007-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Yakini Na Kutawakali Kwa Allaah

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب في اليقين والتوكل

007 - Mlango Wa Yakini Na Kutawakali Kwa Allaah

 

قَالَ اللهُ تَعَالَى:

وَلَمَّا رَأَى الْمُؤْمِنُونَ الْأَحْزَابَ قَالُوا هَـٰذَا مَا وَعَدَنَا اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَصَدَقَ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ ۚ وَمَا زَادَهُمْ إِلَّا إِيمَانًا وَتَسْلِيمًا ﴿٢٢﴾

Basi Waumini walipoona makundi, walisema: “Haya ndio yale Aliyotuahidi Allaah na Rasuli Wake, na Amesema kweli Allaah na Rasuli Wake; na haikuwazidishia isipokuwa iymaan na kujisalimisha. [Al-Ahzaab: 22]

 

 

الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّـهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ﴿١٧٣﴾

Wale walioambiwa na watu: “Hakika watu wamejumuika dhidi yenu, basi waogopeni” (Haya) Yakawazidishia iymaan; na wakasema: “Allaah Anatutosheleza, Mzuri Alioje Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.”

  

فَانقَلَبُوا بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ لَّمْ يَمْسَسْهُمْ سُوءٌ وَاتَّبَعُوا رِضْوَانَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ ذُو فَضْلٍ عَظِيمٍ ﴿١٧٤﴾

Basi wakarudi na neema kutoka kwa Allaah na fadhila; halijawagusa ovu lolote; na wakafuatilia radhi za Allaah.  Na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu.  [Aal-‘Imraan: 173-174]

 

قَالَتْ لَهُمْ رُسُلُهُمْ إِن نَّحْنُ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَمُنُّ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ وَمَا كَانَ لَنَا أَن نَّأْتِيَكُم بِسُلْطَانٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١١﴾

Rasuli wao wakawajibu: “Sisi si chochote isipokuwa ni watu kama nyinyi, lakini Allaah Anamfadhilisha Amtakaye miongoni mwa waja Wake. Na haikutupasa sisi kukujieni kwa ushahidi isipokuwa kwa idhini ya Allaah. Na kwa Allaah watawakali Waumini.  [Ibraahiym: 11]

 

فَبِمَا رَحْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ لِنتَ لَهُمْ ۖ وَلَوْ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ الْقَلْبِ لَانفَضُّوا مِنْ حَوْلِكَ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَوكِّلِينَ ﴿١٥٩﴾

Basi ni kwa rahmah kutoka kwa Allaah umekuwa mpole kwao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).  Na lau ungelikuwa mjeuri mwenye moyo mgumu wangelitawanyika mbali nawe (wakakukimbia). Basi wasamehe na waombee maghfirah na washauri katika mambo. Na unapoazimia basi tawakali kwa Allaah. Hakika Allaah Anapenda wanaotawakali. [Aal-‘Imraan:159]

 

وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ ۚ وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ فَهُوَ حَسْبُهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بَالِغُ أَمْرِهِ ۚ قَدْ جَعَلَ اللَّـهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا﴿٣﴾

Na Atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii. Na yeyote anayetawakali kwa Allaah, basi Yeye Humtosheleza. Hakika Allaah Anatimiza kusudio Lake. Allaah Amejaalia kwa kila kitu makadirio.  [Atw-Twalaaq: 3]

 

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ﴿٢﴾

Hakika Waumini ni wale ambao anapotajwa Allaah nyoyo zao, zinajaa khofu na wanaposomewa Aayaat Zake huwazidishia iymaan, na kwa Rabb wao wanatawakali. [Al-Anfaal: 2]

 

