013-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ubainifu Wa Njia Nyingi Za Khayr

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب في بيان كثرة طرق الخير

13 – Mlango Wa Ubainifu Wa Njia Nyingi Za Khayr

 

Alhidaaya.com

 

 

قَالَ الله تَعَالَى:

 

وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٢١٥﴾

Na lolote mlifanyalo katika khayr basi hakika Allaah kwa hilo ni Mjuzi.[Al-Baqarah: 215]

 

وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ﴿١٩٧﴾

Na lolote mlifanyalo katika ya khayr Allaah Analijua. [Al-Baqarah: 197]

 

فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾

Basi yule atakayetenda kheri uzito wa chembe ya atomu (au mdudu chungu) ataiona. [Az-Zalzalah: 7]

 

مَنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِنَفْسِهِ ۖ ﴿١٥﴾

Yeyote atendaye jema, basi ni kwa ajili ya nafsi yake. [Al-Jaathiyah: 15]

 

 

Hadiyh – 1

 

عن أبي ذر جُنْدبِ بنِ جُنَادَةَ رضي الله عنه قَالَ: قُلْتُ: يَا رسولَ الله، أيُّ الأعمالِ أفْضَلُ؟ قَالَ: ((الإيمانُ باللهِ وَالجِهادُ في سَبيلِهِ)). قُلْتُ: أيُّ الرِّقَابِ أفْضَلُ؟ قَالَ: ((أنْفَسُهَا عِنْدَ أهلِهَا وَأكثَرهَا ثَمَنًا)). قُلْتُ: فإنْ لَمْ أفْعَلْ؟ قَالَ: ((تُعِينُ صَانِعًا أَوْ تَصْنَعُ لأَخْرَقَ)). قُلْتُ: يَا رَسُول الله، أرأيْتَ إنْ ضَعُفْتُ عَنْ بَعْضِ العَمَلِ؟ قَالَ: ((تَكُفُّ شَرَّكَ عَنِ النَّاسِ؛ فإنَّهَا صَدَقَةٌ مِنْكَ عَلَى نَفْسِكَ)). مُتَّفَقٌ عليه

Abuu Dharr, Jundub bin Junaadah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nilimuuliza Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Ni ‘amali gani bora zaidi? Akajibu: “Ni kumuamini Allaah na kupigana Jihaad katika njia Yake.” Nikamuuliza: Ni kupi kuacha huru mtumwa kuliko bora zaidi? Akajibu: “Ni yule aliye mbora na mzuri kwa watu wake na mwenye thamani kubwa.” Nikamuuliza: Nisipoweza? Akajibu: “Umsaidie mwenye kuhitaji au umsaidie kazi yule ambaye hana ujuzi nayo.” Nikamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah, nieleze iwapo sitoweza kufanya baadhi ya ‘amali? Akajibu: “Utaizuia shari yako isiwafikie watu; kufanya hivyo ni swadaqah juu ya nafsi yako.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

 

عن أبي ذر أيضًا رضي الله عنه: أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((يُصْبحُ عَلَى كُلِّ سُلامَى منْ أَحَدِكُمْ صَدَقةٌ: فَكُلُّ تَسبيحَةٍ صَدَقَةٌ، وَكُلُّ تَحمِيدةٍ صَدَقَة، وَكُلُّ تَهْلِيلَةٍ صَدَقَةٌ، وَكُلُّ تَكبيرَةٍ صَدَقَةٌ، وَأمْرٌ بِالمعرُوفِ صَدَقةٌ، ونَهيٌ عَنِ المُنْكَرِ صَدَقةٌ، وَيُجزئُ مِنْ ذلِكَ رَكْعَتَانِ يَركَعُهُما مِنَ الضُّحَى)). رواه مسلم

Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hupambaukiwa kila kiungo cha mmoja wenu kulazimika kutoa swadaqah. Kila Tasbiyh (Subhaana Allaah) ni swadaqah, kila Tahmiyd (AlhamduliLLaah) ni swadaqah, kila Tahliyl (Laa ilaaha illa-Allaah) ni swadaqah, na kila Takbiyr (Allaahu Akbar) ni swadaqah. Kuamrisha mema ni swadaqah na kukataza maovu ni swadaqah. Yote haya hutosheleza na rakaa mbili za Dhwuhaa mtu anapoziswali.” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

