Sifa Gani Za Kutafuta Mke?
SWALI:
asalaam aleykum
mimi naomba kuuliza lifuatalo
.naimba mnisaidie kunitajia sifa au jinsi ya kuchagua mchumba
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukran kwa swali lako
Ndoa ni jambo ambalo limepatiwa kipaumbele na Uislamu kwa kuwa ni Sunnah ya Manabii na Mitume na watu wema. Ndoa ni maumbile ambayo mwanadamu amepatiwa na Allah Aliyetukuka. Katika Uislamu hakuna utawa na kujitenga na majukumu ya kimaisha na kujenga jamii. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika Allah ametubadilishia utawa kwa Uislamu ulionyooka” (al-Bayhaqiy). Pia amesema: “Nami naoa wake, mwenye kukengeuka na Sunnah yangu basi si katika mimi” (al-Bukhaariy na Muslim).
Ndoa ni maslahi ya kijamii, hivyo ina faida nyingi. Miongoni mwayo ni:
1. Kuhifadhi jinsi ya mwanadamu:
Kwa ndoa wanadamu wanaendelea kubakia katika mgongo wa ardhi. Allah Aliyetukuka Anasema: “Na Allah Amekuumbieni wake katika jinsi yenu, na Akakujaalieni kutoka kwa wake zenu watoto na wajukuu” (16: 72).
2. Kuhifadhi nasaba za watu.
3. Kusalimika jamii kutoka kupotoka kimaadili: Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwahimiza
4. Jamii kusalimika na magonjwa:
Magonjwa ya zinaa ni natija ya kuliendea jambo hili la kushibisha matamanio kwa njia ya haramu. Magonjwa haya ni hatari na ukimwi haujapatikana tiba hadi sasa, tahadhari usije ukapata adhabu mara mbili. AIDS ni gonjwa hatari mno.
5. Utulivu wa kiroho na kinafsi:
Ndoa inaleta mapenzi, upole, ulaini na rehema. Allah Aliyetukuka Anasema: “Na katika Ishara Zake ni kuwa Amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mupate utulivu kwao, Naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaofikiri” (30: 21).
6. Kushirikiana baina wanandoa katika kujenga familia na kuwalea watoto:
Kwa ndoa wanashirikiana wanandoa katika kujenga familia ya Kiislamu na kubeba majukumu hayo.
Ama kuhusu sifa njema na nzuri ambazo kwayo mwanamme anafaa achague mkewe na mwanamke naye achague mumewe ni
Kuchagua kwa msingi wa Dini:
Huu ni msingi wa kwanza na muhimu
Amesema tena: “Akikujieni ambaye mumeridhika na dini na maadili yake, muozesheni. Msipofanya hivyo kutakuwa na fitna katika ardhi na ufisadi mkubwa” (at-Tirmidhiy).
Amesema tena (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Mwenye kumuoa mwanamke kwa sababu ya
Kufadhilisha mwanamke mwenye kuzaa:
Alikuja mtu kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza: “Ewe Mtume wa Allah mimi nampenda mwanamke mwenye nasaba nzuri, cheo na
Na Allah Anajua zaidi