009-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kutafakari Viumbe ‘Adhiym Vya Allaah Dunia Kutoweka ...

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب التفكر في عظيم مخلوقات الله تَعَالَى، وفناء الدنيا وأهوال الآخرة وسائر أمورهما وتقصير النفس، وتهذيبها وحملها عَلَى الاستقامة

 

009 – Mlango Wa Kutafakari Viumbe ‘Adhiym Vya Allaah, Dunia Kutoweka – Vitisho Vya Aakhirah Na Mambo Mengine Yanayohusiana Nayo Nafsi Kufanya Taqswiyr, Kuiadabisha Nafsi Na Kuifanya Iwe Na Msimamo

 

قَالَ اللهُ تَعَالَى:

قُلْ إِنَّمَا أَعِظُكُم بِوَاحِدَةٍ ۖ أَن تَقُومُوا لِلَّـهِ مَثْنَىٰ وَفُرَادَىٰ ثُمَّ تَتَفَكَّرُوا ۚ

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika nakuwaidhini kwa jambo moja tu!  Msimame kwa ajili ya Allaah wawili wawili, au mmoja mmoja kisha mtafakari.” [Sabaa: 46]

 

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾ 

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko (ya mfuatano) ya usiku na mchana; bila shaka ni Aayaat (ishara, dalili, zingatio n.k) kwa wenye akili.

 

الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَـٰذَا بَاطِلًا سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴿١٩١﴾ 

Ambao wanamdhukuru Allaah (kwa) kusimama, na (kwa) kukaa na (kwa) kulala ubavuni mwao na wanatafakari katika kuumbwa mbingu na ardhi (wakisema): “Rabb wetu, Hukuumba haya bure. Subhaanak! (Utakasifu ni Wako!) Tukinge na adhabu ya moto. [Aal-‘Imraan: 190-191]

 

أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ ﴿١٧﴾

Je, hawamtazami ngamia namna walivyoumbwa?

 

وَإِلَى السَّمَاءِ كَيْفَ رُفِعَتْ ﴿١٨﴾

Na mbingu vipi zilivyonyanyuliwa?

 

وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ ﴿١٩﴾

Na majabali vipi yamekongomewa imara.

 

وَإِلَى الْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ ﴿٢٠﴾

Na ardhi vipi ilivyotandazwa?

 

فَذَكِّرْ إِنَّمَا أَنتَ مُذَكِّرٌ ﴿٢١﴾

Basi kumbusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم); hakika wewe ni mkumbushaji tu. [Al-Ghaashiyah: 17-21]

 

أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ

Je, hawakutembea katika ardhi wakatazama vipi imekuwa hatima ya ambao wa kabla yao? [Muhammad: 10]

 

 

 

 

Share