002-Riyaadhw Asw-Swalihiyn: Mlango Wa Tawbah
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب التوبة
002 - Mlango Wa Tawbah
قَالَ العلماءُ: التَّوْبَةُ وَاجبَةٌ مِنْ كُلِّ ذَنْب، فإنْ كَانتِ المَعْصِيَةُ بَيْنَ العَبْدِ وبَيْنَ اللهِ تَعَالَى لا تَتَعلَّقُ بحقّ آدَمِيٍّ فَلَهَا ثَلاثَةُ شُرُوط:
أحَدُها: أنْ يُقلِعَ عَنِ المَعصِيَةِ.
والثَّانِي: أَنْ يَنْدَمَ عَلَى فِعْلِهَا.
والثَّالثُ: أنْ يَعْزِمَ أَنْ لا يعُودَ إِلَيْهَا أَبَدًا. فَإِنْ فُقِدَ أَحَدُ الثَّلاثَةِ لَمْ تَصِحَّ تَوبَتُهُ.
وإنْ كَانَتِ المَعْصِيةُ تَتَعَلقُ بآدَمِيٍّ فَشُرُوطُهَا أرْبَعَةٌ: هذِهِ الثَّلاثَةُ، وأنْ يَبْرَأ مِنْ حَقّ صَاحِبِها، فَإِنْ كَانَتْ مالًا أَوْ نَحْوَهُ رَدَّهُ إِلَيْه، وإنْ كَانَت حَدَّ قَذْفٍ ونَحْوَهُ مَكَّنَهُ مِنْهُ أَوْ طَلَبَ عَفْوَهُ، وإنْ كَانْت غِيبَةً استَحَلَّهُ مِنْهَا. ويجِبُ أنْ يَتُوبَ مِنْ جميعِ الذُّنُوبِ، فَإِنْ تَابَ مِنْ بَعْضِها صَحَّتْ تَوْبَتُهُ عِنْدَ أهْلِ الحَقِّ مِنْ ذلِكَ الذَّنْبِ وبَقِيَ عَلَيهِ البَاقي.
وَقَدْ تَظَاهَرَتْ دَلائِلُ الكتَابِ والسُّنَّةِ، وإجْمَاعِ الأُمَّةِ عَلَى وُجوبِ التَّوبةِ.
التوبة: الرجوع عن معصية الله تعالى إلى طاعته، وطلب الاستحلال مِنَ المقذوف ونحوه إن بلغه ذلك، وإلا كفى الاستغفار
‘Ulamaa wamesema: ni wajibu kutubia kwa kila dhambi anayoitenda mtu. Maasi yanapokuwa ni baina ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’aalaa) na mja Wake yasiyofungamana na haki ya mwana Aadam, yana shuruti tatu:
1- Aache maasi
2- Ajute juu ya kuyatenda
3- Aazimie kutoyarudia tena kabisa. Moja katika shuruti hizo ikikosekana, tawbah yake haitosihi.
4- Maasi yanapofungamana na haki ya mwana Aadam, basi shuruti za tawbah ni nne: ni hizo tatu zilizotangulia na ya nne ni: aache haki ya mwenyewe; ikiwa ni mali na mfano wake amrejeshee, ikiwa ni haddi (adhabu) ya kutukana au mfano wake, atammakinisha au amuombe msamaha. Na ikiwa ni kusengenya basi atamuomba amhalalishie. Yapasa atubie dhambi zote. Akitubia baadhi yake, tawbah yake itasihi kutokana na dhambi ile kwa watu wa haki, na atabakiwa na dhambi nyinginezo. Dalili ya Qur-aan, Hadiyth na ijmaa’ ya ummah zipo nyingi katika kuthibitisha namna inavyotakiwa mtu kutubia.
قَالَ الله تَعَالَى:
وَتُوبُوا إِلَى اللَّـهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
Na tubuni kwa Allaah nyote, enyi Waumini mpate kufaulu. [An-Nuwr: 31]
وَأَنِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ
Na kwamba: “Mwombeni Rabb wenu maghfirah kisha tubuni Kwake.” [Huwd: 3]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّـهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا
Enyi walioamini! Tubieni kwa Allaah tawbah ya nasuha (kwelikweli). [At-Tahriym: 8]
Hadiyth – 1
عن أبي هريرةَ رضي الله عنه قَالَ: سمعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((واللهِ إنِّي لأَسْتَغْفِرُ الله وأَتُوبُ إِلَيْه في اليَوْمِ أَكْثَرَ مِنْ سَبْعِينَ مَرَّةً)). رواه البخاري
Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Wa-Allaahi mimi namuomba Allaah maghfirah na natubia Kwake zaidi ya mara sabini kwa siku.” [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 2
وعن الأَغَرِّ بنِ يسار المزنِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((يَا أَيُّهَا النَّاسُ، تُوبُوا إِلى اللهِ واسْتَغْفِرُوهُ، فإنِّي أتُوبُ في اليَومِ مائةَ مَرَّةٍ)). رواه مسلم.
Al-Agharri bin Yasaar Al-Muzaniyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Enyi watu, tubieni kwa Allaah na mumuombe maghfirah. Hakika mimi natubia Kwake mara mia kwa siku.” [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أبي حمزةَ أنسِ بنِ مالكٍ الأنصاريِّ- خادِمِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم رضي الله عنه- قَالَ: قَالَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((للهُ أفْرَحُ بِتَوْبَةِ عَبْدِهِ مِنْ أَحَدِكُمْ سَقَطَ عَلَى بَعِيرهِ وقد أضلَّهُ في أرضٍ فَلاةٍ)). مُتَّفَقٌ عليه.
وفي رواية لمُسْلمٍ: ((للهُ أَشَدُّ فَرَحًا بِتَوبَةِ عَبْدِهِ حِينَ يتوبُ إِلَيْهِ مِنْ أَحَدِكُمْ كَانَ عَلَى رَاحِلَتهِ بأرضٍ فَلاةٍ، فَانْفَلَتَتْ مِنْهُ وَعَلَيْهَا طَعَامُهُ وَشَرَابهُ فأَيِسَ مِنْهَا، فَأَتى شَجَرَةً فاضطَجَعَ في ظِلِّهَا وقد أيِسَ مِنْ رَاحلَتهِ، فَبَينَما هُوَ كَذَلِكَ إِذْ هُوَ بِها قائِمَةً عِندَهُ، فَأَخَذَ بِخِطامِهَا، ثُمَّ قَالَ مِنْ شِدَّةِ الفَرَحِ: اللَّهُمَّ أنْتَ عَبدِي وأنا رَبُّكَ! أَخْطَأَ مِنْ شِدَّةِ الفَرَحِ))
Abuu Hamzah, Anas bin Maalik Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) mtumishi wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Huifurahia mno tawbah ya mja Wake kuliko mmoja wenu aliyempata kwa ghafla ngamia wake baada ya kwisha kumpoteza katika ardhi ya jangwa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riwaayah nyingine ya Muslim inasema: “Allaah Ana furaha mno kwa mja Wake wakati anapomuomba tawbah kuliko mmoja wenu aliyekuwa juu ya ngamia wake katika ardhi ya jangwa, akimkimbia naye amebeba chakula chake na maji yake, akakata tamaa kuwa atampata; akauendea mti na akalala kivulini mwake naye ameshakata tamaa ya kumpata ngamia wake. Alipokuwa yuko katika hali hiyo, ghafla akamuona amemsimamia mbele yake, akamshika hatamu yake, halafu akasema kutokana na furaha kubwa: Ee Rabb! Wewe ni mja wangu nami ni Rabb wako! Amekosea kutokana na furaha kubwa (aliyonayo).”
