003-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Subira

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب الصبر

003 – Mlango Wa Subira

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

Enyi walioamini! Subirini na zidini kuvuta subira na bakieni imara na mcheni Allaah ili mpate kufaulu. [Al-Baqarah: 200]

 

وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ

Na bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao. Na wabashirie wenye kusubiri. [Al-Baqarah: 155]

 

قُلْ يَا عِبَادِ الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا رَبَّكُمْ ۚ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةٌ ۗ وَأَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةٌ ۗ إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ

Sema: “Enyi waja Wangu ambao mmeamini, mcheni Rabb wenu. Kwa wale waliofanya mazuri katika dunia hii watapata mazuri. Na ardhi ya Allaah ni pana. Hakika wanaosubiri watalipwa kikamilifu ujira wao bila ya hesabu. [Az-Zumar: 10]

 

وَلَمَن صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ

Na atakayevuta subira na akasamehe, hakika hilo bila shaka ni katika mambo ya kuazimiwa. [As-Shuwra: 43]

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ

Enyi walioamini! Tafuteni msaada kwa subira na Swalaah; hakika Allaah Yu pamoja na wanaosubiri. [Al-Baqarah: 153]

 

وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ حَتَّىٰ نَعْلَمَ الْمُجَاهِدِينَ مِنكُمْ وَالصَّابِرِينَ وَنَبْلُوَ أَخْبَارَكُمْ

Na bila shaka Tutakujaribuni mpaka Tutambue wenye kufanya jihaad miongoni mwenu na wenye kuvuta subira na tutazitahini habari zenu. [Muhammad: 31]

 

Aayah zinazoamrisha subira na kubainisha fadhila zake ni nyingi na mashuhuri.

 

 

Hadiyth – 1

وعن أبي مالكٍ الحارث بن عاصم الأشعريِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((الطُّهُورُ شَطْرُ الإِيمان، وَالحَمدُ لله تَمْلأُ الميزَانَ، وَسُبْحَانَ الله والحَمدُ لله تَملآن- أَوْ تَمْلأُ- مَا بَينَ السَّماوات وَالأَرْضِ، والصَّلاةُ نُورٌ، والصَّدقةُ بُرهَانٌ، والصَّبْرُ ضِياءٌ، والقُرْآنُ حُجةٌ لَكَ أَوْ عَلَيْكَ. كُلُّ النَّاسِ يَغْدُو فَبَائعٌ نَفسَهُ فَمُعْتِقُهَا أَوْ مُوبِقُها)). رواه مسلم

Abuu Maalik, Al-Haarith bin ‘Aaswim Al-Ash’ariy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Wudhuu ni nusu ya iymaan, (kusema:) AlhamduliLLaah hujaza miyzaan, Subhaana Allaah wal-HamduliLLaah hujaza baina ya mbingu na ardhi, Swalaah ni nuru, Swadaqah ni hojja (kwa mwenye iymaan na kuitoa), subira ni mwangaza na Qur-aan ni hojja ya kukuokoa au kukuangamiza. Kila mtu huifanyia ‘amali nafsi yake, kuna mwenye kujiuza, mwenye kujiacha huru au mwenye kujiangamiza.” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أبي سَعيد سعدِ بن مالكِ بنِ سنانٍ الخدري رضي الله عنهما: أَنَّ نَاسًا مِنَ الأَنْصَارِ سَألوا رسولَ الله صلى الله عليه وسلم فَأعْطَاهُمْ، ثُمَّ سَألوهُ فَأعْطَاهُمْ، حَتَّى نَفِدَ مَا عِندَهُ، فَقَالَ لَهُمْ حِينَ أنْفْقَ كُلَّ شَيءٍ بِيَدِهِ: ((مَا يَكُنْ عِنْدي مِنْ خَيْر فَلَنْ أدَّخِرَهُ عَنْكُمْ، وَمَنْ يَسْتَعْفِفْ يُعِفهُ اللهُ، وَمَنْ يَسْتَغْنِ يُغْنِهِ اللهُ، وَمَنْ يَتَصَبَّرْ يُصَبِّرْهُ اللهُ. وَمَا أُعْطِيَ أَحَدٌ عَطَاءً خَيْرًا وَأوْسَعَ مِنَ الصَّبْر)). مُتَّفَقٌ عليه

Abuu Sa’iyd, Sa’d bin Maalik bin Sinaan Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: “Watu fulani miongoni mwa Answaar walimuomba Rasuli  wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), naye akawapa, kisha wakamuomba tena, naye akawapa mpaka akamaliza chote alichokuwa nacho. Akawaambia baada ya kuwa ameshatoa kila kitu: “Khayr yoyote niliyonayo siwezi kuwanyima, mwenye kujizuia kuomba Allaah Atamlipa kwa kutoomba, mwenye kutosheka basi na Allaah Atamtosheleza zaidi, na Atakae jisubirisha basi na Allaah Atamzidishia subira. Hakuna yoyote yule aliyepewa zawadi bora na iliyokunjufu zaidi kulikoni subira.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

 وعن أبي يحيى صهيب بن سنانٍ رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((عَجَبًا لأمْرِ المُؤمنِ إنَّ أمْرَهُ كُلَّهُ لَهُ خيرٌ ولَيسَ ذلِكَ لأَحَدٍ إلا للمُؤْمِن: إنْ أَصَابَتْهُ سَرَّاءُ شَكَرَ فَكانَ خَيرًا لَهُ، وإنْ أصَابَتْهُ ضرَاءُ صَبَرَ فَكانَ خَيْرًا لَهُ)). رواه مسلم

Abuu Yahyaa, Swuhayb bin Sinaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ajabu kwa jambo la Muumin; hakika mambo yake ni khayr, wala hakuna anayepata hilo isipokuwa Muumin pekee; akipatwa na furaha hushukuru basi huwa ni khayr kwake, na akipatwa na madhara husubiri basi huwa khayr kwake.” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 4

وعن أنَسٍ رضي الله عنه قَالَ: لَمَّا ثَقُلَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم جَعلَ يَتَغَشَّاهُ الكَرْبُ، فَقَالَتْ فَاطِمَةُ رضي الله عنها: وَاكَربَ أَبَتَاهُ. فقَالَ: ((لَيْسَ عَلَى أَبيكِ كَرْبٌ بَعْدَ اليَوْمِ)) فَلَمَّا مَاتَ، قَالَتْ: يَا أَبَتَاهُ، أَجَابَ رَبًّا دَعَاهُ! يَا أَبتَاهُ، جَنَّةُ الفِردَوسِ مَأْوَاهُ! يَا أَبَتَاهُ، إِلَى جبْريلَ نَنْعَاهُ! فَلَمَّا دُفِنَ قَالَتْ فَاطِمَةُ رَضي الله عنها: أَطَابَتْ أنْفُسُكُمْ أنْ تَحْثُوا عَلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم التُّرَابَ؟! رواه البخاري.

Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mambo yalivyomzidia uzito, ukamjia uchungu wa mauti, Faatwimah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) akasema: “Ee uchungu gani unaomshika baba yangu.”  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Baba yako hatoteseka baada ya leo.” Alipofariki Faatwimah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) akasema: “Ee baba yangu ameitika wito wa Rabb wake! Ee baba yangu Jannah ya Al-Firdaws ndio mashukio yake. Ee baba yangu! Kwa Jibriyl tunamuombeleza!” Alipozikwa, Faatwimah alisema: “Nyoyo zenu zimeridhika kwa kumiminia mchanga Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)?” [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 5

وعن أبي زَيدٍ أُسَامَةَ بنِ زيدِ بنِ حارثةَ مَوْلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم وحِبِّه وابنِ حبِّه رضي اللهُ عنهما، قَالَ: أرْسَلَتْ بنْتُ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم إنَّ ابْني قَد احْتُضِرَ فَاشْهَدنَا، فَأَرْسَلَ يُقْرئُ السَّلامَ، ويقُولُ: ((إنَّ لله مَا أخَذَ وَلَهُ مَا أعطَى وَكُلُّ شَيءٍ عِندَهُ بِأجَلٍ مُسَمًّى فَلتَصْبِرْ وَلْتَحْتَسِبْ)) فَأَرسَلَتْ إِلَيْهِ تُقْسِمُ عَلَيهِ لَيَأتِينَّهَا. فقامَ وَمَعَهُ سَعْدُ بْنُ عُبَادَةَ، وَمُعَاذُ بْنُ جَبَلٍ، وَأُبَيُّ بْنُ كَعْبٍ، وَزَيْدُ بْنُ ثَابتٍ، وَرجَالٌ رضي الله عنهم، فَرُفعَ إِلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم الصَّبيُّ، فَأقْعَدَهُ في حِجْرِهِ وَنَفْسُهُ تَقَعْقَعُ، فَفَاضَتْ عَينَاهُ فَقالَ سَعدٌ: يَا رسولَ الله، مَا هَذَا؟ فَقالَ: ((هذِهِ رَحمَةٌ جَعَلَها اللهُ تَعَالَى في قُلُوبِ عِبَادِهِ)) وفي رواية: ((فِي قُلُوبِ مَنْ شَاءَ مِنْ عِبَادِهِ، وَإِنَّما يَرْحَمُ اللهُ مِنْ عِبادِهِ الرُّحَماءَ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Abuu Zayd, Usaamah bin Zayd bin Haarithah muachwa huru wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kipenzi chake na ni mwana wa kipenzi chake (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Binti mmoja wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimpelekea salaamu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa “Mwana wangu amejiwa na umauti, basi njoo.” Naye akamtuma mtu akimpelekea salaamu na akamwambia: “Allaah Ana khiyari ya kuchukua Anachotaka na kutoa Anachotaka. Kila kitu Kwake kina muda maalumu, basi asubiri na taraji malipo kwa Allaah.” Akamtumia tena ujumbe akimuapia aende. Akasimama, pamoja naye alikuwepo Sa’d bin ‘Ubaadah, Mu’aadh bin Jabal, Ubayyi bin Ka’b, Zayd bin Thaabit na wengineo (Radhwiya Allaahu ‘anhum). Yule mtoto akapelekewa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), akamkalisha katika paja lake na nafsi ya yule mtoto ikiwa katika hali ya woga, macho ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yakabubujikwa na machozi, Sa’d akauliza: “Una nini yaa Rasula-Allaah?” Akamwambia: “Hii ni rahmah, Allaah Amejaalia katika nyoyo za waja Wake.”

Riwaayah nyingine imesema: “Katika nyoyo za Anaowataka miongoni mwa waja Wake. Hakika Allaah Huwarehemu wenye huruma katika waja Wake.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 6

وعن صهيب رضي الله عنه: أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((كَانَ مَلِكٌ فيمَنْ كَانَ قَبلَكمْ وَكَانَ لَهُ سَاحِرٌ فَلَمَّا كَبِرَ قَالَ للمَلِكِ: إنِّي قَدْ كَبِرْتُ فَابْعَثْ إلَيَّ غُلامًا أُعَلِّمْهُ السِّحْرَ؛ فَبَعثَ إِلَيْهِ غُلامًا يُعَلِّمُهُ، وَكانَ في طرِيقِهِ إِذَا سَلَكَ رَاهِبٌ، فَقَعدَ إِلَيْه وسَمِعَ كَلامَهُ فَأعْجَبَهُ، وَكانَ إِذَا أتَى السَّاحِرَ، مَرَّ بالرَّاهبِ وَقَعَدَ إِلَيْه، فَإذَا أَتَى السَّاحِرَ ضَرَبَهُ، فَشَكَا ذلِكَ إِلَى الرَّاهِب، فَقَالَ: إِذَا خَشيتَ السَّاحِرَ، فَقُلْ: حَبَسَنِي أَهْلِي، وَإذَا خَشِيتَ أهلَكَ، فَقُلْ: حَبَسَنِي السَّاحِرُ.

