075-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Mwenye Kuakhirishia Au Kusamehe Deni, Atakuwa Katika Kivuli Cha Allaah Siku Ya Qiyaamah

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 75

 

Mwenye Kuakhirishia Au Kusamehe Deni,

Atakuwa Katika Kivuli Cha Allaah Siku Ya Qiyaamah

 

Alhidaaya.com

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ أَنْظَرَ مُعْسِرًا أَوْ وَضَعَ لَهُ، أَظَلَّهُ اللَّهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ تَحْتَ ظِلِّ عَرْشِهِ يَوْمَ لاَ ظِلَّ إِلاَّ ظِلُّهُ)) رواه الترمذي وقَال حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ

 

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه)  ambaye amesema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه  وآله وسلم ) amesema: ((Atakayemuakhirishia mwenye usiri [wa kulipa deni] au akamsamehe, Allaah Atamfunika kivuli Siku ya Qiyaamah chini ya kivuli cha ‘Arshi Yake, Siku ambayo hakutakuwa na kivuli isipokuwa kivuli Chake)). [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

 

1. Uislamu unafunza kuoneana huruma katika hali ya dhiki kama kumsamehe mtu deni lake.

 

 

2.  Himizo la kusameheana deni, ima kuakhirisha wakati wake ulioahidiwa au kulisamehe lote. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

 

وَإِن كَانَ ذُو عُسْرَةٍ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيْسَرَةٍ ۚ وَأَن تَصَدَّقُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٨٠﴾

Na ikiwa (mdaiwa) ni mwenye hali ngumu, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na mkifanya deni kuwa ni swadaqah basi ni kheri kwenu mkiwa mnajua. [Al-Baqarah (2: 280)]

 

 

 

3. Fadhila kwa aliye na wasaa wa mali kusamehe deni kupata malipo mema Aakhirah na hiyo ni sifa ya Muhsin na kughufuriwa dhambi.

 Rejea: Aal ‘Imraan (3: 134), An-Nuwr (24: 22).

 

 

Pia Hadiyth ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

 

عن حذيفة عن رسول الله صلى الله عليه وسلم  أنه قال: ((أُتِيَ اللهُ بِعَبْدٍ مِنْ عَبِيدِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ قَالَ: مَاذَا عَمِلْتَ لِي فِي الدُّنْيَا؟ فَقَالَ: مَا عَمِلْتُ لَكَ يَا رَبِّ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ فِي الدُّنْيَا أَرْجُوكَ بِهَا،  قَالَهَا ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، قَالَ الْعَبْدُ عِنْدَ آخِرِهَا: يَا رَبِّ إِنَّكَ كُنْتَ أَعْطَيْتَنِي فَضْلَ مَالٍ، وَكُنْتُ رَجُلًا أُبَايِعُ النَّاسَ، وَكَانَ مِنْ خُلُقِي الْجَوازُ، فَكُنْتُ أُيَسِّرُ عَلَى الْمُوسِرِ وَأُنْظِرُ الْمُعْسِرَ، قَالَ: فَيَقُولُ اللهُ عَزَّوَجَلَّ: أَنَا أَحَقُّ مَنْ يُيَسِّرُ، ادْخُلِ الْجَنَّة))

Hudhayfah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Siku ya Qiyaamah, mmoja wa waja wa Allaah ataitwa mbele Yake na Atamuuliza: Umefanya ‘amali gani kwa ajili yangu katika maisha yako? Atajibu: Ee Rabb wangu! Sikuwahi katika uhai wangu kufanya ‘amali kwa ajili Yako iliyo sawa na chembe ndogo! (Ataulizwa na atajibu) Mara tatu, kisha mara ya tatu atasema: Ee Rabb wangu! Ulinijaalia mali na nilikuwa nafanya biashara. Nilikuwa mpole, nikiwapa masharti mepesi wenye uwezo na nikiwapa muda wa kulipa wadaiwa. Allaah Atamwambia: Mimi Ndiye Mwenye haki zaidi ya kutoa masharti mepesi kwa hiyo, ingia Jannah!)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

4. Malipo yanalingana, kama ilivyo, kwamba mwenye deni anapomuondoshea dhiki mwenziwe duniani ya kulipa deni, naye pia Allaah (سبحانه وتعالى) Atamuondoshea dhiki Aakhirah.