Hadiyth – 4
وعن أبي موسَى عبدِ اللهِ بنِ قَيسٍ الأشْعريِّ رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((إنَّ الله تَعَالَى يَبْسُطُ يَدَهُ بالليلِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ النَّهَارِ، ويَبْسُطُ يَدَهُ بالنَّهَارِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ اللَّيلِ، حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِها)). رواه مسلم
Abuu Muwsa, 'Abdullaah bin Qays Al-Ash’ariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Hunyoosha Mkono Wake usiku ili yule aliyekosea mchana apate kutubia, na Hunyoosha mkono Wake mchana ili yule aliyekosea usiku apate kutubia, (hali hiyo huendelea) mpaka jua lichomozapo upande wa magharibi” [Muslim]
Hadiyth – 5
وعن أبي هُريرةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ تَابَ قَبْلَ أنْ تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِها تَابَ اللهُ عَلَيهِ)). رواه مسلم
Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwenye kutubia kabla ya jua kuchomoza upande wa magharibi, Allaah Atamkubalia tawbah yake.” [Muslim]
Hadiyth – 6
وعن أبي عبد الرحمن عبد الله بنِ عمَرَ بنِ الخطابِ رضيَ اللهُ عنهما عن النَّبي صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((إِنَّ الله عز وجل يَقْبَلُ تَوبَةَ العَبْدِ مَا لَمْ يُغَرْغِرْ)). رواه الترمذي، وَقالَ: ((حديث حسن))
Abuu ‘Abdir-Rahmaan, ‘Abdullaah bin ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu anhumaa) amehadithia kwamba: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika Allaah ‘Azza wa Jallaa Huikubali tawbah ya mja madamu roho yake haijafika kooni.” [At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth hii ni Hasan]
Hadiyth – 7
وعن زِرِّ بن حُبَيْشٍ، قَالَ: أَتَيْتُ صَفْوَانَ بْنَ عَسَّالٍ رضي الله عنه أسْألُهُ عَن الْمَسْحِ عَلَى الخُفَّيْنِ، فَقالَ: ما جاءَ بكَ يَا زِرُّ؟ فقُلْتُ: ابتِغَاء العِلْمِ، فقالَ: إنَّ المَلائكَةَ تَضَعُ أجْنِحَتَهَا لطَالبِ العِلْمِ رِضىً بِمَا يطْلُبُ. فقلتُ: إنَّهُ قَدْ حَكَّ في صَدْري المَسْحُ عَلَى الخُفَّينِ بَعْدَ الغَائِطِ والبَولِ، وكُنْتَ امْرَءًا مِنْ أَصْحَابِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم فَجئتُ أَسْأَلُكَ هَلْ سَمِعْتَهُ يَذكُرُ في ذلِكَ شَيئًا؟ قَالَ: نَعَمْ، كَانَ يَأْمُرُنا إِذَا كُنَّا سَفرًا- أَوْ مُسَافِرينَ- أنْ لا نَنْزعَ خِفَافَنَا ثَلاثَةَ أَيَّامٍ وَلَيالِيهنَّ إلا مِنْ جَنَابَةٍ، لكنْ مِنْ غَائطٍ وَبَولٍ ونَوْمٍ. فقُلْتُ: هَلْ سَمِعْتَهُ يَذْكرُ في الهَوَى شَيئًا؟ قَالَ: نَعَمْ، كُنّا مَعَ رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم في سَفَرٍ، فبَيْنَا نَحْنُ عِندَهُ إِذْ نَادَاه أَعرابيٌّ بصَوْتٍ لَهُ جَهْوَرِيٍّ: يَا مُحَمَّدُ، فأجابهُ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم نَحْوًا مِنْ صَوْتِه: ((هَاؤُمْ)) فقُلْتُ لَهُ: وَيْحَكَ! اغْضُضْ مِنْ صَوتِكَ فَإِنَّكَ عِنْدَ النَّبي صلى الله عليه وسلم، وَقَدْ نُهِيتَ عَنْ هذَا! فقالَ: والله لا أغْضُضُ. قَالَ الأعرَابيُّ: المَرْءُ يُحبُّ القَوْمَ وَلَمَّا يلْحَقْ بِهِمْ؟ قَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم: ((المَرْءُ مَعَ مَنْ أَحَبَّ يَومَ القِيَامَةِ)). فَمَا زَالَ يُحَدِّثُنَا حَتَّى ذَكَرَ بَابًا مِنَ المَغْرِبِ مَسيرَةُ عَرْضِهِ أَوْ يَسِيرُ الرَّاكبُ في عَرْضِهِ أرْبَعينَ أَوْ سَبعينَ عامًا- قَالَ سُفْيانُ أَحدُ الرُّواةِ: قِبَلَ الشَّامِ- خَلَقَهُ الله تَعَالَى يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاواتِ والأَرْضَ مَفْتوحًا للتَّوْبَةِ لا يُغْلَقُ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْهُ. رواه الترمذي وغيره، وَقالَ: ((حديث حسن صحيح)).
Zirru bin Hubaysh amesema: “Nilimuendea Swafwaan bin ‘Assaal (Radhwiya Allaahu ‘anhu) nikimuuliza kuhusu kupangusa juu ya khuffu mbili. Akaniuliza: Ni jambo lipi limekuleta Ee Zirru? Akasema: “Hakika Malaika humuwekea mbawa zao mwenye kutafuta ‘Ilmu kwa kumridhia anachokitafuta. Nikamwambia: “Kwa hakika nimeingiwa na shaka moyoni mwangu na kupangusa juu ya khuffu baada hajja kubwa na ndogo, nami nilikuwa mmoja katika Swahaba wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa hivyo nimekuja kukuuliza je, uliwahi kumsikia akisema chochote katika hilo?” Akajibu: “Ndio. Alikuwa akituamuru tunapokuwa safarini tusivue khuffu zetu michana mitatu na masiku yake, isipokuwa tu kutokana na janaba, lakini kutokana na haja kubwa, ndogo na kulala (tusivue).” Nikamuuliza: “Je, ulimsikia akisema chochote juu ya mapenzi?” Akajibu: “Ndio. Tulikuwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) safarini, tulipokuwa tupo kwake, kwa ghafla akaitwa na Bedui kwa sauti kubwa: “Ee Muhammad!” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuitikia kwa sauti kama yake: “Njoo.” Nikamwambia (Bedui): “Nakuhurumia, teremsha sauti yako kwani upo mbele ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na umekatazwa jambo hili!” Akasema: “Wa-Allaahi siteremshi!” Yule Bedui akasema: “Unaonaje kuhusu mtu anapenda watu na bado hajakutana nao?” Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Mtu atakuwa pamoja na ampendae siku ya Qiyaamah.” Basi akaendelea kutuzungumzia mpaka akautaja mlango upande wa magharibi mwendo wa upana wake au atasafiri mpandaji kwa upana huu miaka miaka arobaini au sabini. Akasema Sufyaan mmoja wa wapokezi: “Upande wa Shamu. Allaah Aliuumba tokea siku Aliyoumba mbingu na ardhi hali ya kuwa umefunguliwa kwa ajili ya tawbah, haufungwi mpaka jua lichomoze upande huo.” [At-Tirmidhiy na wengineo, na akasema: Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 8
وعن أبي سَعيد سَعْدِ بنِ مالكِ بنِ سِنَانٍ الخدريِّ رضي الله عنه أنّ نَبِيَّ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((كَانَ فِيمَنْ كَانَ قَبْلَكمْ رَجُلٌ قَتَلَ تِسْعَةً وتِسْعينَ نَفْسًا، فَسَأَلَ عَنْ أعْلَمِ أَهْلِ الأرضِ، فَدُلَّ عَلَى رَاهِبٍ، فَأَتَاهُ. فقال: إنَّهُ قَتَلَ تِسعَةً وتِسْعِينَ نَفْسًا فَهَلْ لَهُ مِنْ تَوبَةٍ؟ فقالَ: لا، فَقَتَلهُ فَكَمَّلَ بهِ مائَةً، ثُمَّ سَأَلَ عَنْ أَعْلَمِ أَهْلِ الأَرضِ، فَدُلَّ عَلَى رَجُلٍ عَالِمٍ. فقَالَ: إِنَّهُ قَتَلَ مِائَةَ نَفْسٍ فَهَلْ لَهُ مِنْ تَوْبَةٍ؟ فقالَ: نَعَمْ، ومَنْ يَحُولُ بَيْنَهُ وبَيْنَ التَّوْبَةِ؟ انْطَلِقْ إِلى أرضِ كَذَا وكَذَا فإِنَّ بِهَا أُناسًا يَعْبُدُونَ الله تَعَالَى فاعْبُدِ الله مَعَهُمْ، ولا تَرْجِعْ إِلى أَرْضِكَ فَإِنَّهَا أرضُ سُوءٍ، فانْطَلَقَ حَتَّى إِذَا نَصَفَ الطَّرِيقَ أَتَاهُ الْمَوْتُ، فاخْتَصَمَتْ فِيهِ مَلائِكَةُ الرَّحْمَةِ ومَلائِكَةُ العَذَابِ. فَقَالتْ مَلائِكَةُ الرَّحْمَةِ: جَاءَ تَائِبًا، مُقْبِلًا بِقَلبِهِ إِلى اللهِ تَعَالَى، وقالتْ مَلائِكَةُ العَذَابِ: إنَّهُ لمْ يَعْمَلْ خَيرًا قَطُّ، فَأَتَاهُمْ مَلَكٌ في صورَةِ آدَمِيٍّ فَجَعَلُوهُ بَيْنَهُمْ- أيْ حَكَمًا- فقالَ: قِيسُوا ما بينَ الأرضَينِ فَإلَى أيّتهما كَانَ أدنَى فَهُوَ لَهُ. فَقَاسُوا فَوَجَدُوهُ أدْنى إِلى الأرْضِ التي أرَادَ، فَقَبَضَتْهُ مَلائِكَةُ الرَّحمةِ)). مُتَّفَقٌ عليه
وفي رواية في الصحيح: ((فَكَانَ إلى القَريَةِ الصَّالِحَةِ أقْرَبَ بِشِبْرٍ فَجُعِلَ مِنْ أهلِهَا))
Abuu Sa’iyd bin Maalik bin Sinaan Al-Khudriyy (Radhiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kulikuwepo mtu kabla yenu aliua watu tisini na tisa (99) akaulizia aliye mjuzi zaidi katika watu katika nchi ile. Akajulishwa mtawa (miongoni mwa Bani Israaiyl). Akamwendea, akamuuliza: “Nimeua watu tisini na tisa, je, nina tawbah?” Akamjibu: “Hapana!” Akamuua, akawa mtu wa mia. Kisha akauuliza mjuzi zaidi katika watu katika nchi ile. Akafahamishwa kuhusu Mwanachuoni. Akamuuliza: “Nimeua watu mia. Je, nina tawbah?” Akamjibu: “Ndio, ni nani atakayezuia baina yako na tawbah? Nenda katika nchi fulani, huko kuna watu wanaomuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) basi nenda ukamuabudu Allaah pamoja nao wala usirejee katika nchi yako, kwani hiyo ni nchi ya maovu.” Akaenda, hata alipofika nusu ya njia, alifikwa na mauti. Malaika wa rahmah wakaanza kuvutana na Malaika wa adhabu. Malaika wa rahmah wakasema: “Alikuja hali ya kutubia na ameelekea moyo wake kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).” Malaika wa adhabu wakasema: “Yeye hakutenda khayr katu!” Akaja Malaika (mwengine) katika sura ya mwana Aadam, wakamfanya ndiye hakimu baina yao. Akawaambia: “Pimeni baina ya nchi mbili, katika nchi yoyote iliyopo karibu naye, atakuwa ni wa huko.” Wakapima, wakamkuta kuwa yupo karibu zaidi na nchi anayokusudia kwenda. Malaika wa rahmah wakamchukua.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riwaayah nyingine ya Swahiyh Al-Bukhaariy, imesema: “Akawa katika kijiji cha watu wema yu karibu nacho kwa shubiri moja. Akajaaliwa ni wa huko.”
