Shairi La الحَائِيَّة (Al-Haaiyyah) La Ibn Abiy Daawuwd

 

Shairi La الحَائِيَّة (Al-Haaiyyah)  Katika 'Aqiydah Ya Sunnah La

Imaam Abuu Bakr Bin Abiy Daawuwd As-Sijistaaniyy

 

المَنظُومَةُ الحَائِيَّة في السُّنَّة

لِأَبِي بَكْر بْنِ أَبِي دَاوُد السِّجِسْتَانِيِّ

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Shairi la Al-Haaiyyah (linaloishia na herufi ya  ح (Ha) ni shairi la kisunni na ni shairi zuri sana lilotungwa na Al-Haafidhw Abuu Bakr bin Abiy Daawuwd As-Sijistaaniy.

 

Shairi hilo lenye beti 36 limekusanya masuala ya msingi yanayohusu ‘Aqiydah ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah (Salafiyyah), na ambalo linabainisha tofauti baina ya Ahlus-Sunnah na wapinzani wake ambao ni Ahlul-Bid’ah.

 

Mtunzi kabainisha ndani ya shairi hilo, itikadi iliyo sahihi na kasisitiza kushikamana na Kitaabu (Qur-aan) na Sunnah, na kahadharisha bid’ah na watu wake.

 

Akabainisha vilevile kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah na si kiumbe, na kuwa kumuona Allaah Qiyaamah ni jambo la uhakika lisilo na shaka.

 

Akathibitisha ndani ya shairi hilo, Sifa za Allaah ambazo Amejisifu nazo Yeye kwa nafsi Yake.

 

Akabainisha fadhila za Swahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Akabainisha kadhaalika, Iymaan juu ya Qadar na Siku ya Mwisho.

 

Akahadharisha kuhusu Khawaarij, na pia bid’ah ya Irjaa-a.

 

Akafafanua na kuelezea masuala ya Iymaan na akatoa wito wa kurejea katika Qur-aan na Sunnah na kujiepusha na kutumia na kutanguliza rai na maoni mbele ya Qur-aan na Sunnah.

 

 

 

Shairi La الحَائِيَّة (Al-Haaiyyah)  

Imaam Abuu Bakr Bin Abiy Daawuwd As-Sijistaaniyy

 

 

تَمسَّـكْ بحَـبْلِ اللهِ واتَّبِع الهُـدَى                    ولا تَـكُ بِدْعِيَّـاً لَعلَّـكَ تُفْلِــحُ

 

1- Shikamana na kamba ya Allaah na fuata uongofu, na wala usiwe mtu wa bid’ah bila shaka utafaulu.

 

 

 

وَدِنْ بِكِتَابِ اللهِ والسُّـنـَنِ التِـي                      أَتَتْ عَن رَسُولِ اللهِ تَنْجُ وَتَرْبَحُ

 

2- Na itekeleze Dini kwa (kufuata) Kitabu cha Allaah na Sunnah ambazo, zimekuja kutoka kwa Rasuli wa Allaah utaokoka na utapata faida.

 

 

 

وَقُـلْ غَيْـرُ مَخْلِوقٍ كَلامُ مَليكِنا                بِـذَلكَ دَانَ الأتْقِياءُ وأَفْصحُــوا

 

3- Na sema si kiumbe maneno (Qur-aan) ya Mfalme wetu, kwa itikadi hiyo waliitekeleza Dini wachaji Allaah na kwa ufasaha wakaifikisha.

 

 

 

وَلا تَكُ فِي القُرْآنِ بالوَقْفِ قَائِــلاً                    كَمَا قَالَ أتْبَاعٌ لِجَهْمٍ وَأَسْجَحُوا

 

4- Na wala usiwe katika Qur-aan ni mwenye kusema kwa kusita, kama walivyosema wafuasi wa Jahm na Nyoyo zao zikaridhia hii itikadi mbaya.