 

عَنْهُ، قَالَ: قَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم: ((عُرِضَتْ عَلَيَّ أعْمَالُ أُمَّتِي حَسَنُهَا وَسَيِّئُهَا فَوَجَدْتُ في مَحَاسِنِ أعْمَالِهَا الأذَى يُمَاطُ عَنِ الطَّريقِ، وَوَجَدْتُ في مَسَاوِئِ أعمَالِهَا النُّخَاعَةُ تَكُونُ في المَسْجِدِ لا تُدْفَنُ)). رواه مسلم

Abuu Dharr (RadhwiyaAllaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Nilionyeshwa ‘amali nzuri na mbaya za Ummah wangu. Nikaona katika jumla ya mema yao ni kuondoshwa takataka njiani, na nikaona katika jumla ya mabaya yao ni kutema mate Masjid na wala yasifunikwe.” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 4

 

عَنْهُ: أنَّ ناسًا قالوا: يَا رَسُولَ الله، ذَهَبَ أهلُ الدُّثُور بالأُجُورِ، يُصَلُّونَ كَمَا نُصَلِّي، وَيَصُومُونَ كَمَا نَصُومُ، وَيَتَصَدَّقُونَ بِفُضُولِ أمْوَالِهِمْ، قَالَ: ((أَوَلَيسَ قَدْ جَعَلَ اللهُ لَكُمْ مَا تَصَدَّقُونَ بِهِ: إنَّ بِكُلِّ تَسْبِيحَةٍ صَدَقةً، وَكُلِّ تَكبيرَةٍ صَدَقَةً، وَكُلِّ تَحمِيدَةٍ صَدَقَةً، وَكُلِّ تَهْلِيلَةٍ صَدَقَةً، وَأمْرٌ بالمَعْرُوفِ صَدَقَةٌ، وَنَهيٌ عَنِ المُنْكَرِ صَدَقَةٌ، وفي بُضْعِ أَحَدِكُمْ صَدَقَةٌ)) قالوا: يَا رسولَ اللهِ، أيَأتِي أَحَدُنَا شَهْوَتَهُ وَيَكُونُ لَهُ فِيهَا أجْرٌ؟ قَالَ: ((أرَأيتُمْ لَوْ وَضَعَهَا في حَرامٍ أَكَانَ عَلَيهِ فِيهَا وِزرٌ؟ فكذَلِكَ إِذَا وَضَعَهَا في الحَلالِ كَانَ لَهُ أَجْرٌ)). رواه مسلم

Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: Baadhi ya watu walimuendea Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakamwambia: Ee Rasuli wa Allaah, matajiri wamechukua thawabu zote. Wao wanaswali kama tunavyoswali, wanafunga kama tunavyofunga na wanatoa swadaqah katika mali yao iliyobaki. Akawaambia: “Nanyi pia Allaah Amewajaalia cha kutolea swadaqah; kila Tasbiyh (Subhaana Allaah) ni swadaqah, na kila Takbiyr (Allaahu Akbar) ni swadaqah, na kila Tahliyl (Laa ilaaha illa-Allaah) ni swadaqah, na kila Tahmiyd (AlhamduliLLaah) ni swadaqah. Kuamrisha mema ni swadaqah na kukataza maovu ni swadaqah, na mmoja wenu kujimai na mke wake ni swadaqah.” Wakauliza: Ee Rasuli wa Allaah, mmoja wetu anaenda kufanya matamanio yake na awe amepata swadaqah? Akawaambia: “Nielezeni lau kitendo kile atakifanya kwa njia ya haraam, si atapata dhambi? Vile vile atakapokitenda kwa njia ya halaal atakuwa na ujira.” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 5

 

عَنْهُ، قَالَ: قَالَ لي النَّبيّ صلى الله عليه وسلم: ((لاَ تَحْقِرنَّ مِنَ المَعرُوفِ شَيئًا وَلَوْ أنْ تَلقَى أخَاكَ بِوَجْهٍ طَليقٍ)). رواه مسلم

Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinambia: “Usidharau chochote katika wema hata kama ni kumtazama ndugu yako (Muislamu) kwa uso wenye bashasha.” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 6

 

