094-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Kuweka Amani Baina Ya Watu Kwa Ulimi Na Kuacha Yaliyoharamishwa

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

 

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 94

 

Kuweka Amani Baina Ya Watu Kwa Ulimi Na Kuacha Yaliyoharamishwa

 

 

 

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو (رضي الله عنهما) قَال: قَال رَسُولُ الله صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((الْمُسْلِمُ مَنْ سَلِمَ الْمُسْلِمُونَ مِنْ لِسَانِهِ وَيَدِهِ  وَالْمُهَاجِرُ مَنْ هَجَرَ مَا نَهَى اللَّهُ عَنْهُ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah in ‘Amr (رضي الله عنهما) ambaye amesema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Muislamu ni yule anayeweka amani kwa watu [ambaye Waislamu wenziwe wanasalimika] kwa ulimi na mkono wake. Na mhamaji ni yule anayehama Aliyoyakataza Allaah)).  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Uislamu asili yake ni ‘amani’ na hata maamkizi yetu ni ya amani. 

 

Rejea Hadiyth namba (72).

 

 

2. Himizo la kuepusha kila maudhi baina ya Waislamu kwa kila njia, kwa maneno maovu, kuumizana au kupigana.

 

Rejea Hadiyth namba (22), (87), (88), (89), (93), (126).

 

 

3. Aayah na Hadiyth nyingi zimetaja yanayohusiana na mambo yaliyoharamishwa na Allaah (سبحانه وتعالى).

 

Rejea Hadiyth namba (139).

 

Na baadhi ya mambo ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Ameyaharamisha:

 

 

 قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۖ وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُم مِّنْ إِمْلَاقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ ۖ وَلَا تَقْرَبُوا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ ۖ وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١٥١﴾

Sema: “Njooni nikusomeeni yale Aliyoyaharamisha Rabb wenu kwenu. Kwamba msimshirikishe na chochote, na muwafanyie ihsaan wazazi wawili, na wala msiwaue watoto wenu kutokana na umasikini. Sisi Tunakuruzukuni pamoja nao. Na wala msikaribie machafu yaliyo dhahiri na yaliyofichika. Na wala msiue nafsi ambayo Ameiharamisha Allaah (kuiua) isipokuwa kwa haki (ya shariy’ah). Hivyo ndivyo Alivyokuusieni kwayo mpate kutia akilini.” [Al-An’aam (6: 151)]

 

Baadhi ya maharamisho hayo yanaendelea kutajwa hadi Aayah namba 153.

 

 

4. Himizo la kuacha kila aina ya maasi.

 

 

5. Kuhama kumelinganishwa na kuacha maasi, kwa vile si jambo jepesi kulitenda, na maasi pia ni jambo gumu, kwani si wepesi kuacha matamanio yake mtu na si wepesi kumwepuka shaytwaan.

 

 

 

Share