Hadiyth – 1

عن ابن عباس رضي الله عنهما، قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((عُرِضَتْ عَلَيَّ الأُمَمُ، فَرَأيْتُ النَّبيّ ومَعَهُ الرُّهَيطُ، والنبي وَمَعَهُ الرَّجُلُ وَالرَّجُلانِ، والنبيَّ ولَيْسَ مَعَهُ أَحَدٌ إِذْ رُفِعَ لي سَوَادٌ عَظيمٌ فَظَنَنْتُ أَنَّهُمْ أُمَّتِي فقيلَ لِي: هَذَا مُوسَى وَقَومُهُ، ولكنِ انْظُرْ إِلَى الأُفُقِ، فَنَظَرتُ فَإِذا سَوادٌ عَظِيمٌ، فقيلَ لي: انْظُرْ إِلَى الأفُقِ الآخَرِ، فَإِذَا سَوَادٌ عَظيمٌ، فقيلَ لِي: هذِهِ أُمَّتُكَ وَمَعَهُمْ سَبْعُونَ ألفًا يَدْخُلُونَ الجَنَّةَ بِغَيرِ حِسَابٍ ولا عَذَابٍ))، ثُمَّ نَهَضَ فَدخَلَ مَنْزِلَهُ فَخَاضَ النَّاسُ في أُولئكَ الَّذِينَ يَدْخُلُونَ الجَنَّةَ بِغَيْرِ حِسَابٍ ولا عَذَابٍ، فَقَالَ بَعْضُهُمْ: فَلَعَلَّهُمْ الَّذينَ صَحِبوا رسولَ الله صلى الله عليه وسلم، وَقالَ بعْضُهُمْ: فَلَعَلَّهُمْ الَّذِينَ وُلِدُوا في الإِسْلامِ فَلَمْ يُشْرِكُوا بِالله شَيئًا- وذَكَرُوا أشيَاءَ- فَخَرجَ عَلَيْهِمْ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ: ((مَا الَّذِي تَخُوضُونَ فِيهِ؟)) فَأَخْبَرُوهُ فقالَ: ((هُمُ الَّذِينَ لا يَرْقُونَ، وَلا يَسْتَرقُونَ، وَلا يَتَطَيَّرُونَ؛ وعَلَى رَبِّهِمْ يَتَوكَّلُون)) فقامَ عُكَّاشَةُ بنُ محصنٍ، فَقَالَ: ادْعُ الله أنْ يَجْعَلني مِنْهُمْ، فَقَالَ: ((أنْتَ مِنْهُمْ)). ثُمَّ قَامَ رَجُلٌ آخَرُ، فَقَالَ: ادْعُ اللهَ أنْ يَجْعَلنِي مِنْهُمْ، فَقَالَ: ((سَبَقَكَ بِهَا عُكَّاشَةُ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Nilionyeshwa ummah mbali mbali. Nikamuona Nabiy ana kipote, Nabiy mwengine ana mtu mmoja na wawili, na Nabiy mwengine hana mfuasi. Mara kwa ghafla, nikaonyeshwa kundi kubwa, nikadhani kuwa ni ummah wangu. Nikaambiwa: Huyu ni Muwsaa na Qawmu yake, lakini tazama upande huu. Nikatazama, nikaona kundi kubwa. Nikaambiwa: Tazama upande mwengine. Nikaona kundi kubwa, nikaambiwa: Huu ni Ummah wako, pamoja nao kuna watu sabini elfu wataingia Jannah bila hisabu wala adhabu.” Halafu akainuka na kuingia nyumbani kwake. Watu wakaanza kuzungumza na kujadiliana kuhusu wale watakaoingia Jannah bila hisabu wala adhabu. Baadhi yao wakasema: Labda hao ni wale waliosuhubiana na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Wengine wakasema: Labda hao ni wale waliozaliwa katika Uislamu na wala hawakumshirikisha Allaah na chochote. Wakaongea mambo mengi. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawatokea, akawauliza: “Mlikuwa mnazungumza kuhusu nini?” Wakamueleza. Akawaambia: “Hao ni wale ambao hawazingui (hawafanyi Ruqyyah) wala hawataki kuzinguliwa kutoka kwa mwengine, wala hawapigi ramli na wameegemea kwa Rabb wao tu.” Akasimama ‘Ukaashah bin Mihswan akasema: Muombe Allaah Anijaalie katika wao. Akamwambia: “Wewe ni katika wao.” Kisha akasimama mtu mwengine, akamwambia: Muombe Allaah Anijaalie miongoni mwao. Akamwambia: “Amekutangulia ’Ukaashah (daraja hiyo).” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

