Imaam Ibn Hajr Al-'Asqalaaniy - Ni Wajibu Kujizuia Kuwasema Vibaya Maswahaba

Ni Wajibu Kujizuia Kuwasema Vibaya Maswahaba

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn Hajr Al-‘Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

 

“Na wameafikiana Ahlus-Sunnah kuhusu uwajibu wa kukataza kuwasema vibaya (kuwashambulia) yeyote katika Maswahaba kwa sababu ya yale yaliyotokea kwao miongoni mwa vita, hata kama atakuwa anajulikana mwenye haki miongoni mwao. Kwani wao hawakupigana katika vita hivyo isipokuwa kwa Ijtihaad, na Allaah Ta’aalaa Ameshamsamehe yule aliyekosea katika Ijtihaad yake, bali imethibiti kuwa yeye (huyo aliyekosea) anapata ujira mmoja (kwa aliyojitahidi akakosea) na yule aliyepatia (katika Ijitihaad yake) hupata ujira mbili.”

 

[Fat-hu Al-Baariy, mj. 13, uk. 34]

 

Share