Imaam Ibn Taymiyyah: Watu Wa Bid'ah Ni Waovu Kuliko Watu Wa Maasi

Watu Wa Bid'ah Ni Waovu Kuliko Watu Wa Maasi

Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah

www.alhidaaya.com

 

 

Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

 

 

"Watu wa bid'ah ni waovu zaidi kuliko watu wa maasi kwa mujibu wa Sunnah na Ijmaa'.
Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamrisha kupigana na Khawaarij wakati ambapo kakataza kupigana na Watawala dhalimu.
Na yeye (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema kumhusu yule mtu aliyekuwa akinywa pombe, "Msimlaani, hakika yeye anampenda Allaah na Rasuli Wake," wakati ambapo alisema kumhusu Dhul Khuwaysirah, "Watatoka katika kizazi cha mtu huyu, watu ambao watasoma Qur-aan lakini haitovuka koo zao.” Katika riwaayah nyengine: “Watatoka katika Uislamu”.. kama mshale unavyopenyeza na kutoka kwenye kiwindwa..."

 

[Majmuw' Al-Fataawaa, mj. 20, uk. 103]

 

Share