فَبَيْنَما هُوَ عَلَى ذلِكَ إِذْ أَتَى عَلَى دَابَّةٍ عَظِيمَةٍ قَدْ حَبَسَتِ النَّاسَ فَقَالَ: اليَوْمَ أعْلَمُ السَّاحرُ أفْضَلُ أم الرَّاهبُ أفْضَلُ؟ فَأخَذَ حَجَرًا، فَقَالَ: اللَّهُمَّ إنْ كَانَ أمْرُ الرَّاهِبِ أَحَبَّ إِلَيْكَ مِنْ أمْرِ السَّاحِرِ فَاقْتُلْ هذِهِ الدّابَّةَ حَتَّى يَمضِي النَّاسُ، فَرَمَاهَا فَقَتَلَها ومَضَى النَّاسُ، فَأتَى الرَّاهبَ فَأَخبَرَهُ. فَقَالَ لَهُ الرَّاهبُ: أَيْ بُنَيَّ أَنْتَ اليَومَ أفْضَل منِّي قَدْ بَلَغَ مِنْ أَمْرِكَ مَا أَرَى، وَإنَّكَ سَتُبْتَلَى، فَإن ابْتُلِيتَ فَلا تَدُلَّ عَلَيَّ؛ وَكانَ الغُلامُ يُبْرىءُ الأكْمَهَ وَالأَبْرصَ، ويداوي النَّاسَ مِنْ سَائِرِ الأَدْوَاء. فَسَمِعَ جَليسٌ لِلملِكِ كَانَ قَدْ عَمِيَ، فأتاه بَهَدَايا كَثيرَةٍ، فَقَالَ: مَا هاهُنَا لَكَ أَجْمعُ إنْ أنتَ شَفَيتَنِي، فَقَالَ: إنّي لا أشْفِي أحَدًا إِنَّمَا يَشفِي اللهُ تَعَالَى، فَإنْ آمَنْتَ بالله تَعَالَى دَعَوتُ اللهَ فَشفَاكَ، فَآمَنَ بالله تَعَالَى فَشفَاهُ اللهُ تَعَالَى، فَأَتَى المَلِكَ فَجَلسَ إِلَيْهِ كَما كَانَ يَجلِسُ، فَقَالَ لَهُ المَلِكُ: مَنْ رَدّ عَلَيْكَ بَصَرَكَ؟ قَالَ: رَبِّي، قَالَ: وَلَكَ رَبٌّ غَيري؟ قَالَ: رَبِّي وَرَبُّكَ اللهُ، فَأَخَذَهُ فَلَمْ يَزَلْ يُعَذِّبُهُ حَتَّى دَلَّ عَلَى الغُلامِ، فَجيء بالغُلاَمِ، فَقَالَ لَهُ المَلِكُ: أيْ بُنَيَّ، قَدْ بَلَغَ مِنْ سِحْرِكَ مَا تُبْرئ الأَكْمَهَ وَالأَبْرَصَ وتَفْعَلُ وتَفْعَلُ! فَقَالَ: إنِّي لا أَشْفي أحَدًا، إِنَّمَا يَشفِي الله تَعَالَى. فَأَخَذَهُ فَلَمْ يَزَلْ يُعَذِّبُهُ حَتَّى دَلَّ عَلَى الرَّاهبِ؛ فَجِيء بالرَّاهبِ فَقيلَ لَهُ: ارجِعْ عَنْ دِينكَ، فَأَبَى، فَدَعَا بِالمِنْشَارِ فَوُضِعَ المِنْشَارُ في مَفْرق رَأسِهِ، فَشَقَّهُ حَتَّى وَقَعَ شِقَّاهُ، ثُمَّ جِيءَ بِجَليسِ المَلِكِ فقيل لَهُ: ارْجِعْ عَنْ دِينِكَ، فَأَبَى، فَوضِعَ المِنْشَارُ في مَفْرِق رَأسِهِ، فَشَقَّهُ بِهِ حَتَّى وَقَعَ شِقَّاهُ، ثُمَّ جِيءَ بالغُلاَمِ فقيلَ لَهُ: ارْجِعْ عَنْ دِينكَ، فَأَبَى، فَدَفَعَهُ إِلَى نَفَرٍ مِنْ أصْحَابهِ، فَقَالَ: اذْهَبُوا بِهِ إِلَى جَبَلِ كَذَا وَكَذَا فَاصْعَدُوا بِهِ الجَبَل، فَإِذَا بَلَغْتُمْ ذِرْوَتَهُ فَإِنْ رَجَعَ عَنْ دِينِهِ وَإلا فَاطْرَحُوهُ. فَذَهَبُوا بِهِ فَصَعِدُوا بِهِ الجَبَلَ، فَقَالَ: اللَّهُمَّ أكْفنيهمْ بِمَا شِئْتَ، فَرَجَفَ بهِمُ الجَبلُ فَسَقَطُوا، وَجاءَ يَمشي إِلَى المَلِكِ، فَقَالَ لَهُ المَلِكُ: مَا فَعَلَ أصْحَابُكَ؟ فَقَالَ: كَفَانِيهمُ الله تَعَالَى، فَدَفَعَهُ إِلَى نَفَرٍ مِنْ أَصْحَابِهِ فَقَالَ: اذْهَبُوا بِهِ فاحْمِلُوهُ في قُرْقُورٍ وتَوَسَّطُوا بِهِ البَحْرَ، فَإنْ رَجعَ عَنْ دِينِهِ وإِلا فَاقْذِفُوهُ. فَذَهَبُوا بِهِ، فَقَالَ: اللَّهُمَّ أكْفِنيهمْ بمَا شِئْتَ، فانْكَفَأَتْ بِهمُ السَّفينةُ فَغَرِقُوا، وَجَاء يَمْشي إِلَى المَلِكِ. فَقَالَ لَهُ المَلِكُ: مَا فعلَ أصْحَابُكَ؟ فَقَالَ: كَفَانيهمُ الله تَعَالَى. فَقَالَ لِلمَلِكِ: إنَّكَ لَسْتَ بقَاتلي حَتَّى تَفْعَلَ مَا آمُرُكَ بِهِ. قَالَ: مَا هُوَ؟ قَالَ: تَجْمَعُ النَّاسَ في صَعيدٍ وَاحدٍ وتَصْلُبُني عَلَى جِذْعٍ، ثُمَّ خُذْ سَهْمًا مِنْ كِنَانَتي، ثُمَّ ضَعِ السَّهْمَ في كَبدِ القَوْسِ ثُمَّ قُلْ: بسْم الله ربِّ الغُلاَمِ، ثُمَّ ارْمِني، فَإنَّكَ إِذَا فَعَلْتَ ذلِكَ قَتَلتَني، فَجَمَعَ النَّاسَ في صَعيد واحدٍ، وَصَلَبَهُ عَلَى جِذْعٍ، ثُمَّ أَخَذَ سَهْمًا مِنْ كِنَانَتِهِ، ثُمَّ وَضَعَ السَّهْمَ في كَبِدِ القَوْسِ، ثُمَّ قَالَ: بِسمِ اللهِ ربِّ الغُلامِ، ثُمَّ رَمَاهُ فَوقَعَ في صُدْغِهِ، فَوَضَعَ يَدَهُ في صُدْغِهِ فَمَاتَ، فَقَالَ النَّاسُ: آمَنَّا بِرَبِّ الغُلامِ، فَأُتِيَ المَلِكُ فقيلَ لَهُ: أَرَأَيْتَ مَا كُنْتَ تَحْذَرُ قَدْ والله نَزَلَ بكَ حَذَرُكَ. قَدْ آمَنَ النَّاسُ. فَأَمَرَ بِالأُخْدُودِ بأفْواهِ السِّكَكِ فَخُدَّتْ وأُضْرِمَ فيهَا النِّيرانُ وَقَالَ: مَنْ لَمْ يَرْجعْ عَنْ دِينهِ فَأقْحموهُ فيهَا، أَوْ قيلَ لَهُ: اقتَحِمْ فَفَعَلُوا حَتَّى جَاءت امْرَأةٌ وَمَعَهَا صَبيٌّ لَهَا، فَتَقَاعَسَتْ أنْ تَقَعَ فيهَا، فَقَالَ لَهَا الغُلامُ: يَا أُمهْ اصْبِري فَإِنَّكِ عَلَى الحَقِّ!)). رواه مسلم

Swuhayb (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Alikuwepo mfalme kabla ya zama zenu. Alikuwa anae mchawi, yule mchawi alipozeeka alimwambia mfalme: “Mimi nimezeeka, niletee kijana nitakaemfunza uchawi.” (mfalme) akampelekea kijana ili amfunze. Alikuwa (yule kijana) katika njia anayoelekea kuna Rahibu (mtawa mwanaume). Akakaa kumsikiliza, akapendezewa na maneno yake, na alikuwa akitaka kumuendea mchawi yule hupita kwa Rahibu yule na kukaa naye na kumsikiliza, anapomwendea mchawi, humpiga. Jambo hili akamshitakia yule mtawa. (Mtawa) akamwambia: “Utakapomuendea mchawi mwambie: ‘Nimezuiliwa na watu wangu,’ na unapowarudia watu wako, waambie: Nimezuiliwa na mchawi.” Alipokuwa akiendelea katika hali hiyo, kwa ghafla akaona mnyama mkubwa aliyezuia watu. Akasema: “Leo ndiyo nitajua kati ya mtawa na mchawi nani aliye bora.” Akachukua jiwe na akasema: “Ee Rabb, ikiwa jambo la yule Mtawa linapendeza Kwako kuliko jambo la yule mchawi, basi muuwe mnyama huyu ili watu waweze kupita.” Akamrushia (jiwe) na akamuua, watu wakapita. Akamuendea Mtawa na kumueleza habari ile. Yule Mtawa akamwambia: “Ee mwanangu leo hii wewe ni bora kulikoni mimi, jambo lako limefikia jinsi ninavyoliona, kwa yakini utapata mtihani; basi utakapopata mtihani, usimjulishe yoyote yule kwangu.” Yule kijana akaanza kuwaponya waliozaliwa vipofu, wenye ukoma na akiwatibu watu kila aina ya maradhi. Jalisi wa mfalme aliyekuwa amepofoka, akasikia habari hii. Akampelekea zawadi nyingi, akamwambia: “Mimi sina uwezo wa kumponya yoyote, hakika Anaeponya ni Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Ukimuamini Allaah nitamuomba Naye Atakuponya.” Akamuamini Allaah, Allaah Akamponya. Akaenda kwa mfalme na kukaa nae kama anavyokaa nae (kila siku). Mfalme akamuuliza: “Ni nani aliyekuponya macho yako?” Akajibu: “Ni Rabb wangu.” Akamuuliza: “Unae Rabb asiyekuwa mimi?” Akamjibu: “Rabb wangu na Rabb wako ni Allaah.” Akamchukua na akamuadhibu mpaka akamtaja yule kijana. Yule kijana akaletwa mbele ya mfalme, akamuuliza: “Ee kijana wangu, uchawi wako umefikia kiwango cha kuwaponya vipofu na wenye ukoma, na unafanya kadhaa na kadhaa?” Akamwambia: “Mimi sina uwezo wa kumponya yoyote yule, kwa yakini Anaeponya ni Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).” Akamchukua na kumuadhibu mpaka akamtaja yule Mtawa. Mtawa akaletwa, akaambiwa: “Acha dini yako.” Akakataa. Akaitisha msumeno akauweka utosini mwake, akampasua vipande viwili vikaanguka (akamgawanya pande mbili). Halafu akaletwa jalisi wa mfalme. Akaambiwa: “Acha dini yako.” Akakataa. Msumeno ukawekwa utosini mwake, akapasuliwa pande mbili zikaanguaka. Kisha akaletwa yule kijana. Akaambiwa: “Wacha dini yako.” Akakataa. Akamkabidhi kwa askari wake, akawaambia: “Nendeni naye katika jabali kadhaa wa kadhaa, mtakapofika katika kilele chake na akawa ameiwacha dini yake, basi muacheni, ikiwa hakuacha basi mtupeni chini.” Wakaenda nae na wakapanda nae juu ya jabali. Yule kijana akaomba: “Ee Rabb! Nitosheleze na shari yao namna Upendavyo.” Lile jabali likatikisika wakaanguka. Akarudi kwa mfalme huku akitembea. Mfalme akamuuliza: “Wamekuaje watu wako?” Akamwambia: Allaah Amenitosheleza.” Akamkabidhisha kwa kundi (lingine) la maaskari wake. Akawaambia: “Mpelekeni na mumpandishe jahazi ndogo hadi katikati ya bahari, akiwacha dini yake muacheni, akikataa basi mtoseni.” Wakaenda naye, akaomba: “Ee Rabb! Nitosheleze na shari yao namna Upendavyo.” Jahazi likapinduka wakazama. Akarudi kwa mfalme akitembea. Mfalme akamuuliza: “Wamekuaje watu wako?” Akamwambia: “Allaah Amenitosheleza.” Akamwambia mfalme: “Hakika huwezi kuniua mpaka ufanye nitakalokuamuru.” Akamuuliza: “Ni jambo gani hilo utakaloniamuru?” Akamwambia: “Wakusanye watu katika uwanja ulio wazi, halafu unisulubishe juu ya gogo, halafu uchukue mshale utakaokuwa katika ziaka yangu, kisha utauweka mshale katika upinde, halafu useme: “Kwa jina la Allaah, Rabb wa kijana huyu”. Kisha unirushie. Hakika ukifanya hivyo, utafanikiwa kuniua.” Yule mfalme akawakusanya watu katika uwanja mmoja, akamtundika juu ya gogo, halafu akachukua mshale kutoka katika ziaka yake, kisha akauweka mshale katikati ya upinde, halafu akasema: “Kwa jina la Allaah, Rabb wa kijana huyu,” kisha akamrushia ule mshale ukaingia katika panda lake uso, akauweka mkono wake katika panda lake na akafa. Watu wakasema: “Tumemuamini Rabb wa kijana huyu.” Mfalme akaendewa na kuambiwa: “Je, umeliona ulilokuwa ukilitahadhari? Wa-Allaahi limekuwa ulilolikataa, watu wamekuwa na iymaan.” Akaamuru kuchimbwe mahandaki barabarani, mioto ikawashwa humo. Akasema: “Ambae hatoacha dini yake mtupeni humo.” Au huambiwa: “Jitoseni wenyewe.” Wakafanya hivyo. Akaletwa mwanamke aliye na mtoto wake. Akasimama na akafanya uoga kuingia humo, yule mtoto wake akamwambia: “Ee mama yangu, subiri hakika wewe upo katika haki!” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 7