Riwaayah nyingine ya Swahiyh Al-Bukhaariy, imesema: “Allaah Akakiambia kijiji alichotoka: “Kuwa mbali!” na kijiji anachoenda: “Kuwa karibu!” Na Akawaambia pimeni baina yake.” Wakampata kuwa yupo karibu zaidi ya kijiji anachokwenda kwa shubiri moja; akasamehewa.”
Riwaayah nyingine inasema: “Akakaribia kwa kifua chake upande ule.”
Hadiyth – 9
وعن عبدِ الله بن كعبِ بنِ مالكٍ، وكان قائِدَ كعبٍ رضي الله عنه مِنْ بَنِيهِ حِينَ عمِيَ، قَالَ: سَمِعتُ كَعْبَ بنَ مالكٍ رضي الله عنه يُحَدِّثُ بحَديثهِ حينَ تَخلَّفَ عن رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم في غَزْوَةِ تَبُوكَ. قَالَ كعبٌ: لَمْ أتَخَلَّفْ عَنْ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم في غَزْوَةٍ غزاها قط إلا في غزوة تَبُوكَ، غَيْرَ أنّي قَدْ تَخَلَّفْتُ في غَزْوَةِ بَدْرٍ، ولَمْ يُعَاتَبْ أَحَدٌ تَخَلَّفَ عَنْهُ؛ إِنَّمَا خَرَجَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم والمُسْلِمُونَ يُريدُونَ عِيرَ قُرَيْشٍ حَتَّى جَمَعَ الله تَعَالَى بَيْنَهُمْ وبَيْنَ عَدُوِّهمْ عَلَى غَيْر ميعادٍ. ولَقَدْ شَهِدْتُ مَعَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم لَيلَةَ العَقَبَةِ حينَ تَوَاثَقْنَا عَلَى الإِسْلامِ، وما أُحِبُّ أنَّ لي بِهَا مَشْهَدَ بَدْرٍ، وإنْ كَانَتْ بدرٌ أذْكَرَ في النَّاسِ مِنْهَا. وكانَ مِنْ خَبَري حينَ تَخَلَّفْتُ عَنْ رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم في غَزْوَةِ تَبُوكَ أنِّي لم أكُنْ قَطُّ أَقْوى ولا أَيْسَرَ مِنِّي حِينَ تَخَلَّفْتُ عنْهُ في تِلكَ الغَزْوَةِ، وَالله ما جَمَعْتُ قَبْلَهَا رَاحِلَتَيْنِ قَطُّ حَتَّى جَمَعْتُهُمَا في تِلْكَ الغَزْوَةِ وَلَمْ يَكُنْ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يُريدُ غَزْوَةً إلا وَرَّى بِغَيرِها حَتَّى كَانَتْ تلْكَ الغَزْوَةُ، فَغَزَاها رسولُ الله صلى الله عليه وسلم في حَرٍّ شَديدٍ، واسْتَقْبَلَ سَفَرًا بَعِيدًا وَمَفَازًا، وَاستَقْبَلَ عَدَدًا كَثِيرًا، فَجَلَّى للْمُسْلِمينَ أمْرَهُمْ ليتَأهَّبُوا أُهْبَةَ غَزْوِهمْ فأَخْبرَهُمْ بوَجْهِهِمُ الَّذِي يُريدُ، والمُسلِمونَ مَعَ رسولِ الله كثيرٌ وَلا يَجْمَعُهُمْ كِتَابٌ حَافِظٌ (يُريدُ بذلِكَ الدّيوَانَ) قَالَ كَعْبٌ: فَقَلَّ رَجُلٌ يُريدُ أنْ يَتَغَيَّبَ إلا ظَنَّ أنَّ ذلِكَ سيخْفَى بِهِ ما لَمْ يَنْزِلْ فِيهِ وَحْيٌ مِنَ الله، وَغَزا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم تِلْكَ الغَزوَةَ حِينَ طَابَت الثِّمَارُ وَالظِّلالُ، فَأنَا إلَيْهَا أصْعَرُ، فَتَجَهَّزَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم وَالمُسْلِمُونَ مَعَهُ وطَفِقْتُ أغْدُو لكَيْ أتَجَهَّزَ مَعَهُ، فأرْجِعُ وَلَمْ أقْضِ شَيْئًا، وأقُولُ في نفسي: أنَا قَادرٌ عَلَى ذلِكَ إِذَا أَرَدْتُ، فَلَمْ يَزَلْ يَتَمادى بي حَتَّى اسْتَمَرَّ بالنَّاسِ الْجِدُّ، فأصْبَحَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم غَاديًا والمُسْلِمُونَ مَعَهُ وَلَمْ أقْضِ مِنْ جِهَازي شَيْئًا، ثُمَّ غَدَوْتُ فَرَجَعْتُ وَلَمْ أقْضِ شَيئًا، فَلَمْ يَزَلْ يَتَمَادَى بي حَتَّى أسْرَعُوا وتَفَارَطَ الغَزْوُ، فَهَمَمْتُ أنْ أرْتَحِلَ فَأُدْرِكَهُمْ، فَيَا لَيْتَني فَعَلْتُ، ثُمَّ لم يُقَدَّرْ ذلِكَ لي، فَطَفِقْتُ إذَا خَرَجْتُ في النَّاسِ بَعْدَ خُرُوجِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَحْزُنُنِي أنِّي لا أرَى لي أُسْوَةً، إلا رَجُلًا مَغْمُوصًا عَلَيْهِ في النِّفَاقِ، أوْ رَجُلًا مِمَّنْ عَذَرَ اللهُ تَعَالَى مِنَ الضُّعَفَاءِ، وَلَمْ يَذْكُرْنِي رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم حَتَّى بَلَغَ تَبُوكَ، فَقَالَ وَهُوَ جَالِسٌ في القَوْمِ بِتَبُوكَ: ((ما فَعَلَ كَعْبُ بْنُ مَالِكٍ؟)) فَقَالَ رَجُلٌ مِنْ بَنِي سَلِمَةَ: يا رَسُولَ اللهِ، حَبَسَهُ بُرْدَاهُ والنَّظَرُ في عِطْفَيْهِ. فَقَالَ لَهُ مُعَاذُ بْنُ جَبَلٍ رضي الله عنه: بِئْسَ مَا قُلْتَ! واللهِ يا رَسُولَ اللهِ مَا عَلِمْنَا عَلَيْهِ إلا خَيْرًا، فَسَكَتَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم. فَبَيْنَا هُوَ عَلى ذَلِكَ رَأى رَجُلًا مُبْيِضًا يَزُولُ بِهِ السَّرَابُ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: ((كُنْ أَبَا خَيْثَمَةَ))، فَإذَا هُوَ أبُو خَيْثَمَةَ الأنْصَارِيُّ وَهُوَ الَّذِي تَصَدَّقَ بِصَاعِ التَّمْرِ حِيْنَ لَمَزَهُ المُنَافِقُونَ.
