Shaykh 'Abdul-'Aziyz Ar-Rajihiy: Namna Ya Kujikinga Kunapotokea Fitnah
Namna Ya Kujikinga Kunapotokea Fitnah
Amesema
Shaykh 'Abdul-'Aziyz Ar-Rajihiy (Hafidhwahu-Allaah)
Katika wakati wa fitnah, ni waajib Muislamu kufanya yafuatayo:
1. Kujishughulisha na kutafuta elimu ya Dini.
2. Kujishughulisha na kumuabudu Allaah (Tabaaraka wa Ta'alaa); mambo haya yatamlinda na fitnah.
Kadhaalika, kujikinga na fitnah kunapatikana kwa kufanya yafuatayo:
1. Kushikamana na Qur-aan na Sunnah.
2. Kujishughulisha sana na kumfanyia 'Ibaadah Allaah (Tabaaraka wa Ta'alaa)
3. Kuwa na ukaribu na maingiliano na watu wema.
4. Kukaa mbali na watu waovu.
5. Kujiweka mbali na maeneo maovu, na vilevile kujiweka mbali na mambo yenye kupelekea katika maovu.
Shaykh 'Abdul-'Aziyz Ar-Rajihiy (Hafidhwahu-Allaah),
Sharh Uswuwl As-Sunnah, uk. 147.