Imaam Ash-Sha'biy - Sijui!!
Sijui!!
Aliulizwa Imaam Ash-Sha'biy (Rahimahu Allaah) kuhusiana na mas-alah (katika Dini), akajibu: 'Sijui'
Akaambiwa: 'Je, hustahi kusema, 'Sijui'? Na wewe ni Faqiyh wa watu wa 'Iraaq?
Akajibu (Rahimahu Allaah): 'Lakini Malaika hawakustahi pindi waliposema:
{{...Hatuna elimu isipokuwa Uliyotufunza...}}!
[I'laam Al-Muwaqi'iyn, juz. 4, uk. 167-168]