قَالَ كَعْبٌ: فَلَمَّا بَلَغَنِي أنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَدْ تَوَجَّهَ قَافِلًا مِنْ تَبُوكَ حَضَرَنِي بَثِّي، فَطَفِقْتُ أتَذَكَّرُ الكَذِبَ وأقُولُ: بِمَ أخْرُجُ مِنْ سَخَطِهِ غَدًا؟ وأسْتَعِيْنُ عَلى ذَلِكَ بِكُلِّ ذِي رأْيٍ مِنْ أهْلِي، فَلَمَّا قِيْلَ: إنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قّدْ أظَلَّ قَادِمًا، زَاحَ عَنّي البَاطِلُ حَتَّى عَرَفْتُ أَنِّي لَنْ أَنْجُوَ مِنْهُ بِشَيءٍ أَبَدًا، فَأجْمَعْتُ صدْقَهُ وأَصْبَحَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم قَادِمًا، وَكَانَ إِذَا قَدِمَ مِنْ سَفَرٍ بَدَأَ بِالمَسْجِدِ فَرَكَعَ فِيهِ رَكْعَتَيْنِ ثُمَّ جَلَسَ لِلنَّاسِ، فَلَمَّا فَعَلَ ذلِكَ جَاءهُ المُخَلَّفُونَ يَعْتَذِرونَ إِلَيْه ويَحْلِفُونَ لَهُ، وَكَانُوا بِضْعًا وَثَمانينَ رَجُلًا، فَقَبِلَ مِنْهُمْ عَلانِيَتَهُمْ وَبَايَعَهُمْ واسْتَغْفَرَ لَهُمْ وَوَكَلَ سَرَائِرَهُمْ إِلى الله تَعَالَى، حَتَّى جِئْتُ، فَلَمَّا سَلَّمْتُ تَبَسَّمَ تَبَسُّمَ المُغْضَبِ. ثُمَّ قَالَ: ((تَعَالَ))، فَجِئْتُ أمْشي حَتَّى جَلَسْتُ بَيْنَ يَدَيْهِ، فقالَ لي: ((مَا خَلَّفَكَ؟ ألَمْ تَكُنْ قَدِ ابْتَعْتَ ظَهْرَكَ؟)) قَالَ: قُلْتُ: يَا رسولَ الله، إنّي والله لَوْ جَلَسْتُ عِنْدَ غَيْرِكَ مِنْ أهْلِ الدُّنْيَا لَرَأيتُ أنِّي سَأخْرُجُ مِنْ سَخَطِهِ بِعُذْرٍ؛ لقَدْ أُعْطِيتُ جَدَلًا، ولَكِنِّي والله لَقَدْ عَلِمْتُ لَئِنْ حَدَّثْتُكَ اليوم حَدِيثَ كَذبٍ تَرْضَى به عنِّي لَيُوشِكَنَّ الله أن يُسْخِطَكَ عَلَيَّ، وإنْ حَدَّثْتُكَ حَدِيثَ صِدقٍ تَجِدُ عَلَيَّ فِيهِ إنّي لأَرْجُو فِيهِ عُقْبَى الله- عز وجل، والله ما كَانَ لي مِنْ عُذْرٍ، واللهِ مَا كُنْتُ قَطُّ أَقْوَى وَلا أَيْسَرَ مِنِّي حِينَ تَخَلَّفْتُ عَنْكَ. قَالَ: فقالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((أمَّا هَذَا فقَدْ صَدَقَ، فَقُمْ حَتَّى يَقْضِيَ اللهُ فيكَ)). وَسَارَ رِجَالٌ مِنْ بَنِي سَلِمَة فاتَّبَعُوني فَقالُوا لِي: واللهِ مَا عَلِمْنَاكَ أذْنَبْتَ ذَنْبًا قَبْلَ هذَا لَقَدْ عَجَزْتَ في أنْ لا تَكونَ اعتَذَرْتَ إِلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بما اعْتَذَرَ إليهِ المُخَلَّفُونَ، فَقَدْ كَانَ كَافِيكَ ذَنْبَكَ اسْتِغْفَارُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم لَكَ. قَالَ: فَوالله ما زَالُوا يُؤَنِّبُونَنِي حَتَّى أَرَدْتُّ أَنْ أرْجعَ إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم فأُكَذِّبَ نَفْسِي، ثُمَّ قُلْتُ لَهُمْ: هَلْ لَقِيَ هذَا مَعِيَ مِنْ أَحَدٍ؟ قَالُوا: نَعَمْ، لَقِيَهُ مَعَكَ رَجُلانِ قَالا مِثْلَ مَا قُلْتَ، وَقيلَ لَهُمَا مِثْلَ مَا قيلَ لَكَ، قَالَ: قُلْتُ: مَنْ هُما؟ قَالُوا: مُرَارَةُ بْنُ الرَّبيع الْعَمْرِيُّ، وهِلاَلُ ابنُ أُمَيَّةَ الوَاقِفِيُّ؟ قَالَ: فَذَكَرُوا لِي رَجُلَينِ صَالِحَينِ قَدْ شَهِدَا بَدْرًا فيهِما أُسْوَةٌ، قَالَ: فَمَضَيْتُ حِينَ ذَكَرُوهُما لِي. ونَهَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم عَنْ كَلامِنا أيُّهَا الثَّلاثَةُ مِنْ بَيْنِ مَنْ تَخَلَّفَ عَنْهُ، فاجْتَنَبَنَا النَّاسُ- أوْ قَالَ: تَغَيَّرُوا لَنَا- حَتَّى تَنَكَّرَتْ لي في نَفْسي الأَرْض، فَمَا هِيَ بالأرْضِ الَّتي أعْرِفُ، فَلَبِثْنَا عَلَى ذلِكَ خَمْسِينَ لَيْلَةً. فَأمّا صَاحِبَايَ فَاسْتَكَانا وقَعَدَا في بُيُوتِهِمَا يَبْكيَان. وأمَّا أنَا فَكُنْتُ أشَبَّ الْقَومِ وأجْلَدَهُمْ فَكُنْتُ أخْرُجُ فَأشْهَدُ الصَّلاَةَ مَعَ المُسْلِمِينَ، وأطُوفُ في الأَسْوَاقِ وَلا يُكَلِّمُنِي أَحَدٌ، وَآتِي رسولَ الله صلى الله عليه وسلم فأُسَلِّمُ عَلَيْهِ وَهُوَ في مَجْلِسِهِ بَعْدَ الصَّلاةِ، فَأَقُولُ في نَفسِي: هَلْ حَرَّكَ شَفَتَيْه برَدِّ السَّلام أَمْ لا؟ ثُمَّ أُصَلِّي قَريبًا مِنْهُ وَأُسَارِقُهُ النَّظَرَ، فَإِذَا أقْبَلْتُ عَلَى صَلاتِي نَظَرَ إلَيَّ وَإِذَا الْتَفَتُّ نَحْوَهُ أعْرَضَ عَنِّي، حَتَّى إِذَا طَال ذلِكَ عَلَيَّ مِنْ جَفْوَةِ المُسْلِمينَ مَشَيْتُ حَتَّى تَسَوَّرْتُ جِدارَ حائِط أبي قَتَادَةَ وَهُوَ ابْنُ عَمِّي وأَحَبُّ النَّاس إِلَيَّ، فَسَلَّمْتُ عَلَيهِ فَوَاللهِ مَا رَدَّ عَليَّ السَّلامَ، فَقُلْتُ لَهُ: يَا أَبَا قَتَادَةَ، أنْشُدُكَ بالله هَلْ تَعْلَمُنِي أُحِبُّ الله وَرَسُولَهُ صلى الله عليه وسلم؟ فَسَكَتَ، فَعُدْتُ فَنَاشَدْتُهُ فَسَكَتَ، فَعُدْتُ فَنَاشَدْتُهُ، فَقَالَ: اللهُ ورَسُولُهُ أَعْلَمُ. فَفَاضَتْ عَيْنَايَ، وَتَوَلَّيْتُ حَتَّى تَسَوَّرْتُ الجِدَارَ، فَبَيْنَا أَنَا أمْشِي في سُوقِ الْمَدِينة إِذَا نَبَطِيٌّ مِنْ نَبَطِ أهْلِ الشَّام مِمّنْ قَدِمَ بالطَّعَامِ يَبيعُهُ بِالمَدِينَةِ يَقُولُ: مَنْ يَدُلُّ عَلَى كَعْبِ بْنِ مَالِكٍ؟ فَطَفِقَ النَّاسُ يُشِيرُونَ لَهُ إلَيَّ حَتَّى جَاءنِي فَدَفَعَ إِلَيَّ كِتَابًا مِنْ مَلِكِ غَسَّانَ، وَكُنْتُ كَاتبًا. فَقَرَأْتُهُ فإِذَا فِيهِ: أَمَّا بَعْدُ، فإِنَّهُ قَدْ بَلَغَنا أنَّ صَاحِبَكَ قَدْ جَفَاكَ وَلَمْ يَجْعَلْكَ اللهُ بدَارِ هَوانٍ وَلا مَضْيَعَةٍ، فَالْحَقْ بنَا نُوَاسِكَ، فَقُلْتُ حِينَ قَرَأْتُهَا: وَهَذِهِ أَيضًا مِنَ البَلاءِ، فَتَيَمَّمْتُ بهَا التَّنُّورَ فَسَجَرْتُهَا، حَتَّى إِذَا مَضَتْ أَرْبَعُونَ مِنَ الْخَمْسينَ وَاسْتَلْبَثَ الْوَحْيُ إِذَا رسولُ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم يَأتِيني، فَقالَ: إنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يَأمُرُكَ أنْ تَعْتَزِلَ امْرَأتَكَ، فَقُلْتُ: أُطَلِّقُهَا أمْ مَاذَا أفْعَلُ؟ فَقالَ: لا، بَلِ اعْتَزِلْهَا فَلا تَقْرَبَنَّهَا، وَأَرْسَلَ إِلَى صَاحِبَيَّ بِمِثْلِ ذلِكَ. فَقُلْتُ لامْرَأتِي: الْحَقِي بِأهْلِكِ فَكُوني عِنْدَهُمْ حَتَّى يَقْضِيَ اللهُ في هَذَا الأمْرِ. فَجَاءتِ امْرَأةُ هِلاَلِ بْنِ أُمَيَّةَ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم فَقَالَتْ لَهُ: يَا رَسُولَ الله، إنَّ هِلاَلَ بْنَ أمَيَّةَ شَيْخٌ ضَائِعٌ لَيْسَ لَهُ خَادِمٌ، فَهَلْ تَكْرَهُ أنْ أخْدُمَهُ؟ قَالَ: ((لا، وَلَكِنْ لا يَقْرَبَنَّكِ)) فَقَالَتْ: إِنَّهُ واللهِ ما بِهِ مِنْ حَرَكَةٍ إِلَى شَيْءٍ، وَوَالله مَا زَالَ يَبْكِي مُنْذُ كَانَ مِنْ أمْرِهِ مَا كَانَ إِلَى يَومِهِ هَذَا. فَقَالَ لي بَعْضُ أهْلِي: لَو اسْتَأْذَنْتَ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم في امْرَأَتِكَ فَقَدْ أَذِن لاِمْرَأةِ هلاَل بْنِ أمَيَّةَ أنْ تَخْدُمَهُ؟ فَقُلْتُ: لا أسْتَأذِنُ فيها رسولَ الله صلى الله عليه وسلم وَمَا يُدْرِيني مَاذَا يقُول رسولُ الله صلى الله عليه وسلم إِذَا اسْتَأْذَنْتُهُ، وَأَنَا رَجُلٌ شَابٌ! فَلَبِثْتُ بِذَلِكَ عَشْرَ لَيَالٍ فَكَمُلَ لَنا خَمْسُونَ لَيْلَةً مِنْ حِينَ نُهِيَ عَنْ كَلاَمِنا، ثُمَّ صَلَّيْتُ صَلاَةَ الْفَجْرِ صَبَاحَ خَمْسِينَ لَيْلَةً عَلَى ظَهْرِ بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِنَا، فَبَيْنَا أَنَا جَالِسٌ عَلَى الْحالِ الَّتي ذَكَرَ الله تَعَالَى مِنَّا، قَدْ ضَاقَتْ عَلَيَّ نَفْسي وَضَاقَتْ عَلَيَّ الأرْضُ بِمَا رَحُبَتْ، سَمِعْتُ صَوْتَ صَارِخٍ أوفَى عَلَى سَلْعٍ يَقُولُ بِأعْلَى صَوتِهِ: يَا كَعْبَ بْنَ مَالِكٍ أبْشِرْ، فَخَرَرْتُ سَاجِدًا، وَعَرَفْتُ أنَّهُ قَدْ جَاءَ فَرَجٌ. فآذَنَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم النَّاسَ بِتَوْبَةِ الله عز وجل عَلَيْنَا حِينَ صَلَّى صَلاةَ الفَجْر فَذَهَبَ النَّاسُ يُبَشِّرُونَنَا، فَذَهَبَ قِبَلَ صَاحِبَيَّ مُبَشِّرونَ وَرَكَضَ رَجُلٌ إِلَيَّ فَرَسًا وَسَعَى سَاعٍ مِنْ أسْلَمَ قِبَلِي، وَأَوْفَى عَلَى الْجَبَلِ، فَكانَ الصَّوْتُ أسْرَعَ مِنَ الفَرَسِ، فَلَمَّا جَاءني الَّذِي سَمِعْتُ صَوْتَهُ يُبَشِّرُني نَزَعْتُ لَهُ ثَوْبَيَّ فَكَسَوْتُهُمَا إيَّاهُ بِبشارته، وَاللهِ مَا أمْلِكُ غَيْرَهُمَا يَوْمَئِذٍ، وَاسْتَعَرْتُ ثَوْبَيْنِ فَلَبسْتُهُما، وَانْطَلَقْتُ أتَأمَّمُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يَتَلَقَّاني النَّاسُ فَوْجًا فَوْجًا يُهنِّئونَني بالتَّوْبَةِ وَيَقُولُونَ لِي: لِتَهْنِكَ تَوْبَةُ الله عَلَيْكَ. حَتَّى دَخَلْتُ الْمَسْجِدَ فَإِذَا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم جَالِسٌ حَوْلَه النَّاسُ، فَقَامَ طَلْحَةُ بْنُ عُبَيْدِ اللهِ رضي الله عنه يُهَرْوِلُ حَتَّى صَافَحَني وَهَنَّأَنِي، والله مَا قَامَ رَجُلٌ مِنَ المُهَاجِرينَ غَيرُهُ- فَكَانَ كَعْبٌ لا يَنْسَاهَا لِطَلْحَةَ.
