Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Shikamana Na Haki Usibadili Msimamo Hata Kama Watu Wengi Wanakupinga

 
Shikamana Na Haki, Usibadili Msimamo Hata Kama Watu Wengi Wanakupinga
 
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
 
 
 
 
Imaam Muhammad bin Swaalih Al-'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) wakati akizungumzia kuhusu kushikamana na Haki alisema,
 
“Shikamana imara na msimamo na usibadilishe msimamo kwa kuwa watu wengi wanakushambulia, au wanakasirishwa na maneno yako.
 
Maadam uko kwenye Haki, basi shikamana nayo na kuwa na msimamo, kwani Haki haishindwi (Na Baatwil).
Kwa hiyo, pigania (Haki) hata katika hali ya udhaifu (uko peke yako).
 
Hakuna zaidi ya kutetea Haki.
 
Lakini ukiwa katika hali ya uimara, basi usiache kuipiga vita (Baatwil).
Kwa kuwa siku zinabadilika (kuna wakati siku zinakuwa upande wako, na kuna zenye kuwa kinyume nawe).
 
Lakini kumbuka kitu muhimu hata pale katika wakati mgumu na udhaifu, usiyumbe wala kutetereka na shikamana na Haki. Na daima usiseme: ‘Ah, watu wote wanapingana na hili (ninalolisimamia). Bali, kuwa na msimamo, kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anailinda Dini Yake, Kitabu Chake, Mtume Wake katika zama zote.
 
Hakuna shaka utapata madhara kutoka kwa watu. Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah), alifungwa na kuburutwa na Nyumbu katikati ya soko na huku akipigwa. Lakini alisubiri na kubaki imara (hakutetereka).
 
Na Shaykh Al-Islaam (Ibn Taymiyyah, Rahimahu Allaah), alipitishwa katikati ya soko ndani ya rikwama  na akasekwa jela, lakini alibaki imara (akishikamana na misimamo yake).
 
Haiwezekani katika hii Dunia kuwa daima kama zulia la mawaridi na maua kwa mtu ambaye anataka kushikamana na Sunnah (ajue atapata upinzani na kudhuriwa na watu).”
 
[Sharh ya An-Nuwniyyah ya Ibn Al-Qayyim, iliyoshereheshwa na Imaam Ibn Al-`Uthaymiyn (3/270)]
 
Share