Habbat Sawdaa: Manufaa Yake - 1
Habbat Sawdaa: Manufaa Yake – 1
Imekusanywa Na: Iliyaasah
Habbat-Sawdaa, mbegu ambazo zina tiba ya kila kitu, faida ambayo Nabiy wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuacha kutuongoza katika mas-ala ya afya zetu na shifaa za maradhi ya mwana-Aadam, nayo ni katika Hadiyth:
عن أبي هريرة رضي الله عنه أنه سمع رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «في الحَبَّةِ السوْدَاءِ شِفَاءٌ من كل دَاءٍ إلاَّ السَّام
Amesimulia Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Katika Habbat-Sawdaa kuna Shifaa (Poza) ya kila maradhi isipokuwa sumu.” [Al-Bukhaariy]
Muumini anayepatwa na maradhi, akimbilie kutumia dawa hii huku akiwa na Iymaan thabiti kumwamini Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kila alokuja nacho kwa sababu alipotuambia kuwa Habbat-Sawdaa ni Shifaa ya kila ugonjwa, basi hakuna shaka hata chembe kuwa ni dawa ya maradhi yote yanayomfika mwana Aadam. Mgonjwa asikate tamaa kutokana na Rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa), bali akithirishe kutumia Habbat-Sawdaa huku imthibitika Iymaan yake katika tiba hii. Na pia mwombe Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akujaalie shifaa kwani hakuna Shifaa isipo
Mbegu hizi za Habbat-Sawdaa zimekuwa maarufu mno miongoni mwa Waislaam na wasio Waislaam, na hadi sasa wengi kati ya wasio Waislaam wametambua kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kweli kuhusiana na tiba ya Habbat-Sawdaa. Na hivyo wanaitumia katika madawa kadhaa, na katika vipodozi na kadhaalika. Umaarufu wake Habbat-Sawdaa umeenea ulimwengu mzima na imetambulika kuwa inatibu kila aina ya maradhi. Baadhi ya maradhi hayo ni kama yafuatayo:
Kwa Faida Ya Afya Kwa Ujumla:
Kunywa kijiko kimoja cha mafuta ya Habbat-Sawdaa asubuhi na usiku, au kunywa japo asubuhi kabla ya kifungua kinywa, unaweza kunywa kijiko kimoja cha mafuta peke yake au ukachanganya na kijiko kimoja cha asali safi.
Vipele (Chunusi) Na Ngozi:
Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, ½ (nusu) kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na ½ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha (apple). Paka katika sehemu inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka wiki tatu na ni lazima uwekwe katika hali ya ubaridi.
Upara (Alopeshia):
Sugua mafuta ya Habbat-Sawdaa katika mabaka yanayokusumuba.
Pumu:
Tia ½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa iliyochemshwa katika maji ya yaliyochemshwa kisha unywe moto.
Kuumwa kwa Mgongo (Sehemu ya Chini):
Changanya asali pamoja na ¼ (robo) kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.
Mwiba Wa Nyuki Na Nyigu:
Tia ½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa iliyochemshwa katika maji ya yaliyochemshwa kisha unywe moto.
Kibofu cha Mkojo/Figo:
Kunywa maji ya moto yaliyochanganywa na½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa pamoja na asali kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Changanya vikombe viwili vya Habbat-Sawdaa iliyosagwa na ½ (nusu) kikombe cha asali safi. Kunywa kijiko kimoja cha mchanganyiko pamoja na kikombe kimoja cha maji ya moto kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Mchanganyiko unaweza kukaa kwa siku 15 na ni lazima uwekwe katika hali ya ubaridi.
Jiwe La Figo:
Kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyochanganwa pamoja na gilasi (bilauri) moja ya asali, vitunguu saumu vitatu vilivyosagwa na karafuu. Changanya vitunguu saumu pamoja na asali na Habbat-Sawdaa. Kunywa kijiko kimoja kabla ya kula chakula na kwa pendekezo kula limau (bila ya kumenywa). Rudia haya kwa wiki moja Insha-Allah jiwe litaondoka.
Maathiriko Ya Figo:
Changanya baadhi ya Habbat-Sawdaa pamoja na mafuta ya alizeti. Chukua mchanganyiko na weka katika sehemu ambapo figo limeathirika. Kunywa kijiko cha Habbat-Sawdaa asubuhi. Rudia haya kwa muda wa wiki moja Insha-Allah maathiriko yatatibika.
Mafua:
Chukua mbegu za Habbat-Sawdaa 21, ziweke katika kitambaa na roweka usiku. Tumia kama matone kwenye pua siku ya pili nusa poda ya Habbat-Sawdaa iliyomo katika kitambaa.
Kikohozi:
Tumia matone matatu au manne ya mafuta ya Habbat-Sawdaa kwenye kahawa au chai.
Bawasiri:
Kula unga wa Habbat-Sawdaa pamoja na maji.
Shinikizo La Damu (high blood pressure):
Changanya kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, kijiko kimoja cha asali safi na kitunguu thomu kiasi kidogo. Chukua mchanganyo kabla ya kufungua kinywa kwa siku ishirini.
Uwasho Na Maumivu Ya Jino Na Ufizi:
Chemsha Habbat-Sawdaa katika siki na itumie kwa kusukutulia meno na ufizi. Na jikinge kutumia dawa za msuwaki za kibiashara na tumia dawa za msuwaki ambazo zinatengenezwa kutoka kwenye nyuzi za mboga za mti wa siwak ambao kwa karne ulikuwa unatumiwa na Wahindi, Waafrika na Waarabu, ni msuwaki wa kiasili.
Kumbukumbu (memory):
Kunywa kijiko kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa na changanya na asali mara mbili kwa siku.
Utaratibu Wa Ulinzi Wa Mwili:
Kula kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa na asali mchana na usiku Kutoweza kuzuia haja ndogo (mkojo): Kunywa kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa pamoja na asali, kisha kunywa maji ya vugu vugu.
Jaundice:
Tumia Habbat-Sawdaa pamoja na maziwa.
Maumivu Sugu ya kichwa (Maumivu ya kichwa ya upande mmoja, maumivu ya kichwa):
Kaanga Habbat-Sawdaa na iweke katika kitambaa cha pamba, funga au weka tu kitambaa katika kikomo (kipaji cha uso). Roweka Habbat-Sawdaa ndani ya siki wakati wa usiku, siku ya pili ivuruge kufanya unga. Ingiza katika pua halafu vuta pumzi.
Ngozi kavu:
Changanya asali pamoja na robo kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.
Kutokwa na Upepo:
Changanya asali pamoja na robo kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.
Minyoo:
Kunywa Habbat-Sawdaa pamoja na siki kuondoa minyoo.