وعن أنس رضي الله عنه قَالَ: مَرَّ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم بامرأةٍ تَبكي عِنْدَ قَبْرٍ، فَقَالَ: ((اتّقِي الله واصْبِري)) فَقَالَتْ: إِليْكَ عَنِّي؛ فإِنَّكَ لم تُصَبْ بمُصِيبَتي وَلَمْ تَعرِفْهُ، فَقيلَ لَهَا: إنَّه النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم فَأَتَتْ بَابَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم، فَلَمْ تَجِدْ عِنْدَهُ بَوَّابينَ، فقالتْ: لَمْ أعْرِفكَ، فَقَالَ: ((إنَّمَا الصَّبْرُ عِنْدَ الصَّدْمَةِ الأُولى)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

وفي رواية لمسلم: ((تبكي عَلَى صَبيٍّ لَهَا)).

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipita akamuona mwanamke akilia mbele ya kaburi. Akamwambia: “Mche Allaah na usubiri.” Yule mwanamke akasema: “Niondokee, kwani hujapatwa na msiba kama wangu!” Wala hakumjua. Akaambiwa: Huyo alikuwa ni Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), akaenda hadi kwenye mlango wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na hakuwakuta walinzi, akamwambia: “Nilikuwa sijakujua kama ni wewe.” Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Hakika subira ni mwanzo wa kupatwa na msiba.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine ya Muslim imesema: “Alikuwa akimlilia mwanawe.”

 

 

Hadiyth – 8

 وعن أبي هريرة رضي الله عنه: أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((يَقُولُ اللهُ تَعَالَى: مَا لعَبدِي المُؤْمِنِ عِنْدِي جَزَاءٌ إِذَا قَبَضْتُ صَفِيَّهُ مِنْ أهْلِ الدُّنْيَا ثُمَّ احْتَسَبَهُ إلا الجَنَّةَ)). رواه البخاري

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema: “Mja wangu Muumin ni mwenye malipo nitakapomchukua mpenzi wake katika watu wa dunia kisha akataraji thawabu isipokuwa jazaa yake ni Jannah.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 9

وعن عائشةَ رضيَ الله عنها: أَنَّهَا سَألَتْ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم عَنِ الطّاعُونِ، فَأَخْبَرَهَا أنَّهُ كَانَ عَذَابًا يَبْعَثُهُ اللهُ تَعَالَى عَلَى مَنْ يشَاءُ، فَجَعَلَهُ اللهُ تعالى رَحْمَةً للْمُؤْمِنينَ، فَلَيْسَ مِنْ عَبْدٍ يَقَعُ في الطَّاعُونِ فيمكثُ في بلدِهِ صَابرًا مُحْتَسِبًا يَعْلَمُ أنَّهُ لا يصيبُهُ إلا مَا كَتَبَ اللهُ لَهُ إلا كَانَ لَهُ مِثْلُ أجْرِ الشّهيدِ. رواه البخاري

‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) alimuuliza Rasuli  wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu twaa’uwn (ugonjwa wa tauni), akamwambia kuwa: “Ilikuwa ni adhabu ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akimpelekea Anayemtaka; Allaah Akaijaalia kuwa ni rahmah kwa Waumini. Hakuna mja yoyote yule atakaepata twaa’uwn akakaa katika mji ule kwa kusubiri na kutaraji thawabu akijua kuwa hakuna kitakachompata ila alichoandikiwa na Allaah, isipokuwa na ujira mfano wa (aliyekufa) shaahid.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 10

وعن أنس رضي الله عنه قَالَ: سمعتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((إنَّ الله- عز وجل، قَالَ: إِذَا ابْتَلَيْتُ عبدي بحَبيبتَيه فَصَبرَ عَوَّضتُهُ مِنْهُمَا الجَنَّةَ)) يريد عينيه، رواه البخاري

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Hakika Allaah (‘Azza wa Jalla) Amesema: “Nitakapomjaribu mja Wangu kwa kukosa vipenzi vyake (macho mawili) na akasubiri, Nitambadilishia Jannah badala yake.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 11

 وعن عطَاء بن أبي رَباحٍ قَالَ: قَالَ لي ابنُ عَباسٍ رضي اللهُ عنهما: ألا أُريكَ امْرَأةً مِنْ أَهْلِ الجَنَّة؟ فَقُلْتُ: بَلَى، قَالَ: هذِهِ المَرْأةُ السَّوداءُ أتتِ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم، فَقَالَتْ: إنّي أُصْرَعُ، وإِنِّي أتَكَشَّفُ، فادْعُ الله تَعَالَى لي. قَالَ: ((إنْ شئْتِ صَبَرتِ وَلَكِ الجَنَّةُ، وَإنْ شئْتِ دَعَوتُ الله تَعَالَى أنْ يُعَافِيكِ)) فَقَالَتْ: أَصْبِرُ، فَقَالَتْ: إنِّي أتَكَشَّفُ فَادعُ الله أنْ لا أَتَكَشَّف، فَدَعَا لَهَا. مُتَّفَقٌ عَلَيه