عن أبي هريرةَ رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((كُلُّ سُلامَى مِنَ النَّاسِ عَلَيهِ صَدَقَةٌ، كُلَّ يَومٍ تَطلُعُ فِيهِ الشَّمْسُ: تَعْدِلُ بَينَ الاثْنَينِ صَدَقةٌ، وتُعِينُ الرَّجُلَ في دَابَّتِهِ، فَتَحْمِلُهُ عَلَيْهَا أَوْ تَرفَعُ لَهُ عَلَيْهَا مَتَاعَهُ صَدَقَةٌ، وَالكَلِمَةُ الطَيِّبَةُ صَدَقَةٌ، وبكلِّ خَطْوَةٍ تَمشيهَا إِلَى الصَّلاةِ صَدَقَةٌ، وتُميطُ الأذَى عَنِ الطَّريقِ صَدَقَةٌ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

ورواه مسلم أيضًا من رواية عائشة رَضي الله عنها، قَالَتْ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((إنَّهُ خُلِقَ كُلُّ إنْسان مِنْ بَنِي آدَمَ عَلَى سِتِّينَ وثلاثمائة مفْصَل، فَمَنْ كَبَّرَ اللهَ، وحَمِدَ الله، وَهَلَّلَ اللهَ، وَسَبَّحَ الله، وَاسْتَغْفَرَ الله، وَعَزَلَ حَجَرًا عَنْ طَريقِ النَّاسِ، أَوْ شَوْكَةً، أَوْ عَظمًا عَن طَريقِ النَّاسِ، أَوْ أمَرَ بمَعْرُوف، أَوْ نَهَى عَنْ منكَر، عَدَدَ السِّتِّينَ والثَّلاثِمائَة فَإنَّهُ يُمْسِي يَومَئِذٍ وقَدْ زَحْزَحَ نَفسَهُ عَنِ النَّارِ))

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Viungo vyote vya wana Aadam vinawajibia kutoa swadaqah kwa kila siku inapochomozewa na jua. Kusuluhisha kwa uadilifu baina ya watu wawili ni swadaqah. Kumsaidia mtu juu ya mnyama wake ukampandisha au ukamnyanyulia mzigo wake ni swadaqah, kuongea neno zuri ni swadaqah, kila hatua unayoipiga kwenda Masjid ni swadaqah na kuondoa takataka njani ni swadaqah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Vile vile Muslim ameipokea Hadiyth hii kutoka katika riwaayah ya; ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika kila mwana Aadam ameumbwa kwa viungo (vilivyotengana) mia tatu na sitini, atakayemtukuza Allaah (kwa Allaahu Akbar), akamhimidi Allaah (AlhamduliLLaah), akampwekesha Allaah (laa ilaaha illa-Allaah) akamsabih Allaah (Subhaana Allaah), akamuomba Allaah maghfirah (Astaghfiru-Allaah), akaondoa jiwe katika njia wanayopita watu, au akaamrisha mema na kukataza maovu kwa hiyo idadi ya mia tatu na sitini, hakika siku hiyo atafikwa na jioni haliyakuwa ameepushwa na moto.”

 

 

Hadiyth – 7

 

عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((مَنْ غَدَا إِلَى المسْجِد أَوْ رَاحَ، أَعَدَّ اللهُ لَهُ في الجَنَّةِ نُزُلًا كُلَّمَا غَدَا أَوْ رَاحَ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amepokea kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Anayekwenda Masjid asubuhi au jioni, Allaah Humuandalia takrima  (mapokelewo  bora) Jannah kila anapokwenda, (iwe ni) asubuhi au jioni.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 8

 

عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((يَا نِسَاءَ المُسْلِمَاتِ، لا تَحْقِرنَّ جَارَةٌ لِجَارَتِهَا وَلَوْ فِرْسِنَ شاةٍ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

 

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaambia wanawake: “Enyi wanawake wa Kiislamu, jirani asidharau kamwe kumpa zawadi jirani yake japo ni kwato ya mbuzi.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 9

 

عَنْهُ، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((الإيمانُ بِضْعٌ وَسَبعُونَ أَوْ بِضعٌ وسِتُونَ شُعْبَةً: فَأفْضَلُهَا قَولُ: لا إلهَ إلا اللهُ، وَأَدْنَاهَا إمَاطَةُ الأذَى عَنِ الطَّريقِ، والحياءُ شُعبَةٌ مِنَ الإيمان)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amepokea kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Iymaan ni tanzu (matawi) sabini na kitu” au alisema: “ni tanzu (matawi) sitini na kitu, iliyo bora zaidi ni kusema: Laa Ilaaha illa-Allaah. Na ya chini ni kuondoa takataka njiani; na hayaa ni tawi katika matawi ya iymaan.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 10