 

 

 

ولا تَقُـلِ القُرآنُ خَـلقاً قـرأتَـهُ                          فإنَّ كَـلامَ اللهِ باللفْظِ يُــوضَحُ

 

5- Na wala usiseme kuwa Qur-aan ni kiumbe umekisoma, kwa hakika maneno ya Allaah kwa lafdhi yanawekwa wazi.

 

 

 

وَقُـلْ يَتَجلَّى اللهُ للخَلْقِ جَـهْـرةً                      كَمَا البدْرُ لا يَخْفى وَرَبُّكَ أَوْضَـحُ

 

6- Na sema Atajidhihirisha Allaah kwa viumbe kwa uwazi, kama mwezi mpevu haufichikani; na Rabb wako yuko wazi mno.

 

 

 

وَلَيْسَ بمْولُـودٍ وليسَ بِـوَالِــدٍ                          وَلَيسَ لهُ شِـبْهٌ تَعَالَى المسَبَّـحُ

 

7- Na si mzaliwa na wala si mzazi, na hana mfano yeye ametukuka mwenye kutakaswa.

 

 

 

وَقَـدْ يُنكِرُ الجَهْميُّ هَــذَا وعِنْدَنَا                     بِمِصْـدَاقِ ما قُلْنَـا حَدِيثٌ مُصَرِّحُ

 

8- Na kwa hakika anapinga hili Jahmiyyu na sisi tunayo, kwa kusadikisha yale tuliyoyasema Hadiyth iliyo wazi.

 

 

 

رَوَاهُ جَرِيـرٌ عـن مَقَـالِ مُحـمَّدٍ                           فقُـلْ مِثْلَ ما قَدْ قَالَ في ذَاكَ تَنْجَحُ

 

9- Ameipokea Jariyr kutoka katika maneno ya Muhammad, basi sema mfano wa kile alichokisema katika hilo utafaulu.

 

 

 

وَقَـدْ يُنكِـرُ الجَهْمِيُّ أَيضًا يَمِيْنَـهُ                       وَكِلْتَا يَدَيْـهِ بالفواضِـلِ تَنْفَـحُ

 

10- Na kwa hakika anapinga Jahmiyyu pia mkono Wake (Allaah) wa kulia, na mikono Yake yote miwili kwa kipao inatoa.

 

 

 

وَقُـلْ يَنْـزِلُ الجَبَّارُ فـي كُـلِّ لَيْلَةٍ                       بِلا كَيْف جَلَّ الواحدُ المتَمَـدِّحُ

 

11- Na sema anateremka Al-Jabbaar katika kila usiku, bila ya namna ametukuka Mmoja mwenye kusifiwa.

 

 

 

إلى طَبَـقِ الدُّنيا يَمُـنُّ بِفَضْلِــهِ                                 فَتُفْـرَجُ أَبْوابُ السَّـماءِ وتُفْتـحُ

 

12- Mpaka katika tabaka (mbingu) ya dunia Anatoa (Allaah) kwa fadhila Zake, na inaachwa wazi milango ya mbingu na inafunguliwa.

 

 

 

يَقولُ: ألا مُسْـتغفِـرٌ يَلْـقَ غَافِـرًا                       ومُسْـتَمنِحٌ خَـيْرًا ورِزقًا فأمْنَـحُ

 

13- Anasema:je, kuna mwenye kutaka maghfirah akutane na mwenye kughufuria, na mwenye kutaka khayr na rizki ili apewe.

 

 

 

رَوَى ذَاكَ قَـومٌ لا يُـرَدُّ حَــدِيثَهم                              ألا خَابَ قَــوْمٌ كذَّبـوهُم وقُبِّحُوا

 

14- Wamelipokea hilo watu ambao hazirudishwi Hadiyth zao, tambua, ni wenye kupata hasara watu ambao Wamewakadhibisha na wamelaaniwa.

 

 

 

 

وَقُـلْ إنَّ خَيْرَ النَّاسِ بَعْـدَ مُحَمَّـدٍ                             وَزِيـراهُ قُدْمًا، ثُمَّ عُثْمَانُ أرْجَـحُ

       

 

15- Na sema hakika mbora wa watu baada ya Muhammad, ni mawaziri wake wawili toka mwanzo kisha ‘Uthmaan Kwa kauli yenye nguvu.