‘Atwaa bin Abiy Rabaah amesema: “’Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) aliniambia: Je, nikuonyeshe mwanamke ambae ni katika watu wa Jannah?” Nikwambia: “Ni mwanamke huyu mweusi, alimuendea Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kamwambia: “Mimi nina kifafa na huwa nafichulika wazi (sehemu za siri kinaponijia), niombee kwa Allaah.” Akamwambia: “Ukitaka subiri na ukitaka nitamuomba Allaah Akuponye.” Akasema: “Nitasubiri lakini mimi nafichulika wazi basi niombee kwa Allaah nisifichulike wazi (nisitirike nguo isinifunuke).” Akamuombea. [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyh -12

 

وعن أبي عبد الرحمنِ عبدِ الله بنِ مسعودٍ رضي الله عنه قَالَ: كَأَنِّي أنْظُرُ إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم يَحْكِي نَبِيًّا مِنَ الأَنْبِياءِ، صَلَواتُ الله وَسَلامُهُ عَلَيْهمْ، ضَرَبه قَوْمُهُ فَأدْمَوهُ، وَهُوَ يَمْسَحُ الدَّمَ عَنْ وَجْهِهِ، يَقُولُ: ((اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِقَومي، فَإِنَّهُمْ لا يَعْلَمونَ)). مُتَّفَقٌ علَيه

Abuu ‘Abdir-Rahmaan, ‘Abdulaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Kana kwamba namuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akieleza kuhusu Nabiy fulani, (‘Alayhimus-Salaam). Watu wake walimpinga na kumtoa damu usoni mwake, akiomba: “Ee Rabb! Waghufurie kaumu yangu, kwani wao hawajui!” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 13

 

وعن أبي سعيدٍ وأبي هريرةَ رضيَ الله عنهما، عن النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((مَا يُصيبُ المُسْلِمَ مِنْ نَصَبٍ، وَلا وَصَبٍ، وَلا هَمٍّ، وَلا حَزَنٍ، وَلا أذَىً، وَلا غَمٍّ، حَتَّى الشَّوكَةُ يُشَاكُهَا إلا كَفَّرَ اللهُ بِهَا مِنْ خَطَاياهُ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Abuu Sa’iyd na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) wamepokea kutoka kwa Nabiy  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa amesema: “Muislaam hatopatwa na tabu, wala maradhi, wala hamu, wala huzuni, wala udhia, wala ghamu (sononeko) hata akichomwa na mwiba, isipokuwa Allaah Humfutia madhambi yake kwa sababu ya (matatizo) hayo.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 14

وعن ابنِ مسعودٍ رضي الله عنه قَالَ: دخلتُ عَلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم وهو يُوعَكُ، فقلت: يَا رسُولَ الله، إنَّكَ تُوْعَكُ وَعْكًا شَدِيدًا، قَالَ: ((أجَلْ، إنِّي أوعَكُ كمَا يُوعَكُ رَجُلانِ مِنكُمْ)). قلْتُ: ذلِكَ أن لَكَ أجْرينِ؟ قَالَ: ((أَجَلْ، ذلِكَ كَذلِكَ، مَا مِنْ مُسْلِمٍ يُصيبُهُ أذىً، شَوْكَةٌ فَمَا فَوقَهَا إلا كَفَّرَ اللهُ بهَا سَيِّئَاتِهِ، وَحُطَّتْ عَنْهُ ذُنُوبُهُ كَمَا تَحُطُّ الشَّجَرَةُ وَرَقَهَا)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Nilimuendea Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye akiwa na homa. Nikamwambia: Yaa Rasula-Allaah, hakika huwa ukishikwa na homa basi huwa kali mno.” Akasema: “Ndiyo, hakika mimi hushikwa na homa kama vile watu wawili wanavyoshikwa na homa kati yenu.” Nikamuuliza: “Ni kwa vile una ujira mara mbili?” Akasema: “Ndiyo, ni hivyo. Hakuna Muislaamu yoyote anasibiwa na udhia kuanzia mwiba na kuendelea, isipokuwa Allaah humsamehe mabaya yake kwa udhia huo, na dhambi zake hupuputishwa kama vile mti unavyopuputika majani yake.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 15

 وعن أبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ يُرِدِ اللهُ بِهِ خَيْرًا يُصِبْ مِنْهُ)). رواه البخاري

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Anayependelewa khayr na Allaah Humpa msiba.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 16

وعن أنس رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((لا يَتَمَنَّيَنَّ أَحَدُكُمُ المَوتَ لضُرٍّ أَصَابَهُ، فَإِنْ كَانَ لابُدَّ فاعلًا، فَليَقُلْ: اللَّهُمَّ أحْيني مَا كَانَتِ الحَيَاةُ خَيرًا لِي، وَتَوفّنِي إِذَا كَانَتِ الوَفَاةُ خَيرًا لي)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Asitamani mauti mmoja wenu kwa sababu ya madhara yaliyompata, akiwa hana budi ila atamani, basi aombe: Ee Rabb, Nihuishe madamu kuishi kuna khayr kwangu, na Unifishe iwapo kufa kuna khayr kwangu.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 17

وعن أبي عبد الله خَبَّاب بنِ الأَرتِّ رضي الله عنه قَالَ: شَكَوْنَا إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم وَهُوَ متَوَسِّدٌ بُرْدَةً لَهُ في ظلِّ الكَعْبَةِ، فقُلْنَا: أَلا تَسْتَنْصِرُ لَنَا ألا تَدْعُو لَنا؟ فَقَالَ: ((قَدْ كَانَ مَنْ قَبْلَكُمْ يُؤْخَذُ الرَّجُلُ فَيُحْفَرُ لَهُ في الأرضِ فَيُجْعَلُ فِيهَا، ثُمَّ يُؤْتَى بِالمِنْشَارِ فَيُوضَعُ عَلَى رَأسِهِ فَيُجْعَلُ نصفَينِ، وَيُمْشَطُ بأمْشَاطِ الحَديدِ مَا دُونَ لَحْمِه وَعَظْمِهِ، مَا يَصُدُّهُ ذلِكَ عَنْ دِينِهِ، وَاللهِ لَيُتِمَّنَّ الله هَذَا الأَمْر حَتَّى يَسيرَ الرَّاكبُ مِنْ صَنْعَاءَ إِلَى حَضْرَموتَ لا يَخَافُ إلا اللهَ والذِّئْب عَلَى غَنَمِهِ، ولكنكم تَسْتَعجِلُونَ)). رواه البخاري.

وفي رواية: ((وَهُوَ مُتَوَسِّدٌ بُرْدَةً وَقَدْ لَقِينا مِنَ المُشْرِكِينَ شدَّةً))

Abuu ‘Abdillaah, Khabbaab bin Al-Arrat (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Tulimlalamika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye alikuwa ameegemea shuka yake katika kivuli cha Al-Qa’bah. Tukamwambia: “Hutuombei nusra, hutuombei du’ah?” Akatuambia: “Walikuwa waliopita kabla yenu, mtu alikuwa akifukuliwa ardhi na akitiwa humo, halafu ukiletwa msumeno ukiwekwa juu ya kichwa chake, akigawanywa pande mbili, na (mwengine) akichanwa kwa chanuo la chuma akitolewa nyama na mifupa, jambo hilo haliwi kipingamizi katika dini yake. Wa-Allaahi, Allaah Atalikamilisha jambo hili hata msafiri atembee kutoka Sanaa hadi Hadhwramawt hana anachoogopa isipokuwa Allaah, na kumkhofia mbwa mwitu asije akala mbuzi wake; lakini ninyi mnaharaka. [Al-Bukhaariy]

Riwaayah nyingine imesema: “Nae alikuwa ameegemea shuka yake. Kwa hakika tulipata mateso makubwa kutoka kwa mushirikiynah.”