عن ابن عباس رضي الله عنهما أيضًا: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم كَانَ يقول: ((اللَّهُمَّ لَكَ أَسْلَمْتُ، وَبِكَ آمَنْتُ، وَعَليْك تَوَكَّلْتُ، وَإِلَيْكَ أنَبْتُ، وَبِكَ خَاصَمْتُ. اللَّهُمَّ إِنِّي أعُوذُ بعزَّتِكَ؛ لا إلهَ إلا أَنْتَ أنْ تُضلَّني، أَنْتَ الحَيُّ الَّذِي لا يَمُوتُ، وَالجِنُّ والإنْسُ يَمُوتُونَ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ، وهذا لفظ مسلم واختصره البخاري

‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesimulia: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba: “Ee Allaah, kwa ajili Yako nimejisalimisha, Kwako tu nimeamini, Wewe pekee nimekutegemea, Kwako tu nimerejea, kwa ajili Yako tu nakhasimiana. Ee Allaah, hakika mimi najilinda kwa utukufu Wako, hakuna Muabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Usinipoteze. Wewe ni Hai Usiekufa, majini na wana-Aadam watakufa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 3

عن ابن عباس رضي الله عنهما أيضًا، قَالَ: حَسْبُنَا اللهُ وَنِعْمَ الوَكِيلُ، قَالَهَا إِبرَاهيمُ صلى الله عليه وسلم حِينَ أُلقِيَ في النَّارِ، وَقَالَها مُحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم حِينَ قَالُوا: إنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إيْمانًا وَقَالُوا: حَسْبُنَا الله ونعْمَ الوَكيلُ. رواه البخاري.

وفي رواية لَهُ عن ابن عَبَّاسٍ رضي الله عنهما، قَالَ: كَانَ آخر قَول إبْرَاهِيمَ صلى الله عليه وسلم حِينَ أُلْقِيَ في النَّارِ: حَسْبِي الله ونِعْمَ الوَكِيلُ

‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Allaah Anatutosha. Naye ni Mdhamini  bora kabisa, neno hili alisema Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) alipotumbukizwa motoni, na alisema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pale watu (walipokodiwa na Maquraysh) walipowaambia (Waislaam): “Maquraysh wamewakusanyikia, kwa hiyo waogopeni. Lakini maneno hayo yaliwazidishia Iymaan (Waislamu) wakasema: Allaah Anatutosha Naye ni Mdhamini bora kabisa.” [Al-Bukhaariy]

Riwaayah nyingine; kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Neno la mwisho alilolitamka Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) wakati alipotumbukizwa kwenye moto ilikuwa ni kusema: “Allaah Ananitosha, Naye ni Mdhamini bora kabisa.”

 

 

Hadiyth – 4

عن أبي هريرةَ رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((يَدْخُلُ الجَنَّةَ أَقْوامٌ أفْئِدَتُهُمْ مِثلُ أفْئِدَةِ الطَّيرِ)). رواه مسلم

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amepokea kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kuna watu wataingia Jannah nyoyo zao ni mithili ya ndege (Kwa ule ulaini wanyoyo za ndege namna zilivyo).” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 5

عن جابر رضي الله عنه: أَنَّهُ غَزَا مَعَ النبي صلى الله عليه وسلم قِبلَ نَجْدٍ، فَلَمَّا قَفَلَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَفَلَ معَهُمْ، فَأَدْرَكَتْهُمُ القَائِلَةُ في وَادٍ كثير العِضَاه، فَنَزَلَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم وَتَفَرَّقَ النَّاسُ يَسْتَظِلُّونَ بالشَّجَرِ، وَنَزَلَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم تَحتَ سَمُرَة فَعَلَّقَ بِهَا سَيفَهُ وَنِمْنَا نَوْمَةً، فَإِذَا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يَدْعونَا وَإِذَا عِنْدَهُ أعْرَابِيٌّ، فَقَالَ: ((إنَّ هَذَا اخْتَرَطَ عَلَيَّ سَيفِي وَأنَا نَائمٌ فَاسْتَيقَظْتُ وَهُوَ في يَدِهِ صَلتًا، قَالَ: مَنْ يَمْنَعُكَ مِنِّي؟ قُلْتُ: الله- ثلاثًا-)) وَلَمْ يُعاقِبْهُ وَجَلَسَ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

وفي رواية قَالَ جَابرٌ: كُنَّا مَعَ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم بذَاتِ الرِّقَاعِ، فَإِذَا أَتَيْنَا عَلَى شَجَرَةٍ ظَلِيلَةٍ تَرَكْنَاهَا لرسول الله صلى الله عليه وسلم، فجاء رَجُلٌ مِنَ المُشْركينَ وَسَيفُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم معَلَّقٌ بالشَّجَرَةِ فَاخْتَرطَهُ، فَقَالَ: تَخَافُنِي؟ قَالَ: ((لا)). فَقَالَ: فَمَنْ يَمْنَعُكَ مِنِّي؟ قَالَ: ((الله)).

