028-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Kuvumiliana Tabia Mbaya Katika Maisha Ya Ndoa Kwa Kukumbuka Tabia Zilizo Nzuri

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

Hadiyth Ya 28

Kuvumiliana Tabia Mbaya Katika Maisha Ya Ndoa Kwa Kukumbuka Tabia Zilizo Nzuri

www.alhidaaya.com

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((لاَ يَفْرَكْ مُؤْمِنٌ مُؤْمِنَةً إِنْ كَرِهَ مِنْهَا خُلُقًا رَضِيَ مِنْهَا آخَرَ))  مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Muumin [mume] asimchukie Muumin [mke]. Asipompendelea kwa tabia fulani ataridhika naye kwa tabia nyingine)) [Muslim]

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Hakuna binaadamu aliyekamilika kwa tabia njema. Kila mmoja ana kasoro zake; huenda zikawa ni tabia zinazolingana; nzuri au mbaya. 

 

 

2. Kuishi pamoja kunadhihirisha tabia baina ya watu.

 

 

3. Inapasa kuvumiliana katika maisha ya ndoa, kwani kila mmoja ni mtihani kwa mwenziwe. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَجَعَلْنَا بَعْضَكُمْ لِبَعْضٍ فِتْنَةً أَتَصْبِرُونَ ۗ وَكَانَ رَبُّكَ بَصِيرًا ﴿٢٠﴾

Na Tumejaalia baadhi yenu nyinyi kwa nyinyi kuwa ni majaribio je mtasubiri? Na Rabb wako ni Mwenye kuona daima. [Al-Furqaan: 20]

 

 

4. Uislamu unamsisitiza mume kumfanyia wema mke.

 

Rejea: An-Nisaa (4: 19).

 

Rejea pia Hadiyth namba (29).

 

 

5. Hadiyth hii ni suluhisho mojawapo la kutatua matatizo baina ya mume na mkewe.

 

Rejea An-Nisaa (4: 128).

 

 

6. Inasisitizwa Muislamu kuchagua mke mwema, kwani ndio sababu ya furaha yake duniani na Aakhirah.

 

Rejea Hadiyth namba (35), (40).

 

 

7. Hii Hadiyth inamtaka mume awe makini wala asichukue hatua za haraka kama talaka ambayo huenda ikamletea majuto.

 

Share