 

 

Hadiyth – 18

وعن ابن مسعودٍ رضي الله عنه قَالَ: لَمَّا كَانَ يَومُ حُنَينٍ آثَرَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم نَاسًا في القسْمَةِ، فَأعْطَى الأقْرَعَ بْنَ حَابسٍ مائَةً مِنَ الإِبِلِ، وَأَعْطَى عُيَيْنَة بْنَ حصن مِثْلَ ذلِكَ، وَأَعطَى نَاسًا مِنْ أشْرافِ العَرَبِ وآثَرَهُمْ يَوْمَئِذٍ في القسْمَةِ. فَقَالَ رَجُلٌ: واللهِ إنَّ هذِهِ قِسْمَةٌ مَا عُدِلَ فِيهَا، وَمَا أُريدَ فيهَا وَجْهُ اللهِ، فَقُلْتُ: وَاللهِ لأُخْبِرَنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم، فَأَتَيْتُهُ فَأخْبَرتُهُ بمَا قَالَ، فَتَغَيَّرَ وَجْهُهُ حَتَّى كَانَ كالصِّرْفِ. ثُمَّ قَالَ: ((فَمَنْ يَعْدِلُ إِذَا لم يَعْدِلِ اللهُ وَرسولُهُ؟)) ثُمَّ قَالَ: ((يَرْحَمُ اللهُ مُوسَى قَدْ أُوذِيَ بأكْثَرَ مِنْ هَذَا فَصَبر)). فَقُلْتُ: لا جَرَمَ لا أرْفَعُ إِلَيْه بَعدَهَا حَدِيثًا. مُتَّفَقٌ عَلَيه

‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Siku ya vita vya Hunayn, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwafadhilisha baadhi ya watu katika mgao; akampa Al-Aqra’ bin Haabis ngamia mia moja, akampa Uyaynah bin Hiswn mfano wake, na akawapa watu watukufu wa Kiarabu na akawafadhilisha katika mgao siku hiyo. Mtu mmoja akasema: “Wa-Allaahi huu ni mgao usio na uadilifu! Wala haujakusudiwa radhi ya Allaah!” Nikasema: “Wa-Allaahi nitamueleza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam); nikaenda na kumueleza aliyosema. Uso wake Rasuli  wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ukabadilika hata ukawa mwekundu. Kisha akasema: “Ni nani atakaefanya uadilifu ikiwa Allaah na Rasuli wake Hawakufanya uadilifu?” Halafu akasema: “Allaah Amraham Muwsa, hakika aliudhiwa zaidi ya hivi na akasubiri!” Nikasema: “Kwa hakika sitomueleza tena (mazungumzo kama haya ya kumuudhi).” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyh – 19

وعن أنسٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((إِذَا أَرَادَ الله بعبدِهِ الخَيرَ عَجَّلَ لَهُ العُقُوبَةَ في الدُّنْيا، وَإِذَا أَرَادَ اللهُ بِعَبدِهِ الشَّرَّ أمْسَكَ عَنْهُ بذَنْبِهِ حَتَّى يُوَافِيَ بِهِ يومَ القِيَامَةِ)).

وَقالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم: ((إنَّ عِظَمَ الجَزَاءِ مَعَ عِظَمِ البَلاَءِ، وَإنَّ اللهَ تَعَالَى إِذَا أَحَبَّ قَوْمًا ابْتَلاَهُمْ، فَمَنْ رَضِيَ فَلَهُ الرِّضَا، وَمَنْ سَخِطَ فَلَهُ السُّخْطُ)). رواه الترمذي، وَقالَ: ((حديث حسن))

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Anapompendea khayr mja Wake, Humuharakishia adhabu duniani. Na anapomtakia shari mja Wake, Huzuia dhambi zake ili Amlipe siku ya Qiyaamah.” 

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Malipo makubwa yapo pamoja na mitihani kubwa. Hakika Allaah Anapowapenda watu, Huwapa mitihani; atakayeridhika, basi atapata Radhi (za Allaah), na atakayechukia, atapata Hasira (za Allaah).” [At-Tirmidhiy, na amesema hadiyth hii ni Hassan]

 

 

Hadiyth – 20

وعن أنسٍ رضي الله عنه قَالَ: كَانَ ابنٌ لأبي طَلْحَةَ رضي الله عنه يَشتَكِي، فَخَرَجَ أبُو طَلْحَةَ، فَقُبِضَ الصَّبيُّ، فَلَمَّا رَجَعَ أَبُو طَلْحَةَ، قَالَ: مَا فَعَلَ ابْنِي؟ قَالَتْ أمُّ سُلَيم وَهِيَ أمُّ الصَّبيِّ: هُوَ أَسْكَنُ مَا كَانَ، فَقَرَّبَتْ إليه العَشَاءَ فَتَعَشَّى، ثُمَّ أَصَابَ منْهَا، فَلَمَّا فَرَغَ، قَالَتْ: وَارُوا الصَّبيَّ فَلَمَّا أَصْبحَ أَبُو طَلْحَةَ أَتَى رسولَ الله صلى الله عليه وسلم فَأخْبَرَهُ، فَقَالَ: ((أعَرَّسْتُمُ اللَّيلَةَ؟)) قَالَ: نَعَمْ، قَالَ: ((اللَّهُمَّ بَارِكْ لَهُمَا))، فَوَلَدَتْ غُلامًا، فَقَالَ لي أَبُو طَلْحَةَ: احْمِلْهُ حَتَّى تَأْتِيَ بِهِ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم، وَبَعَثَ مَعَهُ بِتَمَراتٍ، فَقَالَ: ((أَمَعَهُ شَيءٌ؟)) قَالَ: نَعَمْ، تَمَراتٌ، فَأخَذَهَا النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم فَمَضَغَهَا، ثُمَّ أَخَذَهَا مِنْ فِيهِ فَجَعَلَهَا في فِيِّ الصَّبيِّ، ثُمَّ حَنَّكَهُ وَسَمَّاهُ عَبدَ الله. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

وفي رواية للبُخَارِيِّ: قَالَ ابنُ عُيَيْنَةَ: فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ الأَنْصارِ: فَرَأيْتُ تِسعَةَ أوْلادٍ كُلُّهُمْ قَدْ قَرَؤُوا القُرْآنَ، يَعْنِي: مِنْ أوْلادِ عَبدِ الله المَولُودِ.

وَفي رواية لمسلمٍ: مَاتَ ابنٌ لأبي طَلْحَةَ مِنْ أمِّ سُلَيمٍ، فَقَالَتْ لأَهْلِهَا: لا تُحَدِّثُوا أَبَا طَلْحَةَ بابْنِهِ حَتَّى أَكُونَ أَنَا أُحَدِّثُهُ، فَجَاءَ فَقَرَّبَتْ إِلَيْه عَشَاءً فَأَكَلَ وَشَرِبَ، ثُمَّ تَصَنَّعَتْ لَهُ أَحْسَنَ مَا كَانَتْ تَصَنَّعُ قَبْلَ ذلِكَ، فَوَقَعَ بِهَا. فَلَمَّا أَنْ رَأَتْ أَنَّهُ قَدْ شَبِعَ وأَصَابَ مِنْهَا، قَالَتْ: يَا أَبَا طَلْحَةَ، أَرَأَيتَ لو أنَّ قَومًا أعارُوا عَارِيَتَهُمْ أَهْلَ بَيتٍ فَطَلَبُوا عَارِيَتَهُمْ، أَلَهُمْ أن يَمْنَعُوهُمْ؟ قَالَ: لا، فَقَالَتْ: فَاحْتَسِبْ ابْنَكَ، قَالَ: فَغَضِبَ، ثُمَّ قَالَ: تَرَكْتِني حَتَّى إِذَا تَلطَّخْتُ، ثُمَّ أخْبَرتني بِابْنِي؟! فانْطَلَقَ حَتَّى أَتَى رسولَ الله صلى الله عليه وسلم فَأخْبَرَهُ بِمَا كَانَ فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((بَارَكَ اللهُ في لَيْلَتِكُمَا))، قَالَ: فَحَمَلَتْ. قَالَ: وَكانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم في سَفَرٍ وَهيَ مَعَهُ، وَكَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم إِذَا أَتَى المَدِينَةَ مِنْ سَفَرٍ لا يَطْرُقُهَا طُرُوقًا فَدَنَوا مِنَ المَدِينَة، فَضَرَبَهَا المَخَاضُ، فَاحْتَبَسَ عَلَيْهَا أَبُو طَلْحَةَ، وانْطَلَقَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم. قَالَ: يَقُولَ أَبُو طَلْحَةَ: إنَّكَ لَتَعْلَمُ يَا رَبِّ أَنَّهُ يُعْجِبُنِي أنْ أخْرُجَ مَعَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم إِذَا خَرَجَ وَأَدْخُلَ مَعَهُ إِذَا دَخَلَ وَقَدِ احْتَبَسْتُ بِمَا تَرَى، تَقُولُ أُمُّ سُلَيْمٍ: يَا أَبَا طَلْحَةَ، مَا أَجِدُ الَّذِي كُنْتُ أجدُ انْطَلِقْ، فَانْطَلَقْنَا وَضَرَبَهَا المَخَاضُ حِينَ قَدِمَا فَوَلدَت غُلامًا. فَقَالَتْ لِي أمِّي: يَا أنَسُ، لا يُرْضِعْهُ أحَدٌ حَتَّى تَغْدُو بِهِ عَلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَلَمَّا أصْبَحَ احْتَمَلْتُهُ فَانْطَلَقْتُ بِهِ إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم. وَذَكَرَ تَمَامَ الحَدِيثِ.

