008-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Istiqaamah Kuthibitika Imara

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب الاستقامة

008 - Mlango Wa Istiqaamah - Kuthibitika Imara (Kuwa Na Msimamo)

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ اللهُ تَعَالَى:

فَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ

Basi thibitika imara kama ulivyoamrishwa. [Huwd: 112]

 

إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ ﴿٣٠﴾

Hakika wale waliosema: “Rabb wetu ni Allaah.” Kisha wakathibitika imara; Malaika huwateremkia (wanapofishwa kuwaambia): “Msikhofu, na wala msihuzunike, na pokeeni bishara njema ya Jannah ambayo mlikuwa mkiahidiwa.”

 

نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَشْتَهِي أَنفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ ﴿٣١﴾

“Sisi ni walinzi wenu katika uhai wa dunia na katika Aakhirah. Na mtapata humo yale yanayotamani nafsi zenu, na mtapata humo yale mtakayoomba. [Fusw-swilat: 30-31]

 

إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿١٣﴾

Hakika wale waliosema: “Rabb wetu ni Allaah.” Kisha wakathibitika imara, basi hakutokuwa na khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.

 

أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٤﴾

Hao ndio watu wa Jannah, ni wenye kudumu humo, jazaa kwa yale waliyokuwa wakitenda. [Al-Ahqaaf: 13-14]

 

 

Hadiyth – 1

 

وعن أبي عمرو، وقيل: أبي عَمرة سفيان بن عبد الله رضي الله عنه قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُول الله، قُلْ لي في الإسْلامِ قَولًا لا أسْأَلُ عَنْهُ أَحَدًا غَيْرَكَ. قَالَ: ((قُلْ: آمَنْتُ بِاللهِ، ثُمَّ استَقِمْ)). رواه مسلم

Abuu ‘Amru, au Abuu 'Amrah Sufyaan bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nilimwambia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam); niambie neno katika Uislamu ambalo sitamuuliza yoyote zaidi yako. Akasema: “Sema: Nimemuamini Allaah, kisha uthibitike imara.” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

 

وعن أبي هريرةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((قَارِبُوا وَسَدِّدُوا، وَاعْلَمُوا أَنَّهُ لَنْ يَنْجُوَ أَحَدٌ مِنْكُمْ بعَمَلِهِ)) قالُوا: وَلا أَنْتَ يَا رَسُول الله؟ قَالَ: ((وَلا أنا إلا أنْ يَتَغَمَّدَني الله برَحمَةٍ مِنهُ وَفَضْلٍ)). رواه مسلم

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Alisema: “Fanyeni wastani (msivuke mipaka) na muwe na msimamo. Jueni kwamba  hakuna yeyote yule miongoni mwenu atakayeokoka na 'amali yake.” Maswahaba wakamuuliza: Hata wewe ee Rasuli wa Allaah? Akajibu: “Hata mimi, isipokuwa Allaah Anifunike kwa rahmah na fadhila Zake.” [Muslim]    

 

 

 

Share