وفي رواية أبي بكر الإسماعيلي في صحيحه، قَالَ: مَنْ يَمْنَعُكَ مِنِّي؟ قَالَ: ((اللهُ)). قَالَ: فَسَقَطَ السيفُ مِنْ يَدهِ، فَأخَذَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم السَّيْفَ، فَقَالَ: ((مَنْ يَمْنَعُكَ مني؟)). فَقَالَ: كُنْ خَيرَ آخِذٍ. فَقَالَ: ((تَشْهَدُ أنْ لا إلهَ إلا الله وَأَنِّي رَسُول الله؟)) قَالَ: لا، وَلَكنِّي أُعَاهِدُكَ أنْ لاَ أُقَاتِلَكَ، وَلا أَكُونَ مَعَ قَومٍ يُقَاتِلُونَكَ، فَخَلَّى سَبيلَهُ، فَأَتَى أصْحَابَهُ، فَقَالَ: جئتُكُمْ مِنْ عنْد خَيْرِ النَّاسِ.

Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia kuwa yeye alikwenda kupigana Jihaad sehemu za Najd akiwa pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliporejea, alirejea pamoja nao. Ikawakuta katikati ya mchana katika bonde lenye miti mingi ya miba. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akashuka. Wa nao wakaenea (huku na kule) wakitafuta vivuli vya miti. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alishuka chini ya mti wa samura (aina ya mti wenye miba), akautundika upanga wake, tukalala kidogo. Mara ghafla Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatuita, akawa yupo na mbedui, akatuambia: “Mtu huyo kauchomoa upanga wangu nami nimelala, nikaamka nao upo mkononi mwake, akaniuliza: Ni nani atakaye kuhami dhidi yangu? Nikamjibu: “Allaah mara tatu.” Wala hakumuadhibu, akaketi. [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Riwaayah nyingine inasema: “Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Tulikuwa pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) huko Dhaatir-Riqaa’, tunapofika kwenye mti wenye kivuli, humuachia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Akaja mtu katika mushrikiyn na upanga wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) umetundikwa kwenye mti. Akauchomoa, akamuuliza: Unaniogopa? Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu: “Hapana” Akamuuliza: Ni nani atakaye kuhami dhidi yangu? Akamwambia: “Allaah”.

 

Riwaayah nyingine ya; Abuu Bakr Al-Ismaa’iyl katika sahihi yake, imesema: Akamuuliza: Ni nani atakaye kuhami dhidi yangu? Akamwambia: “Allaah” Upanga ukamuanguka kutoka mkononi mwake. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akauchukua upanga ule. Akamuuliza: “Ni nani atakaye kuhami dhidi yangu?” Akamjibu: Mbora mwenye kuuchukua. Akamuuliza: “Unashuhudia kuwa hakuna Anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na kuwa mimi ni Rasuli Wake?” Akajibu: Hapana. Lakini nakuahidi kuwa sitakupiga vita, wala sitokuwa pamoja na watu wanaopigana na wewe. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuacha aende zake. Akawaendea Maswahaba zake, akawaambia: “Nimewajia kutoka kwa mbora wa watu.”

 

 

Hadiyh – 6

عن عُمَر رضي الله عنه قَالَ: سمعتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((لَوْ أَنَّكُمْ تَتَوَكَّلُونَ عَلَى اللهِ حَقَّ تَوَكُّلِهِ لَرَزَقَكُمْ كَمَا يَرْزُقُ الطَّيْرَ، تَغْدُو خِمَاصًا وَتَرُوحُ بِطَانًا)). رواه الترمذي، وَقالَ: (حديث حسن)

‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Lau mngelikuwa mnamtegemea Allaah ukweli wa kumtegemea, Angewaruzuku kama Anavyowaruzuku ndege. Wanatoka asubuhi wakiwa wana njaa na wanarudi wakiwa wameshiba.” [At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth hii ni Hasan]