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Alikuwa mtoto wa Abuu Twalhah akiugua. Abuu Twalahah akapata safari na kusafiri. Yule mtoto akafariki. Abuu Twalhah aliporudi”, aliuliza: “Vipi hali ya mwanangu?” Ummu Sulaym (mama wa mtoto) akamwambia: “Ametulia zaidi ya alivyokuwa.” Akampelekea chakula cha jioni akala, kisha akalala na mkewe (akamjamii). Alipomaliza, Ummu Sulaym akamwambi: “Kamzikeni mtoto.” Abuu Twalhah alipopambaukiwa, alikwenda moja kwa moja mpaka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamueleza yaliyotokea. Akamuuliza: “Usiku mlifanya tendo la ndoa?” Akajibu: “Ndiyo” Akaomba: “Ee Rabb, Wabarikie.” Akazaa mvulana. Abuu Twalhah akaniambia: “Mbebe na umepeleke kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akapeleka na tende kadhaa. Akauliza: “Ana kitu?” Akajibu: “Ndiyo, tende kadhaa.” Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akazichua na kuzitafuna, kisha akachukua zile tende zilizokuwa kinywani mwake akazitia kwenye kinywa cha mtoto, halafu akamsugua na kumpa jina la ’Abdullaah”. [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine ya Al-Bukhaariy imesema: “Ibnu Uyaynah amesema: “Mtu mmoja katika Answaariy akasema: “Nikawaona watoto tisa, wote wamehifadhi Qur-aan.” Yaani watoto wa ‘Abdullaah huyu aliezaliwa.

Riwaayah nyingine ya Muslim imesema: “Abuu Twalhah alifiwa na mtoto aliyezaa naye kwa Ummu Sulaym akawaambia jamaa zake: “Msimueleze Abuu Twalhah habari ya mwanawe mpaka mimi niwe ndiye nitakaemueleza.” Akaja, akampelekea chakula jioni, akala na akanywa, halafu akajipamba kulikoni alivyojipamba siku zote. Akamjamii. Ummu Sulaym alipoona kuwa Abuu Twalhah ameshiba na amemjamii, alimwambia: “Ee Abuu Twalhah niambie lau watu wameazima kitu kwa watu fulani kisha hao watu wakataka kitu cha kilichoazimwa, je, wao wanahaki ya kuwanyima?” Akajibu: “Hapana.” Akamwambia: Basi taraji thawabu kwa msiba wa mwanao.” Abuu Twalhah akakasirika, na akasema: “Umeniwacha mpaka nimejichafua (kwa tendo la ndoa) halafu unaniambia habari ya mwanangu?” Akaenda kwa Rasuli  wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamueleza mambo yalivyokuwa. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaombea “Allaah Awabarikie katika usiku wenu.” Ummu Sulaym akabeba ujauzito. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa safarini pamoja na Ummu Sulaym. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapowasili Madiynah akitoka safari, alikuwa haingii usiku. Walipowasili Madiynah Ummu Sulaym alianza kuhisi uchungu wa uzazi, Abuu Twalhah alibaki nyuma, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaendelea na safari. Abuu Twalhah akasema: “Ee Rabb, hakika Unajua ya kuwa mimi hufurahishwa kusafiri pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anaposafiri, na hupenda kurudi pamoja nae anaporudi, na nimezuilika kama Uonavyo.” Ummu Sulaym akasema: “Ee Abuu Twalhah sisikii uchungu tena niliousikia, tuondoke.” Tukaondoka. Akapatwa na uchungu tena wa kuzaa tulipokuwa tumeshawasili Madiynah, akajifungua mtoto wa kiume. Mama yangu akaniambia: “Ee Anas, mtoto huyu asinyonyeshwe na yoyote mpaka uende nae kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).” Kulipopambauka, nilimbeba na kwenda nae kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ...” Akaendelea mpaka mwisho wa Hadiyth.

 

 

Hadiyth – 21

وعن أبي هريرةَ رضي الله عنه أنّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((لَيْسَ الشَّدِيدُ بالصُّرَعَةِ، إنَّمَا الشَدِيدُ الَّذِي يَملكُ نَفْسَهُ عِنْدَ الغَضَبِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwenye nguvu si yule awashindae watu kwa miereka, bali mwenye nguvu ni yule anayemiliki nafsi yake wakati wa hasira.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 22

وعن سُلَيْمَانَ بن صُرَدٍ رضي الله عنه قَالَ: كُنْتُ جالِسًا مَعَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، وَرَجُلانِ يَسْتَبَّانِ، وَأَحَدُهُمَا قدِ احْمَرَّ وَجْهُهُ، وانْتَفَخَتْ أوْدَاجُهُ، فَقَالَ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم: ((إنِّي لأَعْلَمُ كَلِمَةً لَوْ قَالَهَا لَذَهَبَ عَنْهُ مَا يَجِدُ، لَوْ قَالَ: أعُوذ باللهِ منَ الشَّيطَانِ الرَّجِيمِ، ذَهَبَ عنْهُ مَا يَجِدُ)). فَقَالُوا لَهُ: إنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((تَعَوّذْ باللهِ مِنَ الشَّيطَانِ الرَّجِيمِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Sulaymaan bin Swurad (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Nilikuwa nimekaa pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na watu wanatukanana, mmoja kati yao uso wake ulikuwa umeiva na mishipa yake ya shingoni imevimba. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Mimi nalijua neno, lau utalisema basi utaondokewa na hasira:

 

أعُوذ باللهِ منَ الشَّيطَانِ الرَّجِيمِ

“Aa’uwdhu biLLaahi mina shaytwaani rajiym (najilinda kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyelaaniwa), ataondokewa na hasira.” Wakaenda wakamwambia kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekwambia ujikinge kwa Allaah kutokana na shaytwaan aliyelaaniwa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 23

وعن معاذِ بنِ أَنسٍ رضي الله عنه أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((مَنْ كَظَمَ غَيظًا، وَهُوَ قَادِرٌ عَلَى أنْ يُنْفِذَهُ، دَعَاهُ اللهُ سُبحَانَهُ وَتَعَالى عَلَى رُؤُوسِ الخَلائِقِ يَومَ القِيامَةِ حَتَّى يُخَيِّرَهُ مِنَ الحُورِ العِينِ مَا شَاءَ)). رواه أَبو داود والترمذي، وَقالَ: (حديث حسن)

