010-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukimbilia Mambo ya Khayr...
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب المبادرة إلى الخيرات، وحثِّ من توجه لخير على الإقبال عليه بالجد من غير تردد
010 – Mlango Wa Kukimbilia Mambo ya Khayr Na Kumuhimiza Anayefanya Khayr Kuielekea Kwa Jitihada Bila Kusitasita
قَالَ اللهُ تَعَالَى:
فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ ۚ
Basi shindaneni kwenye khayraat. [Al-Baqarah: 148]
وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ ﴿١٣٣﴾
Na kimbilieni maghfirah kutoka kwa Rabb wenu na Jannah upana wake ni wa mbingu na ardhi imeandaliwa kwa wenye taqwa. [Aal-‘Imraan: 133]
Hadiyth – 1
عن أبي هريرة رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((بَادِرُوا بِالأعْمَال فتنًا كقطَعِ اللَّيْلِ المُظْلِمِ، يُصْبحُ الرَّجُلُ مُؤْمِنًا وَيُمْسِي كَافِرًا، وَيُمْسِي مُؤمِنًا ويُصبحُ كَافِرًا، يَبيعُ دِينَهُ بعَرَضٍ مِنَ الدُّنيا)). رواه مسلم
Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Zikimbilieni ‘amali njema kwani zitakuja fitnah (nyingi) kama mfano wa usiku na kiza. Mtu atapambaukiwa akiwa Muumin na akifikiwa na jioni hali ya kuwa ni kafiri, au atafikiwa jioni akiwa Muumin na atapambaukiwa akiwa kafiri, anaiuza Dini yake kwa thamani ya dunia.” [Muslim]
Hadiyth – 2
عن أبي سِروْعَة- بكسر السين المهملة وفتحها- عُقبةَ بن الحارث رضي الله عنه قَالَ: صَلَّيتُ وَرَاءَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم بالمَدِينَةِ العَصْرَ، فَسَلَّمَ ثُمَّ قَامَ مُسْرِعًا، فَتَخَطَّى رِقَابَ النَّاسِ إِلَى بعْضِ حُجَرِ نِسَائِهِ، فَفَزِعَ النَّاسُ مِنْ سُرْعَتِهِ، فَخَرَجَ عَلَيهمْ، فَرأى أنَّهمْ قَدْ عَجبُوا مِنْ سُرعَتهِ، قَالَ: ((ذَكَرتُ شَيئًا مِنْ تِبرٍ عِندَنَا فَكَرِهتُ أنْ يَحْبِسَنِي فَأمَرتُ بِقِسْمَتِهِ)). رواه البخاري.
وفي رواية لَهُ: ((كُنتُ خَلَّفتُ في البَيْتِ تِبرًا مِنَ الصَّدَقةِ فَكَرِهتُ أنْ أُبَيِّتَهُ)). ((التِّبْرُ))
Abuu Sirw’ah, ‘Uqbah bin Al-Haarith (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Niliswali nyuma ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Swalaah ya Al-‘Aswr Madiynah. Akatoa salaam kisha akainuka kwa haraka, akawa anaziruka shingo za watu kuelekea katika chumba cha mkewe. Watu wakapata mshangao kwa ile haraka yake. Kisha akawatokezea na kuwaona wamemstajabu kwa ile haraka yake, akawaambia: “Nilikumbuka kitu katika kipande cha dhahabu kilichokuwa kwetu, nikakichukua kisije kikanizuia, nikaamuru kigawanywe.” [Al-Bukhaariy]
Riwaayah nyingine ya Al-Bukhaariy imesema:
“Nilikuwa nimeacha nyumbani kipande cha dhahabu cha Swadaqah, nikachukia kisije kikapitiwa na usiku (nacho kipo nyumbani).”
Hadiyth – 3
عن جابر رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رجل للنبي صلى الله عليه وسلم يَومَ أُحُد: أَرَأيتَ إنْ قُتِلتُ فَأَيْنَ أَنَا؟ قَالَ: ((في الجنَّةِ)) فَأَلْقَى تَمَرَاتٍ كُنَّ في يَدِهِ، ثُمَّ قَاتَلَ حَتَّى قُتِلَ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: mtu mmoja alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) siku ya Vita vya Uhud: Niambie nikiuliwa nitakwenda wapi? Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu: “Jannah.” Akazitupa tende chache alizokuwa nazo mkononi mwake, kisha akapigana mpaka akauliwa. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
عن أبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ: جاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: يَا رسولَ الله، أيُّ الصَّدَقَةِ أعْظَمُ أجْرًا؟ قَالَ: ((أنْ تَصَدَّقَ وَأنتَ صَحيحٌ شَحيحٌ، تَخشَى الفَقرَ وتَأمُلُ الغِنَى، وَلا تُمهِلْ حَتَّى إِذَا بَلَغتِ الحُلقُومَ قُلْتَ لِفُلان كذا ولِفُلانٍ كَذا، وقَدْ كَانَ لِفُلانٍ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه
Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza: Yaa Rasula-Allaah, ni swadaqah ipi yenye ujira mkubwa zaidi? Akajibu: “Utoe swadaqah nawe ni mzima, unatamani mali na unakhofia ufakiri na unatarajia utajiri, wala usichelewe mpaka roho ikafika kwenye koo, ukaanza kusema: Fulani ana haki kadhaa na fulani ana haki kadhaa, na fulani alikuwa ana haki kadhaa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 5
