076-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Balighisheni Japo Kwa Aayah, Atakayemwongopea Nabiy Ajitayarishie Makazi Motoni

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

 

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 76

 

Balighisheni  Japo Kwa Aayah Moja, Atakayemwongopea Nabiy Ajitayarishie Makazi Yake Motoni

 

 

 

 عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو العَاص (رضي الله عنهما) أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((بَلِّغُوا عَنِّي وَلَوْ آيَةً،  وَحَدِّثُوا عَنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلاَ حَرَجَ، وَمَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنْ النَّارِ)) البخاري

 

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr Al-‘Aasw (رضي الله عنهما)   kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Balighisheni (fikisheni) kutoka kwangu japo Aayah moja. Na simulieni kuhusu habari za Wana wa Israaiyl wala hakuna dhambi [ubaya]. Na mwenye kunizulia uongo kwa makusudi, basi ajiandalie makazi yake motoni)). [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Umuhimu wa kubalighisha ujumbe, kuamrishana mema na kukatazana maovu japo kwa Aayah moja au Hadiyth moja.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ

Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. [Aal-‘Imraan (3: 110)]

 

Rejea pia: Aal-‘Imraan (3: 104),   At-Tawbah (9: 71), (112), Al-Hajj (22: 41).

 

          

2. Umuhimu wa kutafuta na kujifunza elimu sahihi ili kutokubalighisha Hadiyth dhaifu au mambo ya uzushi.

 

 

 

3. Kuruhusiwa kusimulia habari za Wana wa Israaiyl ili kupata mafunzo na mazingatio, ila la muhimu ni kuhakikisha kama masimulizi yamethibiti usahihi wake.

 

 

 

4. Kuzusha yasiyo sahihi ni miongoni mwa madhambi makubwa kwa vile yanamfikisha mtu motoni, kwa hiyo inapasa kutahadhari mno! Hadiyth ifuatayo inataja hatari hizo ambazo zinampeleka mtu kwenye upotofu kwanza kisha motoni.

 

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ فِي خُطْبَتِهِ يَحْمَدُ اللَّهَ، وَيُثْنِي عَلَيْهِ بِمَا هُوَ أَهْلُهُ، ثُمَّ يَقُولُ: مَنْ يَهْدِهِ اللَّهُ فَلَا مُضِلَّ لَهُ وَمَنْ يُضْلِلْهُ فَلَا هَادِيَ لَهُ إِنَّ أَصْدَقَ الْحَدِيثِ كِتَابُ اللَّهِ وَأَحْسَنَ الْهَدْيِ هَدْيُ مُحَمَّدٍ وَشَرُّ الْأُمُورِ مُحْدَثَاتُهَا وَكُلُّ مُحْدَثَةٍ بِدْعَةٌ وَكُلُّ بِدْعَةٍ ضَلَالَةٌ وَكُلُّ ضَلَالَةٍ فِي النَّارِ...)) مسلم، أبو داود، النسائي، ابن ماجه، أحمد، الدارمي

 

Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه)  ambaye amesema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  alikuwa akisema katika khutbah zake: ((Yule ambaye Allaah Amemhidi, hakuna wa kumpotoa, na yule ambaye Allaah Amempotoa hakuna wa kumhidi. Hakika maneno ya kweli kabisa ni Kitabu cha Allaah, na mwongozo mbora kabisa ni wa Muhammad, na jambo la shari kabisa ni uzushi, na kila jambo jipya (katika Dini) ni bid'ah (uzushi) na kila bid'ah ni upotofu, na kila upotofu ni motoni)) [Muslim, Abuu Daawuwd, An-Naasaaiy, Ibn Maajah, Ahmad, Ad-Daarimiy]

 

 

 

5. Mwenye hadhari na khofu ya kuzusha mafunzo yasiyo sahihi na kumzulia uongo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), anadhihirisha wazi mapenzi yake kwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), kwani hakuna apendaye kumzulia uongo kipenzi chake.

 

 

 

6. Dalili kadhaa kutoka katika Qur-aan na Sunnah zimetaja maamrisho na fadhila za kubalighisha kwa kuamrishana mema na kukatazana maovu na kulingania kwa ujumla (da’wah). Na kinyume chake ni kukemewa na kutahadharishwa na adhabu kwa anayepuuza.

 

 

عن حُذيفةَ بنِ اليَمانِ عن النَّبيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلِيهِ وسَلَّم قال: ((والَّذي نَفْسي بيدهِ لتأمرُنَّ بالمعروفِ ولتَنهوُنَّ عن المنكرِ وليوشِكَنَّ اللهُ أنْ يبعثَ عليكُمْ عقاباً منهُ فتدعونَهُ فلا يَستجيبُ لكُمْ)) الترمذي وصححه الألباني

Imepokelewa toka kwa Hudhayfah bin al-Yamaani  (رضي الله عنه) kutoka kwa Nabiy kwamba amesema: ((Naapa kwa Yule nafsi yangu ipo mikononi mwake, mtaamrishana ma’ruwf [mema] na kukatazana munkari [maovu] ama Atawaunganishia kwa kuwapa mfano wake Allaah na kuwateremshia nyinyi adhabu itokayo Kwake, kisha mumuombe Yeye na Asiwajibu du’aa zenu)) [At-Tirmidhiy na akaisahihisha Al-Albaaniy]

 

 

Rejea pia Hadiyth namba (16), (17),

 

Rejea pia utangulizi wa hizi Hadiyth.

 

 

Share