 

عَنْهُ: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((بَينَما رَجُلٌ يَمشي بِطَريقٍ اشْتَدَّ عَلَيهِ العَطَشُ، فَوَجَدَ بِئرًا فَنَزَلَ فِيهَا فَشربَ، ثُمَّ خَرَجَ فإذَا كَلْبٌ يَلْهَثُ يأكُلُ الثَّرَى مِنَ العَطَشِ، فَقَالَ الرَّجُلُ: لَقَدْ بَلَغَ هَذَا الكَلْبُ مِنَ العَطَشِ مِثلُ الَّذِي كَانَ قَدْ بَلَغَ مِنِّي فَنَزَلَ البِئْرَ فَمَلأَ خُفَّهُ مَاءً ثُمَّ أمْسَكَهُ بفيهِ حَتَّى رَقِيَ، فَسَقَى الكَلْبَ، فَشَكَرَ الله لَهُ، فَغَفَرَ لَهُ)) قالوا: يَا رَسُول اللهِ، إنَّ لَنَا في البَهَائِمِ أَجْرًا؟ فقَالَ: ((في كُلِّ كَبِدٍ رَطْبَةٍ أجْرٌ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

وفي رواية للبخاري: ((فَشَكَرَ اللهُ لَهُ، فَغَفَرَ لَهُ، فأدْخَلَهُ الجَنَّةَ))

وفي رواية لهما: ((بَيْنَما كَلْبٌ يُطِيفُ بِرَكِيَّةٍ قَدْ كَادَ يقتلُهُ العَطَشُ إِذْ رَأَتْهُ بَغِيٌّ مِنْ بَغَايَا بَنِي إسْرَائِيل، فَنَزَعَتْ مُوقَها فَاسْتَقَتْ لَهُ بِهِ فَسَقَتْهُ فَغُفِرَ لَهَا بِهِ))

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amepokea kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kulikuwa na mtu aliyekuwa akitembea njiani, akashikwa na kiu, akaona kisima. Akateremka ndani na akanywa maji, kisha akatoka, mara akamuona mbwa ana hema anakula mchanga kwa sababu ya kiu. Yule mtu akasema: Mbwa huyu amepatwa na kiu kama kile kilichonipata. Akateremka kisimani, akaijaza maji khuffu yake halafu akaizuia kwenye mdomo wake, akapanda hata akafika juu, akamnywesha mbwa yule. Allaah Akamlipa na Akamghufuria.” Maswahaba wakauliza: Kwani sisi tuna ujira katika Wanyama? Akawajibu: “Kunywesha kila kilicho hai ni swadaqah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine ya Al-Bukhaariy imesema: “Allaah Akamlipa, Akamghufuria na Akamuingiza Jannah.”

Riwaayah nyingine ya Al-Bukhaariy na Muslim zimesema: “Mbwa aliokuwa akizunguka kando ya kisima, alikaribia kufa kwa kiu, ghafla akaonekana na mwanamke mmoja wa kikahaba katika wana wa Israiyl, akaivua khuffu yake, akachotea maji na akamnywesha, akaghufuriwa kwa kitendo hicho.”

 

 

Hadiyth – 11

 

عَنْهُ، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((لَقدْ رَأيْتُ رَجُلًا يَتَقَلَّبُ في الجَنَّةِ في شَجَرَةٍ قَطَعَهَا مِنْ ظَهْرِ الطَرِيقِ كَانَتْ تُؤذِي المُسْلِمِينَ)). رواه مسلم.

وفي رواية: ((مَرَّ رَجُلٌ بِغُصْنِ شَجَرَةٍ عَلَى ظَهرِ طَرِيقٍ، فَقَالَ: وَاللهِ لأُنْحِيَنَّ هَذَا عَنِ المُسْلِمينَ لا يُؤذِيهِمْ، فَأُدخِلَ الجَنَّةَ)).