عن أنس رضي الله عنه: أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم أخذ سيفًا يَومَ أُحُدٍ، فَقَالَ: ((مَنْ يَأخُذُ منِّي هَذَا؟)) فَبَسطُوا أيدِيَهُمْ كُلُّ إنسَانٍ مِنْهُمْ يقُولُ: أَنَا أَنَا. قَالَ: ((فَمَنْ يَأخُذُهُ بحَقِّه؟)) فَأَحْجَمَ القَومُ فَقَالَ أَبُو دُجَانَةَ رضي الله عنه: أنا آخُذُهُ بِحَقِّهِ، فأخذه فَفَلقَ بِهِ هَامَ المُشْرِكِينَ. رواه مسلم
Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) anaelezea kuwa: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alichukua upanga siku ya Vita vya Uhud. Akauliza: “Ni nani atakayeuchukua upanga huu kutoka kwangu?” Kila mmoja wao akanyoosha mkono akisema: Mimi, mimi. Akawauliza: “Ni nani atakayeuchukua kwa haki yake?” Watu wakasita. Abuu Dujaanah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akasema: Mimi nitauchukua kwa haki yake. Akauchukua, akawa anakata vichwa vya washirikina (katika Jihaad). [Muslim]
Hadiyth – 6
عن الزبير بن عدي، قَالَ: أتينا أنسَ بن مالك رضي الله عنه فشكونا إِلَيْه مَا نلقى مِنَ الحَجَّاجِ. فَقَالَ: ((اصْبرُوا؛ فَإنَّهُ لا يَأتي عَلَيْكُم زَمَانٌ إلا والَّذِي بَعدَهُ شَرٌّ مِنهُ حَتَّى تَلقَوا رَبَّكُمْ)) سَمِعتُهُ مِنْ نَبِيِّكُمْ صلى الله عليه وسلم. رواه البخاري
Az-Zubayr bin ‘Adiyy amesema: Tulimuendea Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) tukamlalamikia hali tuliyoipata kwa Al-Hajjaaj. Akatuambia: Subirini, hakika haiji zama ila zama zilizokuja baadaye ni shari kulikoni zilizopita mpaka mkutane na Rabb wenu. Maneno haya nimeyasikia kutoka kwa Nabiy wenu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 7
عن أبي هريرة رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((بادِرُوا بِالأَعْمَالِ سَبْعًا، هَلْ تَنْتَظِرُونَ إلا فَقرًا مُنسيًا، أَوْ غِنىً مُطغِيًا، أَوْ مَرَضًا مُفسِدًا، أَوْ هَرَمًا مُفْندًا، أَوْ مَوتًا مُجْهزًا، أَوْ الدَّجَّالَ فَشَرُّ غَائِبٍ يُنْتَظَرُ، أَوْ السَّاعَةَ فالسَّاعَةُ أدهَى وَأَمَرُّ)). رواه الترمذي، وَقالَ: (حديث حسن)
Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Zikimbilieni ‘amali njema kabla haijawafikia mambo saba. Je, mnangoja mpaka mfikwe na ufukara wenye kusahaulisha, au utajiri unaopoteza, au maradhi yenye kufisidi, au uzee uletao udhaifu wa akili, au mauti ya ghafla, au Dajjaal ambaye ndio kiumbe muovu asiyepaswa kusubiriwa, au Qiyaamah, na Qiyaamah ndio chenye balaa kubwa na uchungu mwingi zaidi!” [A-Tirmidhiy, na amesema Hadiyth hii ni Hasan]
Hadiyth – 8
أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ يَومَ خيبر: ((لأُعْطِيَنَّ هذِهِ الرَّايَةَ رَجُلًا يُحِبُّ اللهَ وَرَسُولَهُ يَفتَحُ اللهُ عَلَى يَدَيهِ)). قَالَ عُمَرُ رضي الله عنه: مَا أحبَبْتُ الإِمَارَة إلا يَومَئِذٍ، فَتَسَاوَرتُ لَهَا رَجَاءَ أنْ أُدْعَى لَهَا، فَدَعا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم عليّ بن أبي طالب رضي الله عنه فَأعْطَاهُ إيَّاهَا، وَقالَ: ((امْشِ وَلا تَلتَفِتْ حَتَّى يَفتَح اللهُ عَلَيكَ)). فَسَارَ عليٌّ شيئًا ثُمَّ وَقَفَ ولم يلتفت فصرخ: يَا رَسُول الله، عَلَى ماذا أُقَاتِلُ النّاسَ؟ قَالَ: ((قاتِلْهُمْ حَتَّى يَشْهَدُوا أنْ لا إله إلا اللهُ، وَأنَّ مُحَمدًا رسولُ الله، فَإِذَا فَعَلُوا ذلك فقَدْ مَنَعوا مِنْكَ دِمَاءهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ إلا بحَقِّهَا، وحسَابُهُمْ عَلَى الله)). رواه مسلم
Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema siku ya Vita vya Khaybar: “Kwa hakika bendera hii nitampa mtu anayempenda Allaah na Rasuli Wake, Allaah Ataleta ushindi kwa sababu yake.” ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) anasema: Sikuwahi kuupenda uamiri jeshi isipokuwa siku hiyo. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuita ‘Aliy bin Abiy Twaalib, akampa bendera ile. Akamwambia: “Nenda wala usigeuke mpaka Allaah Akupe ushindi.” ‘Aliy akatembea kidogo. Kisha akasimama wala hakugeuka nyuma, akauliza kwa sauti ya juu: Yaa Rasula-Allaah, nipigane na watu juu ya nini? Akamwambia: “Pigana nao mpaka washuhudie kuwa hapana Muabudiwa wa haki ispokuwa Allaah, na Muhammad ni Rasuli wa Allaah. Wakifanya hivyo, wameshahifadhika kutokana na nawe katika damu zao na mali yao ila kwa haki yake, na hisabu yao ipo kwa Allaah.” [Muslim]