قَالَ كَعْبٌ: فَلَمَّا سَلَّمْتُ عَلَى رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ وَهُوَ يَبْرُقُ وَجْهُهُ مِنَ السُّرُور: ((أبْشِرْ بِخَيْرِ يَومٍ مَرَّ عَلَيْكَ مُذْ وَلَدَتْكَ أُمُّكَ)) فَقُلْتُ: أمِنْ عِنْدِكَ يَا رَسُول الله أَمْ مِنْ عِندِ الله؟ قَالَ: ((لا، بَلْ مِنْ عِنْدِ الله- عز وجل))، وَكَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم إِذَا سُرَّ اسْتَنَارَ وَجْهُهُ حَتَّى كَأَنَّ وَجْهَهُ قِطْعَةُ قَمَرٍ وَكُنَّا نَعْرِفُ ذلِكَ مِنْهُ، فَلَمَّا جَلَسْتُ بَيْنَ يَدَيْهِ قُلْتُ: يَا رسولَ الله، إنَّ مِنْ تَوْبَتِي أنْ أنْخَلِعَ مِنْ مَالِي صَدَقَةً إِلَى اللهِ وَإِلَى رَسُولهِ. فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((أَمْسِكَ عَلَيْكَ بَعْضَ مَالِكَ فَهُوَ خَيْرٌ لَكَ)). فقلتُ: إِنِّي أُمْسِكُ سَهْمِي الَّذِي بِخَيبَر. وَقُلْتُ: يَا رسولَ الله، إنَّ الله تَعَالَى إِنَّمَا أنْجَانِي بالصِّدْقِ، وإنَّ مِنْ تَوْبَتِي أنْ لا أُحَدِّثَ إلا صِدْقًا مَا بَقِيتُ، فوَالله مَا عَلِمْتُ أَحَدًا مِنَ المُسْلِمينَ أبْلاهُ الله تَعَالَى في صِدْقِ الحَدِيثِ مُنْذُ ذَكَرْتُ ذلِكَ لِرسولِ الله صلى الله عليه وسلم أحْسَنَ مِمَّا أبْلانِي الله تَعَالَى، واللهِ مَا تَعَمَّدْتُ كِذْبَةً مُنْذُ قُلْتُ ذلِكَ لِرسولِ الله صلى الله عليه وسلم إِلَى يَومِيَ هَذَا، وإنِّي لأرْجُو أنْ يَحْفَظَنِي الله تَعَالَى فيما بَقِيَ، قَالَ: فأَنْزَلَ الله تَعَالَى: {لَقَدْ تَابَ اللهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالأَنْصَارِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ الْعُسْرَةِ} حَتَّى بَلَغَ: {إِنَّهُ بِهِمْ رَؤُوفٌ رَحِيم وَعَلَى الثَّلاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا حَتَّى إِذَا ضَاقَتْ عَلَيْهِمُ الأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ} حَتَّى بَلَغَ: {اتَّقُوا اللهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ} [التوبة: 117: 119] قَالَ كَعْبٌ: واللهِ ما أنْعَمَ الله عَليَّ مِنْ نعمةٍ قَطُّ بَعْدَ إذْ هَدَاني اللهُ للإِسْلامِ أَعْظَمَ في نَفْسِي مِنْ صِدقِي رسولَ الله صلى الله عليه وسلم أنْ لا أكونَ كَذَبْتُهُ، فَأَهْلِكَ كما هَلَكَ الَّذينَ كَذَبُوا؛ إنَّ الله تَعَالَى قَالَ للَّذِينَ كَذَبُوا حِينَ أنْزَلَ الوَحْيَ شَرَّ مَا قَالَ لأَحَدٍ، فقال الله تَعَالَى: {سَيَحْلِفُونَ بِاللهِ لَكُمْ إِذَا انْقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ لِتُعْرِضُوا عَنْهُمْ فَأَعْرِضُوا عَنْهُمْ إِنَّهُمْ رِجْسٌ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ يَحْلِفُونَ لَكُمْ لِتَرْضَوْا عَنْهُمْ فَإِنْ تَرْضَوْا عَنْهُمْ فَإِنَّ اللهَ لا يَرْضَى عَنِ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ} [التوبة: 95، 96]
قَالَ كَعْبٌ: كُنّا خُلّفْنَا أيُّهَا الثَّلاَثَةُ عَنْ أمْرِ أُولئكَ الذينَ قَبِلَ مِنْهُمْ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم حِينَ حَلَفُوا لَهُ فَبَايَعَهُمْ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمْ وأرجَأَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم أمْرَنَا حَتَّى قَضَى الله تَعَالَى فِيهِ بذِلكَ. قَالَ الله تَعَالَى: {وَعَلَى الثَّلاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا} وَليْسَ الَّذِي ذَكَرَ مِمَّا خُلِّفْنَا تَخلُّفُنَا عن الغَزْو، وإنَّمَا هُوَ تَخْلِيفُهُ إيّانا وإرْجَاؤُهُ أمْرَنَا عَمَّنْ حَلَفَ لَهُ واعْتَذَرَ إِلَيْهِ فقبِلَ مِنْهُ. مُتَّفَقٌ عليه
وفي رواية: أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم خَرَجَ في غَزْوَةِ تَبْوكَ يَومَ الخَميسِ وكانَ يُحِبُّ أنْ يخْرُجَ يومَ الخمِيس
وفي رواية: وكانَ لا يقْدمُ مِنْ سَفَرٍ إلا نَهَارًا في الضُّحَى، فإِذَا قَدِمَ بَدَأَ بالمَسْجِدِ فَصَلَّى فِيهِ رَكْعَتَيْنِ ثُمَّ جَلَسَ فِيهِ
'Abdullaah bin Ka’b bin Maalik alikuwa miongoni mwa watoto wake anamuongoza Ka’b (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alipokuwa kipofu; amesema: “Nilimsikia Ka’b bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akihadithia kisa chake alipobaki nyuma ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika vita vya Tabuwk; Ka’b ameeleza: “Sijawahi kamwe kubaki nyuma ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika vita vovote alivyopigana ila katika vita vya Tabuwk. Sikushiriki vita vya Badr. Hakulaumiwa yeyote yote aliyebaki nyuma. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka pamoja na Waislamu wakiukusudia msafara wa Maquraysh hadi Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Aliwakutanisha na adui zao bila ya maagano. Nilishuhudia pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) usiku wa ‘Aqabah wakati tulipoandikiana mkataba juu ya Uislamu. Sipendelei kulinganisha hayo na vita vya Badr japokuwa Badr vinatajwa zaidi kuliko ‘Aqabah.
Ama khabari yangu kuhusu vita hivi vya Tabuwk ni pale nilipobaki nyuma ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nami sijapatapo kuwa ni mwenye nguvu na pesa kama nilipobakia nyuma katika vita hivi. Wa-Allaahi sijawahi kuwa na ngamia wawili katu kabla ya hapo isipokuwa wakati wa vita hivyo. Alipokuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anataka kupigana vita alikuwa anaficha niyyah yake kwa kutaja vita vingine mpaka ilipofikia vita hivyo ambavyo alipigana katika siku za joto kali na akaelekea kwenye safari ya mbali na bara refu lenye maji kidogo. Akawapokea watu wengi, akawabainishia wazi Waislamu jambo lao (sehemu wanayokwenda) ili wajiandae kwa maandalizi ya vita hivyo. Akawaeleza sehemu anayoikusudia. Wakati huo Waislamu walikuwa wengi pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wala hakuna kitabu kinachoweza kuwajumuisha (yaani kitabu cha majina yao). Yeyote anayetaka kutoroka angelidhani kuwa anaweza kufanya hivyo madamu Wahyi haujateremka kutoka kwa Allaah. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akapigana vita hivyo wakati matunda yalipokuwa tayari (msimu wa mavuno), nami nilikuwa nikiyapendelea (mazao). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akajiandaa pamoja na Maswahaba zake, na nikawa nimepambaukiwa ili kujitayarisha pamoja naye.
Nikarudi wala sikufanya chochote, nikajiambia: “Naweza kufanya hivyo.” Hivyo nikawa najichelewesha mpaka Waislamu wakawa tayari na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakaondoka nami sijajitayarisha chochote. Asubuhi baada ya kuwa wao wameondoka nilitoka ili kujitayarisha lakini nilirudi bila ya kufanya chochote. Kisha pia asubuhi ya pili yake nilitoka na kurudi bila kufanya chochote. Hivyo ndivyo hali yangu mpaka wakawa wametoka na nikakosa hivyo vita. Hata hivyo nilitia niyyah kuondoka na kuwapata njiani; natamani kuwa ningefanya hivyo! Nikawa kila ninapotoka nje kutembea kati ya watu waliobaki ilinihuzunisha kuwa sikumuona mtu isipokuwa aliyetuhumiwa kwa unafiki au mtu dhaifu aliyepewa udhuru na Allaah.
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakunikumbuka mpaka alipofika Tabuwk. Akasema akiwa amekaa na watu huko: “Ka’b bin Maalik amefikwa na nini?” Mtu mmoja katika kabila la Banu Salamah akasema: “Ee Rasuli wa Allaah, amezuiliwa kutazama nguo zake (yaani: anajiona).” Mu’aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akamwambia: “Umesema jambo baya! Wa-Allaahi ee Rasuli wa Allaah, hatumjui ila kwa khayr tu.” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akanyamaza. Alipokuwa yupo katika hali hiyo, alimuona mtu aliyevaa nguo nyeupe akipeperushwa na sarabi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Kuwa Abuu Khaythamah.” Akawa ndiye Abuu Khaythamah Al-Answaariyy, naye ndiye aliyetoa swadaqah pishi la tende pale wanafiki walipombeza.
Nilipopata khabari kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameelekea kuanza kurudi kutoka Tabuwk, nilijiwa na huzuni, nikawa nawaza niseme uongo, nikasema: “Vipi kesho nitaweza kuepuka na ghadhabu Zake Allaah?” Nikawa nikiomba usaidizi kwa jambo hilo kwa kila mwenye maoni miongoni mwa jamaa zangu. Nilipoambiwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameshakaribia kufika, uongo uliniondokea hata nikawa najua siwezi kumuepuka kwa lolote kabisa. Nikaamua kumueleza ukweli.
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaporejea safari yoyote, huanza kuteremkia Masjid kuswali rakaa mbili kisha huketi na watu. Alipofanya hivyo alijiwa na wale watu waliorudi nyuma wakimtolea nyudhuru na wakimuapia. Walikuwa ni watu zaidi ya themanini. Akawakubalia nyudhuru zao, akachukua bay'ah (kiapo cha utiifu), akawaombea maghfirah na siri zao akamuachia Allaah (Subhaanhu wa Ta’aalaa).
