu alichokichunga)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

 

1. Kila Muislamu analo jukumu lake ambalo ni limekuwa ni amana kwake kuichunga. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

إِنَّا عَرَضْنَا الْأَمَانَةَ عَلَى السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَالْجِبَالِ فَأَبَيْنَ أَن يَحْمِلْنَهَا وَأَشْفَقْنَ مِنْهَا وَحَمَلَهَا الْإِنسَانُ ۖ إِنَّهُ كَانَ ظَلُومًا جَهُولًا ﴿٧٢﴾

Hakika Sisi Tulihudhurisha amana kwa mbingu na ardhi na majabali vikakataa kuibeba na vikaiogopa; lakini insani akaibeba. Hakika yeye amekuwa dhalimu mno, jahili mno. [Al-Ahzaab (33: 72)]

 

 

 

2. Jukumu ni amana na kila Alitochuruzuku Allaah (سبحانه وتعالى) ni neema kwetu, ikiwa ni mali au mke, au mume, au watoto, au elimu, na kila mmoja ataulizwa kuhusu neema hizo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ ﴿٨﴾

Kisha bila shaka mtaulizwa Siku hiyo kuhusu kuhusu neema. [At-Takaathur: 8]

 

 

 

3. Kutimiza amana ni miongoni mwa sifa zitakazompatia Muislamu Jannah ya Firdaws kama zilivyotajwa katika Suwrah: Al-Muuminuwn (23: 1-11)  

 

 

4. Mume na mke washirikiane katika malezi ya watoto ili watoto wakuwe na kuinukia katika maadili mazuri ya Kiislamu.

 

 

5. Mwanamke wa Kiislamu ana cheo kikubwa kwa kuwa ana jukumu kubwa la ulezi wa nyumba yake, na ameahidiwa kupata Jannah.

 

Rejea Hadiyth namba (26).

 

 

6. Kutimizia amana au jukumu ni jambo mojawapo la kumwezesha mtu kuvuka As-Swiraatw Siku ya Qiyaamah

 

Hadiyth: ((...na zitatumwa amana na ar-rahm [fuko la uzazi; uungaji udugu], navyo vitasimama pembeni ya Swiraatw kuliani na kushotoni…..))].[Muslim]

 

 

 

 

Share