Shaykh Bakr Abuu Zayd - Khiyaanah! Haifai Kumrekodi Mtu Kwenye Simu Bila Idhini Yake Wala Yeye Kujua

 

Khiyaanah! Haifai Kumrekodi Mtu Kwenye Simu Bila Idhini Yake

 

www.alhidaaya.com

 

 

Shaykh Bakr Abuu Zayd, mjumbe wa Baraza la Wanachuoni Wakubwa (Rahimahu Allaah) amesema:

 

“Haijuzu Muislamu anayechunga amana na anayechukia khiyaanah, kurekodi mazungumzo ya Mzungumzaji (bila idhini yake wala yeye kujua) kwa namna yoyote ya mazungumzo yatakayokuwa; ya Kidini au ya Kidunia, kama vile fatwa, au utafiti wa kielimu au (mas-alah yanayohusu) mali, na yanayojiri mfano wa hayo.

 

Akaendelea (Rahimahu Allaah):

“Na ukirekodi mazungumzo yake bila idhini yake, basi hiyo ni hila na udanganyifu na khiyaanah kwa amana.

Na endapo utaeneza hayo mazungumzo, basi hiyo ni ziada katika kufanya khiyaanah na kuvunja amana kwa kuifichua.

 

Kwa kifupi:

Kurekodi mazungumzo, sawa iwe kwa simu au kwa njia nyingine isiyo ya simu (bila idhini ya mzungumzaji wala yeye kujua), basi huo ni uovu, dhulma, na khiyaanah. Hafanyi hilo isipokuwa Yule mwenye uchache wa dini (dini finyu) na akhlaaq duni na adabu (mbovu).

Basi mcheni Allaah na msikhini amana zenu, na wala msiwasaliti ndugu zenu.”

 

[Adab Al-Haatif, uk. 28-29]

 

Share