 

Rejea Hadiyth namba (23).

 

 

5. Kuakhirisha au kusamehe deni ni mojawapo wa fadhila za kujipatia kivuli cha Allaah (سبحانه وتعالى) Siku ambayo jua litakuwa karibu mno na joto lake halitoweza kuvumilika.

 

Rejea Hadiyth namba (43). 

 

Na Hadiyth ifuatayo:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ   ((سَبْعَةٌ يُظِلُّهُمْ اللَّهُ فِي ظِلِّهِ يَوْمَ لا ظِلَّ إِلا ظِلُّهُ: الإِمَامُ الْعَادِلُ، وَشَابٌّ نَشَأ فِي عِبَادَةِ رَبِّهِ، وَرَجُلٌ قَلْبُهُ مُعَلَّقٌ فِي الْمَسَاجِدِ، وَرَجُلَانِ تَحَابَّا فِي اللَّهِ اجْتَمَعَا عَلَيْهِ وَتَفَرَّقَا عَلَيْهِ، وَرَجُلٌ طَلَبَتْهُ امْرَأَةٌ ذَاتُ مَنْصِبٍ وَجَمَالٍ فَقَالَ إِنِّي أَخَافُ اللَّهَ، وَرَجُلٌ تَصَدَّقَ بِصَدَقَةٍ فَأَخْفَاهَا حَتَّى لا تَعْلَمَ شِمَالُهُ مَا تُنْفِقُ يَمِينُهُ، وَرَجُلٌ ذَكَرَ اللَّهَ خَالِيًا فَفَاضَتْ عَيْنَاهُ)) متفق عليه

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Watu saba Allaah Atawafunika katika kivuli Chake, Siku ambayo hakutokuwa na kivuli ila kivuli Chake: (i) Imaam (kiongozi) muadilifu. (ii) Kijana ambaye amekulia katika ibaada ya Rabb wake. (iii) Mtu ambaye moyo wake umeambatana na Misikiti (iv) Watu wawili wanaopendana kwa ajili ya Allaah; wanakutana kwa ajili Yake na wanafarikiana kwa ajili Yake. (v) Mwanamme aliyetakwa na mwanamke mwenye hadhi na mrembo wa kuvutia akasema: Mimi namkhofu Allaah! (vi) Mtu aliyetoa swadaqa yake akaificha hadi kwamba mkono wake wa kushoto usijue nini ulichotoa mkono wake wa kulia. (vii) Mtu aliyemdhukuru Allaah kwa siri macho yake yakatokwa machozi.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

6. Muumin anapaswa ajiepushe na uchoyo, ubakhili wa nafsi na badala yake kuwapendelea wenziwe wapate anachokihitajia yeye, ili apate kuwa miongoni mwa watakaofaulu.

 

Rejea:  At-Taghaabun (64: 16).

 

Pia kisa cha Abuu Twalhah na Ummu Sulaym Rumayswaa’ bint Milhaan walipopata wageni wakawakirimu ilhali wao walikuwa wana njaa, Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha Aayah kama ilivyotajwa katika Hadiyth ifuatavyo:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، ‏.‏ أَنَّ رَجُلاً، مِنَ الأَنْصَارِ بَاتَ بِهِ ضَيْفٌ فَلَمْ يَكُنْ عِنْدَهُ إِلاَّ قُوتُهُ وَقُوتُ صِبْيَانِهِ فَقَالَ لاِمْرَأَتِهِ نَوِّمِي الصِّبْيَةَ وَأَطْفِئِي السِّرَاجَ وَقَرِّبِي لِلضَّيْفِ مَا عِنْدَكِ - قَالَ - فَنَزَلَتْ هَذِهِ

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba mtu alilala usiku kama mgeni kwa mtu mmoja katika Answaariy ambaye hakuwa na chakula isipokuwa chakula cha watoto wake akamwambia mkewe: “Laza watoto na zima taa karibisha wageni kwa (chakula) ulichonacho.” Ikateremka kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

  وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿٩﴾

  

Na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wanahitaji. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu. [Al-Hashr (59: 9)]

  

 

 

 

 

 

 

 

 

Share