Nikaja mimi, nikamtolea salaam akatabasamu, tabasamu ya mtu aliyekasirishwa, akaniambia: “Njoo.” Nikaenda mpaka nikakaa kitako mbele yake. Akaniuliza: “Ni jambo gani lililokubakisha nyuma? Hukuwa umenunua ngamia?” Nikamwambia: “Ee Rasuli wa Allaah, Wa-Allaahi mimi lau ningalikuwa niko mbele ya mtu mwengine asiyekuwa wewe katika watu wa kidunia, ningaliona naweza kuepuka hasira zake kwa udhuru. Hakika nimepewa ufasaha na nguvu ya kusema, Lakini Wa-Allaahi najua kuwa iwapo nitakuzungumzia uongo leo utakaoniridhia, itakaribia Allaah Akutie hasira juu yangu. Na nikizungumza mazungumzo ya kweli, utanikasirikia. Mimi nataraji mwisho mwema wa Allaah ‘Azza wa Jallaa. Wa-Allaahi sikuwa nina udhuru. Wa-Allaahi, nilikuwa nina nguvu na wepesi nilipobakia nyuma!” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Ama huyu amesema kweli. Nenda mpaka Allaah Atakapokuhukumu.”
Watu katika kabila la Banu Salamah wakanifuata, wakanambia: “Wa-Allaahi hatukujui kama umeshawahi kufanya kosa kabla ya hili. Umeshindwa kutoa udhuru kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama walivyotoa wale wengine waliokuwa wamebaki nyuma? Dhambi yako ingalifutwa na istighfaar na du’aa ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) “Basi Wa-Allaahi, hawakuacha kunilaumu mpaka nikataka kumrudia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ili nijikadhibishe. Kisha nikawauliza: “Kuna yeyote aliyemkabili na jambo kama langu?” Wakajibu: “Ndio, watu wawili walimkabili wakasema mithli ya ulivyosema, wakaambiwa kama ulivyoambiwa.” Nikauliza: “Ni nani hao?” Wakajibu: “Muraarah bin Rabiy’ Al-‘Amriy na Hilaal bin Umayyah Al-Waaqify.” Wakanitajia watu wawili wema waliohudhuria vita vya Badr wenye kiigizo. Waliponitajia hao, nikaenda zangu.
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawakataza watu kuzungumza nasi watu watatu pekee miongoni mwa watu waliobaki nyuma. Watu wakatuepuka, au wakatubadilikia mpaka ardhi nikaiona moyoni mwangu imebadilika, si ardhi niijuayo! Tukawa katika hali hiyo masiku khamsini. Ama wale wenzangu wawili, walikuwa wametulia kwa unyenyekevu majumbani mwao wakilia tu. Lakini mimi nilikuwa kijana na mwenye nguvu. Nikawa nikitoka nikihudhuria Swalaah (za jamaa’ah) pamoja na Waislamu wengine, nilitembea masokoni wala hakuna yoyote anayenizungumzisha. Nikamuendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nikamtolea salaam naye yupo katika majlis yake baada ya kuswali; nikajiuliza moyoni mwangu: “Ameitikia midomo yake kwa kuirejesha salaam?” Kisha nikaswali karibu yake naye nikimtazama kwa kuibia, nikielekea katika Swalaah yangu naye hunitazama, nikielekea upande wake hugeuka.
Jambo hilo likarefuka kwangu kutokana na Waislamu kujitenga. Nikauparamia ukuta wa bustani ya Abuu Qataadah naye ni bin 'ammi yangu na ni kipenzi zaidi kwangu; nikamsalimia; basi wa-Allaahi hakunirejeshea salaam. Nikamwambia: “Ee Abuu Qataadah, nakuomba kwa jina la Allaah, je, unajua kuwa mimi nampemda Allaah na Rasuli Wake?” Akanyamaza, nikarejea tena nikamuomba akanyamaza. Nikarejea tena nikamuomba, akasema: “Allaah na Rasuli Wake Wanajua Zaidi.” Macho yangu yakabubujika machozi, nikaenda na kuuparamia ukuta.
Nilipokuwa natembea katika soko la Madiynah, nikamuona mkulima kutoka Shaam aliyekuja kuuza nafaka Madiynah, akaniuliza: “Ni nani atakayenionesha Ka’b bin Maalik?” Watu wakawa wanamuelekeza kwangu, akanijia na kunipatia barua inayotoka kwa mfalme Ghassaan, nami nilikuwa nikijua kusoma na kuandika. Nikaisoma ilikuwa imeandikwa: “Ama baada ya haya. Tumepata habari kuwa mwenzako amekuepuka, wala Allaah hajakujaalia kuwa katika nchi ya unyonge wala haki yako kupotea. Njoo kwetu tutakunafisi.” Nilipomaliza kuisoma, nilisema: “ Hii ni balaa nyingine!” Nikaichukua barua nikaitia katika tanuri na nikaichoma.
Zikapita siku arubaini kati ya zile siku khamsini, wahyi ukachelewa. Mara kwa ghafla mjumbe wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akanijia, akaniambia: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anakuambia umuepuke mkeo.” Nikauliza: “Nimtaliki au nifanyeje?” Akaniambia: “Hapana, kuwa mbali naye wala usimkurubie kabisa.” Akawatumia wenzangu kama hivyo. Nikamwambia mke wangu: “Nenda kwa jamaa zako uwe huko mpaka Allaah Atakapotoa hukumu katika jambo hili.” Mke wa Hilaal bin Umayyah akamwendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Ee Rasuli wa Allaah, hakika Hilaal bin Umayyah ni mzee dhaifu na hana mtumishi, je, utachukia nikimhudumia?” Akajibu: “Hapana, lakini asijaribu kukukurubia.” Akasema: “Wa-Allaahi hawezi kutaharaki kukaribia chochote, na wa-Allaahi bado analia tokea yalipomtokea hadi leo hii!” Baadhi ya jamaa zangu wakaniambia: “Lau ungalimuomba udhuru Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu mkeo; kwani mke wa Hilaal bin Umayyah ameruhusiwa amhudumie. Nikasema: “Siwezi kumuomba idhini (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya mke wangu, nitajua lipi atakaloniambia (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwani mimi ni kijana!
Nikakaa kitako katika hali hiyo masiku kumi. Yakakamilika masiku khamsini tangu watu walipokatazwa nasi. Asubuhi ya kupambaukiwa siku ya khamsini, Niliswali Swalaah ya Alfajiri juu ya nyumba miongoni mwa majumba yetu. Nilipokuwa nimekaa kitako katika hali Aliyoitaja Allaah kutuhusu, nafsi yangu ikadhikika kwangu na ardhi ikawa dhiki kwangu ingawa ardhi hiyo ni kunjufu, nikaisikia sauti ya ukelele kutoka katika jabali la Sal’i, mtu akisema kwa sauti ya juu kabisa: “Ee Ka’b bin Maalik! Pokea bishara njema!” Nikaanguka kifudifudi kwa kusujudu, nikajua kuwa faraja imekuja. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kuswali Swalaah ya Alfajiri amewajulisha watu juu ya tawbah yetu kwa Allaah (‘Azza wa Jallaa). Watu wakawa wakitupa bishara njema, watoaji biashara wakawaendea wenzangu wawili. Mtu mmoja akapanda farasi akanijia mbio, na mwengine katika kabila la Aslam aliyepanda juu ya jabali sauti yake ikanifikia haraka zaidi kulikoni yule mpanda farasi. Na aliponijia yule niliyemsikia sauti akinibashiria. Nilimvulia nguo zangu mbili na nikamvisha kwa sababu ya ile bishara yake. Wa-Allaahi siku hiyo nilikuwa sikumiliki isipokuwa nguo hizo tu. Nikaazima nguo mbili nikazivaa. Nikaondoka nikimkusudia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Nilipokuwa njiani, watu walikuwa wakikutana na mimi makundi kwa makundi wakinipa pongezi ya tawbah na wakiniambia: “Hongera kwa kupokelewa Tawbah na Allaah.”
Nilipoingia Masjid, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawa amekaa kitako kando yake kuna watu. Twalhah bin ‘Ubaydillaah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akainuka mbio kunipa mkono na kunipa pongezi. Wa-Allaahi hakuna yoyote katika Muhaajiriyn aliyeinuka isipokuwa ni yeye tu. Nikawa simsahau Twalhah kwa jambo hilo. Nilipomsalimia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema huku sura yake ikimeremeta kwa furaha: “Pokea bishara ya khayr siku iliyo bora toka uzaliwe.” Nikauliza: “Ni kutoka kwako ee Rasuli wa Allaah?” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akipatwa na furaha basi sura yake hung’aa kama kipande cha mwezi, jambo hilo tulikuwa tukilijua kwake. Nilipokaa kitako mbele yake, nilimwambia: “Ee Rasuli wa Allaah, kwa sababu ya kukubaliwa tawbah yangu nitatoa mali yangu yote kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake.” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: “Zuia baadhi ya mali yako, kwani hiyo ni khayr kwako.” Nikamwambia: “Mimi naizuia sehemu yangu iliopo Khaybar.” Na nikamwambia: “Ee Rasuli wa Allaah, hakika Allaah Ameniokoa kwa sababu ya ukweli wangu. Hivyo naahidi kuwa katika uhai wangu wote sitosema isipokuwa ukweli.”