 

 

Hadiyth – 7

عن أبي عُمَارة البراءِ بن عازب رضي الله عنهما، قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((يَا فُلانُ، إِذَا أَوَيْتَ إِلَى فراشِكَ، فَقُل: اللَّهُمَّ أسْلَمتُ نَفْسي إلَيْكَ، وَوَجَّهتُ وَجْهِي إلَيْكَ، وَفَوَّضتُ أَمْري إلَيْكَ، وَأَلجأْتُ ظَهري إلَيْكَ رَغبَةً وَرَهبَةً إلَيْكَ، لا مَلْجَأ وَلا مَنْجَا مِنْكَ إلا إلَيْكَ، آمنْتُ بِكِتَابِكَ الَّذِي أنْزَلْتَ؛ وَنَبِيِّكَ الَّذِي أَرْسَلْتَ. فَإِنَّ مِتَّ مِنْ لَيلَتِكَ مِتَّ عَلَى الفِطْرَةِ، وَإِنْ أصْبَحْتَ أَصَبْتَ خَيرًا)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

وفي رواية في الصحيحين، عن البراءِ، قَالَ: قَالَ لي رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((إِذَا أَتَيْتَ مَضْجِعَكَ فَتَوَضَّأْ وُضُوءكَ للصَّلاةِ، ثُمَّ اضْطَجعْ عَلَى شِقِّكَ الأَيمَنِ، وَقُلْ... وذَكَرَ نَحْوَهُ ثُمَّ قَالَ: وَاجْعَلْهُنَّ آخِرَ مَا تَقُولُ))

Abuu ‘Umaarah Al-Baraa bin ‘Aazib (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia mtu: “Ee fulani utakapokiendea kitanda chako, sema: Ee Allaah, nimejisalimisha Kwako, uso wangu nimeuwelekeza Kwako, mambo yangu nimekuachia Wewe, nimekuegemeza Wewe kwa kutaraji thawabu Zako na kuogopa dhambi Zako, hakuna sehemu ya kuegemea wala kukuepuka ila ni Kwako. Nimekiamini Kitabu Chako Ulichokiteremsha na Rasuli Wako Uliyemtuma. Basi utakapofikwa na mauti usiku huo, utakuwa umekufa katika Uislamu, na ukipambaukiwa utapata khayr.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Riwaayah nyingine iliyomo katika Sahihi Al-Bukhaariy na Sahihi Muslim; kutoka kwa Al-Baraa imesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: “Unapokwenda sehemu yako ya kulala, tawadha wudhuu wa Swalaah, kisha ulale kwa upande wako wa kulia na usema: (Akajata mfano wake kama ilivyotangulia) “Maneno hayo ndiyo yawe ya mwisho utakayoyasema.”

 

 

Hadiyth – 8

عن أبي بكرٍ الصِّديق رضي الله عنه عبدِ اللهِ بنِ عثمان بنِ عامرِ بنِ عمر ابنِ كعب بنِ سعدِ بن تَيْم بنِ مرة بن كعبِ بن لُؤَيِّ بن غالب القرشي التيمي رضي الله عنه وَهُوَ وَأَبُوهُ وَأُمُّهُ صَحَابَةٌ رضي الله عنهم قَالَ: نَظَرتُ إِلَى أَقْدَامِ المُشْرِكينَ وَنَحنُ في الغَارِ وَهُمْ عَلَى رُؤُوسِنا، فقلتُ: يَا رسولَ الله، لَوْ أَنَّ أَحَدَهُمْ نَظَرَ تَحْتَ قَدَمَيهِ لأَبْصَرَنَا. فَقَالَ: ((مَا ظَنُّكَ يَا أَبا بَكرٍ باثنَيْنِ الله ثَالِثُهُمَا)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Abuu Bakr As-Swidiyq, ‘Abdullaah ‘Uthmaan bin ‘Aamir bin ‘Umar bin Ka’b bin Sa’d bin Taym bin Murrah bin Ka’b bin Lu-ayy bin Ghaalib Al-Qurashiy At-Taymiy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) yeye, baba yake na mama yake wote ni maswahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) amesema: Niliitazama miguu ya mshirikina nasi tupo pangoni nao wapo juu yetu (wanatutafuta ili watuue). Nikamwambia: Yaa Rasula-Allaah, lau mmoja wao atautazama mguu wake atatuona! Akasema: “Ee Abuu Bakr, unadhaniaje watu wawili ambao watatu wao ni Allaah?” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 9

