Waliofanya Zinaa Wanaweza Kuoana?
SWALI:
Walioanza kufanya zinaa kabla ya ndoa, wakitaka kuoana wanaruhusiwa?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho
Watu hao wawili wanaruhusiwa kuoana baada ya kukamilisha masharti fulani. Sharti muhimu sana ni kujuta kwa kitendo hicho na kuomba msamaha (tawbah) kwa kufanya hivyo na aazimie kutorudia tena, na lau kungekuwa na dola ya Kiislamu basi angejipeleka ili ahukumiwe, na pia kufanya mambo mazuri kwani Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Mche Allah popote pale ulipo. Na fuatisha baya kwa zuri nalo litalifuta
Na baada ya kufanya hivyo hawatakiwi kukaa pamoja na wale wasifanye kitendo hicho mara nyingine. Wanatakiwa wawe mbali kwa muda wa miezi mitatu ili kuhakikisha
“Mzinifu haolewi ila na mwanamume mzinifu au mshirikina. Na hayo ya. Mwanamume mzinifu hamwoi ila mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina. Na mwanamke meharimishwa kwa Waumini” (24: 3).
Tanbihi: Uislamu umefanya ndoa kuwa ni nyepesi kutekelezeka hivyo ni kwa vijana na wasichana wasijipeleke katika mambo ambayo yanaleta matamanio badala yake waoane na hili linapunguza mengi na pia kujiondoa na mengi yaliyo machafu na ya uasherati. Na Mtume ametupatia kinga pale alipowahutubia vijana:
“Enyi kongamano la vijana! Yule mwenye uwezo wa kuoa na afanye hivyo, kwani
Kwa maelezo zaidi, tafadhali soma majibu yalioko katika viungo vifuatavyo:
Wazinifu Waliotubu Wanaweza Kufunga Ndoa Na Waliotakasika