 

 

 

 

وَرابِعُهُـم خَـيْرُ البريَّـةِ بَعْـدَهُـم                         عَلِـيٌّ حَليفُ الخَـيرِ، بالخَيرِ  مُنْجِح

 

 

16- Na wa nne wao ni mbora wa viumbe baada yao, ‘Aliy mwenye kulazimiana na khayr kwa khayr ni mwenye kufaulu.

 

 

 

وإنَّهمُ والرَّهْطُ لا رَيْــبَ فِيْهِــمُ                        عَلَى نُجُبِ الفِرْدَوْسِ في الخُلْدِ تَسْرَحُ  

 

 

 

17- Na hakika wao ni kundi ambalo hakuna shaka kwao wao, juu ya ubora na utukufu wa Firdaws wataelekea.

 

 

 

سَعِيدٌ وسَعْـدٌ وابنُ عَـوْفٍ وطَلْحـةٌ                          وعَامِرُ فِهْــرٍ والزُّبَيْـرُ المُمَـدَّحُ

 

18- Sa’iyd na Sa’d na Ibn ‘Awf na Twalhah, na ‘Aamir Fihrin na Az-Zubayr mwenye kusifiwa.

 

 

 

وَعَائِشُ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ وَخَالُنا                                مُعَاوِيَة أَكْرِمْ بِهِ فَهْوَ مُصلحُ

 

 

 

19- Na ‘Aaishah mama wa Waumini na mjomba wetu, Mu’aawiyyah mkirimu kwani yeye ni muswlihu.

 

 

 

وَأَنْصارُه وَالهَاجِرونَ دِيارَهم                                 بنصرهُمُ عَنْ ظلمةِ النَّارِ زحزحُوا

 

 

20- Na Answaar wake (Waislamu wa Madiynah) na Muhaajiruwn waliohama nyumba zao, kwa kunusuru kwao kutokana na kiza; Moto wameepushwa.

 

 

 

وَمَنْ بعدَهُم وَالتابِعُون بِحُسنِ مَا                            حَذو حَذوهم قَولاً وَفِعلاً فَأفْلحوا

 

 

 

21- Na waliokuja baada yao na Taabi’uwn waliowafuata kwa wema, wakafuata nyayo zao kwa maneno na matendo; wakafaulu.

 

 

 

 

وَقُلْ خَـيْرَ قولٍ في الصَّحَابةِ كُلِّهِـمْ                          ولا تَــكُ طَعَّاناً تَعِيْـبُ وَتَجْـرَحُ 

       

 

 

22- Na sema kauli nzuri kwa Swahaba wote, na wala usiwe mwingi wa kuwatukana unawatia aibu na unawajeruhi.

 

فَقَدْ نَطَقَ الوَحْيُ المُبينُ بِفَضْلِهِــمْ                           وفي الفَتْحِ آيٌ في الصَّحابةِ تَمْدَحُ

 

 

 

23- Na kwa hakika umetamka wahyi ulio wazi juu ya fadhila zao, na katika (Suwrat) Al-Fat-h kuna Aayah ambazo zinawasifu Swahaba.

 

 

 

 

وبِالقَـدَرِ المقْـدُورِ أيْقِنْ فإنَّهُ                                 دِعَامَةُ عقْدِ الدِّينِ والدِّينُ أفْيَـحُ       

 

24- Na kwa Qadar iliyokadiriwa kuwa na yakini hakika, hiyo Qadar ni nguzo ya Dini na Dini ni pana.

 

 

 

وَلا تُنْكِرَنْ جَهلاً نَكِيرًا ومُنْكَــراً                       وَلا الحوضَ والِميزانَ إنَّـكَ تُنْصَـحُ

 

 

25- Na wala usipinge kwa ujinga Nakiyr na Munkar, na wala hodhi na Miyzaan hakika wewe unanasihiwa.

