Biriani ya Nyama Ng'ombe Na Mtindi
Biriani ya Nyama Ngombe Ya Vitunguu Vingi
Vipimo
Mchele wa biriani - 5 gilasi
Nyama ya ngombe ya mifupa - 1 ½ kilo na nusu
Vitunguu - 2 kilo
Tangawizi mbichi - ¼ kikombe
Thomu (saumu/garlic) - 3 vijiko vya supu
Mtindi - 2 vikombe
Nyanya ilokatwakatwa (chopped) - 3
Nyanya kopo - 1 kikombe
Masala ya biriani - 2 vijiko vya supu
Hiliki ya unga - 2 vijiko vya chai
Pilipili mbichi ilosagwa - 3 kiasi
Kotmiri ilokatwakatwa - 1 msongo (bunch)
Rangi ya biriani ya manjano - ½ kijiko cha chai
Zaafarani au zaafarani flavour - 1 kijiko cha supu
Mafuta ya kukaangia
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katakata vitunguu ukaangae katika mafuta mpaka vigeuke rangi ya brown ilokoza.
- Weka nyama iwe ilokatwakatwa katika treya au bakuli kubwa la oveni.
- Chaganya pamoja na tangawizi, thomu, nyanya, nyanya kopo, mtindi, masala ya biriani, chumvi, pilipili.
- Acha irowanike kwa muda wa masaa mawili takriban.
- Funika kwa karatasi ya jalbosi (foil paper) utie katika oveni upike muda wa dakika 45 takriban mpaka nyama iwive na huku unachanganya changanya sosi. Ikiwa ina maji ongezea nyanya kopo iwe nzito.
- Epua funua, kisha vuruga vitungu umwagie pamoja na kotmiri na umwagie mafuta ya moto kiasi.
- Ongezea kutia masala ya biriani na hiliki ya unga.
- Chemsha mchele nusu kiini, mwaga maji chuja, umwagie juu ya sosi ya nyama ukipenda kuchanganya au chemsha wali pekee.
- Nyunyizia rangi ya biriani pamoja na zaafarani flavour au zaafarani yenyewe ukipenda.
- Mimina mchele juu ya masala ya nyama, funika urudishe ndani ya oven upike muda wa kiasi ya dakika ishirini.
- Epua upake kwa kuchota wali kwanza kisha masala uwekee juu yake, kiwa tayari.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)