عن أم المُؤمنينَ أمِّ سَلَمَةَ وَاسمها هِنْدُ بنتُ أَبي أميةَ حذيفةَ المخزومية رضي الله عنها: أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا خَرَجَ مِنْ بَيتِهِ، قَالَ: ((بِسْمِ اللهِ تَوَكَّلتُ عَلَى اللهِ، اللَّهُمَّ إِنِّي أعُوذُ بِكَ أنْ أضِلَّ أَوْ أُضَلَّ، أَوْ أَزِلَّ أَوْ أُزَلَّ، أَوْ أظْلِمَ أَوْ أُظْلَمَ، أَوْ أجْهَلَ أَوْ يُجْهَلَ عَلَيَّ)) حديثٌ صحيح، رواه أبو داود والترمذي وغيرهما بأسانيد صحيحةٍ. قَالَ الترمذي: (حديث حسن صحيح). وهذا لفظ أبي داود

Mama wa Waumini, Ummu Salamah, jina lake ni Hindu bint Abiy Umayyah Hudhayfah Al-Makhzumiyyah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesimulia: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapotoka nyumbani kwake husema: “Kwa jina la Allaah, Nimeegemea kwa Allaah. Ee Allaah, kwa hakika najilinda Kwako nisije nikapotea au kupotezwa, au nikateleza au nikatelezeshwa, au nikadhumu au nikadhulumiwa au nikafanya ujinga au nikafanyiwa ujinga.” [Hadiyth hii, ni Sahihi imepokelewa na Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy na wengineo kwa isnaad Sahihi. At-Tirmidhiy amesema: Hadiyth hii ni Hasan Sahih]

 

 

Hadiyth – 10

عن أنس رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ قَالَ- يَعْني: إِذَا خَرَجَ مِنْ بَيتِهِ: بِسمِ اللهِ تَوَكَّلْتُ عَلَى اللهِ، وَلا حَولَ وَلا قُوَّةَ إلا باللهِ، يُقالُ لَهُ: هُدِيتَ وَكُفِيتَ وَوُقِيتَ، وَتَنَحَّى عَنْهُ الشَّيطَانُ)). رواه أبو داود والترمذي والنسائي وغيرهم. وَقالَ الترمذي: (حديث حسن)، زاد أبو داود: ((فيقول- يعني: الشيطان-- لِشيطان آخر: كَيفَ لَكَ بِرجلٍ قَدْ هُدِيَ وَكُفِيَ وَوُقِيَ؟))

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayesema anapotoka nyumbani kwake. Kwa jina la Allaah nimeegemea kwa Allaah, hakuna namna ya kuepuka maasi wala nguvu ya kufanya ‘Ibaadah ila kwa msaada wa Allaah. Ataambiwa: Umeshaongozwa, umeshatoshelezwa, na umeshakingwa, na shaytwaan hujitenga naye.” [Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na wengineo. At-Tirmidhiy amesema: Hadiyth hii ni Hasan]

Abuu Daawuwd ameongezea: Shaytwaan humueleza shaytwaan mwenzie: Utamuwezaje mtu aliyeongozwa, akatoshelezwa na akakingwa?

 

 

 

Hadiyth – 11

وعن أنس رضي الله عنه قَالَ: كَانَ أَخَوانِ عَلَى عهد النَّبيّ صلى الله عليه وسلم وَكَانَ أحَدُهُمَا يَأتِي النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم وَالآخَرُ يَحْتَرِفُ، فَشَكَا المُحْتَرِفُ أخَاهُ للنبي صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ: ((لَعَلَّكَ تُرْزَقُ بِهِ)). رواه الترمذي بإسناد صحيحٍ عَلَى شرطِ مسلم

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Kulikuwepo  ndugu wawili zama za Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), mmoja alikuwa akienda kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) (na kukaa naye), na mwengine anafanya kazi; yule anayefanya kazi akamshitakia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) dhidi ya ndugu yake, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Pengine wewe unaruzukiwa kwa sababu yake.” [At-Tirmidhiy kwa isnaad Swahiyh]

 

 

 

Share