 

 

 

وقُـلْ يُخْـرِجُ اللهُ العَظيمُ بِفَضلِـهِ                        مِن النارِ أجْسادًا مِن الفَحْمِ تُطْرَحُ   

 

 

26- Na sema Anatoa Allaah Mtukufu kwa fadhila Zake, Motoni miili ambayo inatokana na mkaa kisha Itatupwa.

 

 

 

عَلَى النَّهرِ في الفِردوسِ تَحْيا بِمَائِهِ                    كَحَبِّ حَميلِ السَّيْلِ إذْ جَاءَ  يَطْفَـحُ

 

27- Juu ya mto katika Firdaws itapata uhai kwa maji yake, kama vile mbegu iliyobebwa na mafuriko pindi yalipofurukuta.

 

 

فإنَّ رَسُـولَ اللـهِ للخَلـقِ شَافـعٌ                              وقُلْ فِي عَذابِ القَبرِ حـقٌّ مُوَضَّحُ              

 

28- Na kwa hakika Rasuli wa Allaah kwa viumbe ni mwenye kuwaombea, na sema kuhusu adhabu ya kaburi ni (jambo la) haki iliyo wazi.

 

 

 

ولا تُكْفِّرَنَّ أهْلَ الصَّلاةِ وإِنْ عَصَـوا          فكلُّهُمُ يَعْصِي وذُو العَرشِ يَصْفَـحُ

 

29- Na wala usiwakufurishe watu wenye kuswali hata kama wakiasi, kwani kila mwana Aadam anafanya maasi; na mwenye ‘Arshi Anasamehe.

 

 

 

ولا تَعتقِــدْ رَأيَ الخَوارجِ إنَّـهُ                          مَقَالٌ لِمَنْ يهـواهُ يُرْدِي ويَفْضَحُ    

 

30- Na wala usiitakidi rai ya Khawaarij kwani hayo, ni maneno ambayo mwenye kuyaitakidi yanamuangamiza na yanamfedhehesha.

 

 

 

ولا تَــكُ مُرْجِيـًّا لَعُوبًا بِدِينِـهِ                          ألا إنَّمَا المُرْجيُّ بالدِّينِ يَمْـزَحُ          

 

31- Na wala usiwe Murji-a mwenye kucheza na dini yake, fahamuni hakika si vinginevyo Murji-a wanaifanyia mzaha Dini.

 

 

 

وقُــلْ إنَّما الإيمانُ قـَوْلٌ ونيَّـةٌ                          وِفعْلٌ عَلَى قَـولِ النبيِّ مُصَرَّحُ

 

32- Na sema hakika si vinginevyo imani ni: kauli na niyyah, na kitendo juu ya kauli ya Nabiy iliyo wazi.

 

 

 

ويَنْقُصُ طَـوْرًا بالمعَاصِي وَتَـارةً                                      بطَاعَتِهِ يَنْمِي وفي الوَزنِ يَرْجَحُ

 

33- Na inapungua wakati mwengine kwa maasi na wakati mwengine, kwa kumtii Allaah inazidi na katika Miyzaan inakuwa nzito.

 

 

 

وَدَعْ عنكَ آراءَ الرِّجالِ وَقـولَهُـم                      فَقْولُ رَسُولِ اللهِ أَزكى وَأَشْــرَحُ

 

34- Na acha wewe rai za watu na kauli zao, kwani kauli ya Rasuli wa Allaah ni bora na ni kunjufu mno.

 

 

 

وَلا تَكُ مِـن قـوْمٍ تَلَهَّـوْ بِدِينِهِـم                             فَتَطْعـنَ في أَهَلِ الحَدَيثِ وتَقْـدَحُ

 

35- Na wala usiwe miongoni mwa watu ambao wamechezea dini yao, ukawa unawasema vibaya watu wa Hadiyth (Salafi) na unawatia dosari.

 

 

إذا مَا اعتقـدْتَ الدَّهْرَ يا صَاحِ هذِه                فَأَنْـتَ عَلـى خَيْـرٍ تَبِيتُ وتُصْبِحُ

 

36- Pindi utakapoitakidi hivi milele ee rafiki, hakika utakuwa katika khayr nyakati za usiku na asubuhi.

 
 
 
Share