Wa-Allaahi simjui yeyote kati ya Waislamu ambaye Allaah Alimsaidia kusema ukweli kuliko mimi. Wa-Allaahi sikusema uongo tangu nilipomwambia ukweli Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka siku yangu hii leo. Nami nataraji Allaah Atanihifadhi kusema uongo maisha yangu yote. Allaah Akateremsha:
لَّقَد تَّابَ اللَّـهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ الْعُسْرَةِ مِن بَعْدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٍ مِّنْهُمْ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّهُ بِهِمْ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١١٧﴾
Kwa yakini Allaah Amepokea tawbah ya Nabiy na Muhajirina na Answaar ambao wamemfuata (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) katika saa ya dhiki (vita vya Tabuwk) baada ya nyoyo za kundi miongoni mwao zilikaribia kuelemea mbali na haki (Allaah) Akapokea tawbah yao. Hakika Yeye kwao ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.
وَعَلَى الثَّلَاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا حَتَّىٰ إِذَا ضَاقَتْ عَلَيْهِمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ وَضَاقَتْ عَلَيْهِمْ أَنفُسُهُمْ وَظَنُّوا أَن لَّا مَلْجَأَ مِنَ اللَّـهِ إِلَّا إِلَيْهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ لِيَتُوبُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ﴿١١٨﴾
Na (pia Allaah Akapokea tawbah) ya wale watatu waliobaki nyuma (kutokwenda vita vya Tabuwk; wakajuta mno) mpaka ardhi ikadhikika kwao juu ya kuwa ni pana na zikadhikika nafsi zao, na wakatambua kwamba hakuna pa kumkimbia Allaah isipokuwa (kuelekea) Kwake; kisha (Allaah) Akapokea tawbah yao, ili watubie. Hakika Allaah Yeye Ndiye Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ﴿١١٩﴾
Enyi walioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli. [At-Tawbah: 117- 119]
Wa-Allaahi Hakunineemesha neema yoyote katu baada ya kuniongoza katika Uislamu, neema iliyo kubwa moyoni mwangu kuliko kumwambia ukweli Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Lau ningesema uongo Angeniangamiza kama Alivyowaangamiza wale waliosema uongo. Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amewaonya vibaya zaidi wasemao uongo kuliko yeyote; Akasema:
سَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَكُمْ إِذَا انقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ لِتُعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ فَأَعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ إِنَّهُمْ رِجْسٌ ۖ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٩٥﴾
Watakuapieni kwa Allaah, mtakaporudi kwao ili muwapuuze. Basi wapuuzeni; hakika wao ni rijs (uchafu) na makazi yao ni (Moto wa) Jahannam. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.
يَحْلِفُونَ لَكُمْ لِتَرْضَوْا عَنْهُمْ ۖ فَإِن تَرْضَوْا عَنْهُمْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يَرْضَىٰ عَنِ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ﴿٩٦﴾
Watakuapieni ili muwaridhie. Mkiwaridhia, basi hakika Allaah Haridhii watu mafasiki. [At-Tawbah 95-96]
Sisi watatu tulitofautiana na wale walioapa mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawakubalia nyudhuru zao, akachukua bay'ah yao na kuwaombea maghfirah. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliacha kadhia yetu ibakie mpaka Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akahukumu. Allaah Anasema:
وَعَلَى الثَّلاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا
Na (pia Allaah Akapokea tawbah) ya wale watatu waliobaki nyuma (kutokwenda vita vya Tabuwk; wakajuta mno) [At-Tawbah; 118]
Hapa haizungumziwi kuhusu kubaki kwetu nyuma kutokwenda vitani. Bali muradi wake ni vile Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyoiakhirisha kadhia yetu kinyume na kadhia ya wale walitoa nyudhuru kwa kula viapo akawakubalia.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riwaayah nyingine inasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka katika vita vya Tabuwk siku ya Alkhamisi na alikuwa akipenda kusafiri siku ya Alkhamisi.
Riwaayah nyingine pia inasema: “Na alikuwa harudi kutoka safari ila mchana katika wakati wa Dhwuhaa anapokuja huanza kuteremkia Masjid akiswali humo rakaa mbili kisha akikaa kitako.
Hadiyth – 10
وَعَنْ أبي نُجَيد- بضَمِّ النُّونِ وفتحِ الجيم- عِمْرَانَ بنِ الحُصَيْنِ الخُزَاعِيِّ رضي الله عنهما: أنَّ امْرَأةً مِنْ جُهَيْنَةَ أتَتْ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم وَهِيَ حُبْلَى مِنَ الزِّنَى، فقالتْ: يَا رسولَ الله، أصَبْتُ حَدًّا فَأَقِمْهُ عَلَيَّ، فَدَعَا نَبيُّ الله صلى الله عليه وسلم وَليَّها، فقالَ: ((أَحْسِنْ إِلَيْهَا، فإذا وَضَعَتْ فَأْتِني)) فَفَعَلَ فَأَمَرَ بهَا نبيُّ الله صلى الله عليه وسلم، فَشُدَّتْ عَلَيْهَا ثِيَابُهَا، ثُمَّ أَمَرَ بِهَا فَرُجِمَتْ، ثُمَّ صَلَّى عَلَيْهَا. فقالَ لَهُ عُمَرُ: تُصَلِّي عَلَيْهَا يَا رَسُول الله وَقَدْ زَنَتْ؟ قَالَ: ((لَقَدْ تَابَتْ تَوْبَةً لَوْ قُسِمَتْ بَيْنَ سَبْعِينَ مِنْ أهْلِ المَدِينَةِ لَوَسِعَتْهُمْ، وَهَلْ وَجَدْتَ أَفضَلَ مِنْ أنْ جَادَتْ بنفْسِها لله- عز وجل-؟!)). رواه مسلم
Abuu Nujayd, ‘Imraan bin Huswayn Al-Khuza'iy (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amehadithia kwamba: Mwanamke kutoka kabila la Juhaynah alimuendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye ana mimba ya zinaa, akamwambia: “Ee Rasuli wa Allaah, nimetenda dhambi inayopaswa haddi (adhabu), kwa hiyo nipitishie.” Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwita msimamizi wake, akamwambia: “Mfanyie ihsaan atakapojifungua mlete.” Yule msimamizi akafanya kama alivyoamrishwa, halafu akaja naye. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaamuru, akafungwe kwa nguo zake, halafu akaamuru arajimiwe, kisha akamswalia. ‘Umar akamwambia: “Ee Rasuli wa Allaah, unamswalia na hali alikuwa amezini?” Akamwambia: “Kwa yakini ametubia tawbah ambayo lau ingeligawanya kwa watu sabini miongoni mwa watu wa Madiynah, ingewatosha. Je, ushawahi kuona lililo bora kuliko yeye kujileta mwenyewe kwa Allaah (‘Azza wa Jalla)?” [Muslim]
Hadiyth – 11
وعن ابنِ عباسٍ رضي الله عنهما أنَّ رَسُولَ الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((لَوْ أنَّ لابنِ آدَمَ وَادِيًا مِنْ ذَهَبٍ أحَبَّ أنْ يكُونَ لَهُ وَادِيانِ، وَلَنْ يَمْلأَ فَاهُ إلا التُّرَابُ، وَيَتْوبُ اللهُ عَلَى مَنْ تَابَ)). مُتَّفَقٌ عليه
'Abdullaah bin ‘Abbaas na Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) wamehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Lau mwana Aadam angalikuwa na bonde la dhahabu, angalipendelea awe na mabonde mawili, wala hakuna kitakachoweza kumtosheleza mdomo wake isipokuwa ni mchanga. Na Allaah Humkubalia tawbah ya yule mwenye kutubia.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 12
وعن أبي هريرة رضي الله عنه أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((يَضْحَكُ اللهُ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَى إِلَى رَجُلَيْنِ يقْتُلُ أَحَدهُمَا الآخَرَ يَدْخُلانِ الجَنَّةَ، يُقَاتِلُ هَذَا في سَبيلِ اللهِ فَيُقْتَلُ، ثُمَّ يتُوبُ اللهُ عَلَى القَاتلِ فَيُسْلِم فَيُسْتَشْهَدُ)). مُتَّفَقٌ عليه
Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Huwacheka watu wawili, mmoja anamuua mwengine, wote wakaingia Jannah. Huyu atapigana na huyu katika njia ya Allaah, atauliwa. Kisha Allaah Atamsamehe aliyeua kwa kusilimu naye akafa shahiyd.” [Al-Bukhaariy na Muslim]