Mu’aadh bin Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema kuwa: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakaezuia hasira na akawa anaweza kuitekeleza, Allaah Atamuita siku ya Qiyaamah mbele ya halaiki ili Amchagulishe Huwrul ‘ayn anayemtaka.” [Abuu Daawud na At-Tirmidhiy, na amesema hadiyth hii ni Hasan]

 

 

Hadiyth – 24

وعن أبي هريرةَ رضي الله عنه: أنَّ رَجُلًا قَالَ للنبي صلى الله عليه وسلم: أوصِني. قَالَ: ((لا تَغْضَبْ)) فَرَدَّدَ مِرارًا، قَالَ: ((لاَ تَغْضَبْ)). رواه البخاري

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema kuwa: “Mtu mmoja alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Niusie.” Akamwambia: “Usighadhibike.” Akarudia ombi lake mara nyingi, (Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Usighadhibike.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 25

وعن أبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَا يَزَالُ البَلاَءُ بالمُؤمِنِ وَالمُؤْمِنَةِ في نفسِهِ ووَلَدِهِ وَمَالِهِ حَتَّى يَلْقَى الله تَعَالَى وَمَا عَلَيهِ خَطِيئَةٌ)). رواه الترمذي، وَقالَ: (حديث حسن صحيح)

Abuu Hurayrah (Rahwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli  wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) “Muumin hatowacha kupatwa na balaa katika nafsi yake, watoto wake na mali yake mpaka akutane na Allaah ilihali hana dhambi.” [At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 26

وعن ابْنِ عباسٍ رضي الله عنهما قَالَ: قَدِمَ عُيَيْنَةُ بْنُ حِصْنٍ، فَنَزَلَ عَلَى ابْنِ أخِيهِ الحُرِّ بنِ قَيسٍ، وَكَانَ مِنَ النَّفَرِ الَّذِينَ يُدْنِيهِمْ عُمرُ رضي الله عنه، وَكَانَ القُرَّاءُ أصْحَابَ مَجْلِس عُمَرَ رضي الله عنه وَمُشاوَرَتِهِ كُهُولًا كانُوا أَوْ شُبَّانًا، فَقَالَ عُيَيْنَةُ لابْنِ أخيهِ: يَا ابْنَ أخِي، لَكَ وَجْهٌ عِنْدَ هَذَا الأمِيرِ فَاسْتَأذِنْ لِي عَلَيهِ، فاسْتَأذَن فَأذِنَ لَهُ عُمَرُ. فَلَمَّا دَخَلَ قَالَ: هِي يَا ابنَ الخَطَّابِ، فَواللهِ مَا تُعْطِينَا الْجَزْلَ وَلا تَحْكُمُ فِينَا بالعَدْلِ. فَغَضِبَ عُمَرُ رضي الله عنه حَتَّى هَمَّ أنْ يُوقِعَ بِهِ. فَقَالَ لَهُ الحُرُّ: يَا أميرَ المُؤْمِنينَ، إنَّ الله تَعَالَى قَالَ لِنَبيِّهِ صلى الله عليه وسلم: {خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ} [الأعراف: 199] وَإنَّ هَذَا مِنَ الجَاهِلِينَ، واللهِ مَا جَاوَزَهاَ عُمَرُ حِينَ تَلاَهَا، وكَانَ وَقَّافًا عِنْدَ كِتَابِ اللهِ تَعَالَى. رواه البخاري

‘Abdullaah ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: “’Uyaynah bin Hiswn alikuja kutoka safari, akashukia kwa mtoto wa dada yake Al-Hurri bin Qays, naye alikuwa ni katika watu ambao ‘Umar alikuwa akiwakurubisha karibu naye, wanavyuoni walikuwa ndio wa majilisi ya ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na katika ushauri wake; wawe ni wazee au vijana. ‘Uyaynah akamwambia mtoto wa dada yake: “Ee mtoto wa dada yangu, wewe una nafasi kwa huyu Amiyr, basi niombee idhini (niingie kwake).” Akamuombea idhini, ‘Umar akamruhusu. Alipoingia alisema: “Hii! Ee mwana wa Khattwaab! Wa-Allaahi hutupatii vitu vingi, wala huhukumu kwa audilifu kati yetu.” ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akakasirika hata akataka kumuadhibu. Al-Hurru akamwambia: “Ee Amiyr wa Waumini, hakika Allaah Alimwambia Nabiy Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)

خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ

“Shikamana na usamehevu, na amrisha mema na jiepushe na majahili” [Al-A’raaf: 199]

Hakika huyu ni katika majahili. Basi wa-Allaahi ‘Umar hakumfanya kitu Al-Hurru alipoisoma Aayah hii. Alikuwa ‘Umar amesimama wima katika kitabu cha Allaah.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 26

وعن ابن مسعود رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إنَّهَا سَتَكونُ بَعْدِي أثَرَةٌ وأُمُورٌ تُنْكِرُونَها!)) قَالُوا: يَا رَسُول الله، فَمَّا تَأْمُرُنا؟ قَالَ: ((تُؤَدُّونَ الْحَقَّ الَّذِي عَلَيْكُمْ، وَتَسأَلُونَ الله الَّذِي لَكُمْ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

 ‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika baada yangu kutakuwepo ubinafsi na mambo ambayo hamtokubaliyana nayo.” Maswahaba wakauliza: “Yaa Rasula-Allaah, kwahiyo unatuamrisha tufanye nini?” Akawaambia: “Mutaitekeleza haki inayowapasa, na mumuombe Allaah ambacho ni chenu.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 27

  وعن أبي يحيى أُسَيْد بن حُضَير رضي الله عنه: أنَّ رَجُلًا مِنَ الأنْصارِ قَالَ: يَا رسولَ الله، ألا تَسْتَعْمِلُني كَمَا اسْتَعْمَلْتَ فُلانًا؟ فَقَالَ: ((إنكُمْ سَتَلْقَونَ بَعْدِي أَثَرَةً فَاصْبِرُوا حَتَّى تَلْقَوني عَلَى الحَوْضِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Abuu Yahyaa, Usayd bin Hudhwayr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Mtu mmoja katika Answaari alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Yaa Rasula-Allaah, mbona hunifanyi kuwa hakimu kama ulivyomfanya fulani?” Akamwambia: “Hakika baada yangu mtaona ubinasfi, basi subirini mpaka mkutane nami katika hodhi.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 28

 وعن أبي إبراهيم عبدِ الله بن أبي أوفى رضي الله عنهما: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم في بعْضِ أيامِهِ التي لَقِيَ فِيهَا العَدُوَّ، انْتَظَرَ حَتَّى إِذَا مالَتِ الشَّمْسُ قَامَ فيهمْ، فَقَالَ: ((يَا أيُّهَا النَّاسُ، لا تَتَمَنَّوا لِقَاءَ العَدُوِّ، وَاسْأَلُوا الله العَافِيَةَ، فَإِذَا لقيتُمُوهُمْ فَاصْبرُوا، وَاعْلَمُوا أنّ الجَنَّةَ تَحْتَ ظِلالِ السُّيوفِ)). ثُمَّ قَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم: ((اللَّهُمَّ مُنْزِلَ الكِتَابِ، وَمُجْرِيَ السَّحَابِ، وَهَازِمَ الأحْزَابِ، اهْزِمْهُمْ وَانصُرْنَا عَلَيْهمْ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Abuu Ibraahiym ‘Abdillaah bin Abiy Awfa (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika baadhi ya siku alizokutana na adui, alingoja hadi jua lilipopinduka, akasimama na akawaeleza: “Enyi watu, msitamani kukutana na adui, muombeni Allaah al-‘afiyah (salama), na mtakapo kutana nao, subirini, na fahamuni kuwa Jannah ipo chini ya vivuli vya panga.” Halafu Nabiy  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaomba: “Ee Rabb Mteremsha Kitabu, Mwenye kuendesha mawingu, Mwenye kuyashinda makundi, Washinde na Utunusuru.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share