وفي رواية لهما: ((بَيْنَمَا رَجُلٌ يَمْشي بِطَريقٍ وَجَدَ غُصْنَ شَوكٍ عَلَى الطريقِ فأخَّرَه فَشَكَرَ اللهُ لَهُ، فَغَفَرَ لَهُ))

 

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amepokea kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kwa hakika nilimuona mtu akitembea Jannah kwa sababu ya mti alioukata katikati ya njia uliokuwa ukiwaudhi Waislaamu.” [Muslim]

Riwaayah nyingine inasema: “Mtu mmoja alipita katikati ya tawi la mti uliokuwa katikati ya njia, akasema: Wa-Allaahi nitaliondoa tawi hili lisiwaudhi Waislaamu. Akaingizwa Jannah.”

Riwaayah nyingine ya Al-Bukhaariy na Muslim imesema: “Mtu mmoja alipokuwa akitembea njiani, akakuta tawi la mtu wenye miba njiani, akaliweka nyuma. Allaah Akamjazi na Akamghufuria.”

 

 

Hadiyth – 12

 

عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ تَوَضَّأَ فَأَحْسَنَ الوُضُوءَ، ثُمَّ أَتَى الجُمعَةَ فَاسْتَمَعَ وَأنْصَتَ غُفِرَ لَهُ مَا بَيْنَهُ وَبَيْن الجُمُعَةِ وَزِيادَةُ ثَلاثَةِ أيَّامٍ، وَمَنْ مَسَّ الحَصَا فَقَدْ لَغَا)). رواه مسلم

 

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayetawadha vizuri kisha akaenda katika Swalaah ya Ijumaa, akasikiliza Khutbah na akanyamaza; ataghufuriwa baina ya Ijumaa hiyo na Ijumaa nyingine na ziada ya siku tatu, na atakayepangusa kwa vijiwe ameshafanya upuuzi.” [Muslim]

 

 

Hadiyh – 13

 

عَنْهُ: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إِذَا تَوَضَّأ العَبْدُ المُسْلِمُ، أَو المُؤمِنُ فَغَسَلَ وَجْهَهُ خَرَجَ مِنْ وَجْهِهِ كُلُّ خَطِيئَةٍ نَظَرَ إِلَيْهَا بِعَينهِ مَعَ المَاءِ، أَوْ مَعَ آخِرِ قَطْرِ المَاءِ، فَإِذا غَسَلَ يَدَيْهِ خَرَجَ مِنْ يَدَيهِ كُلُّ خَطِيئَة كَانَ بَطَشَتْهَا يَدَاهُ مَعَ المَاءِ، أَوْ مَعَ آخِرِ قَطْرِ المَاءِ، فَإِذَا غَسَلَ رِجْلَيهِ خَرَجَتْ كُلُّ خَطِيئَةٍ مشتها رِجْلاَهُ مَعَ المَاء أَوْ مَعَ آخِرِ قَطْرِ المَاءِ حَتَّى يَخْرُجَ نَقِيًّا مِنَ الذُّنُوبِ)). رواه مسلم

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amepokea kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mja Muislaam au Muumin anapotawadha akaosha uso wake, litatoka katika uso wake kila dhambi alilolitazama kwa jicho lake pamoja na maji au pamoja na tone la mwisho la maji. Atakapoosha mikono yake, litatoka kila dhambi alilolishika kwa mikono yake pamoja na maji au pamoja na tone la mwisho la maji. Atakapoiosha miguu yake, itatoka kila dhambi aliyoiendea kwa miguu yake pamoja na maji au tone la mwisho la maji, mpaka atoke hali ya kuwa ni msafi na hana dhambi.” [Muslim]

 

 

Hadiyth - 14

 

عَنْهُ، عن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((الصَّلَوَاتُ الخَمْسُ، وَالجُمُعَةُ إِلَى الجُمُعَةِ، وَرَمَضَانُ إِلَى رَمَضَانَ مُكَفِّراتٌ لِمَا بَيْنَهُنَّ إِذَا اجْتُنِبَتِ الكَبَائِرُ)). رواه مسلم

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Swalaah tano. Ijumaa mpaka Ijumaa, na Ramadhwaan mpaka Ramadhwaan ni yenye kufuta (madhambi) yaliyo baina yake pindi yatakapoepukwa al-kabaair (madhambi makubwa).” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 15

 

عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((ألا أَدُلُّكُمْ عَلَى مَا يَمْحُو اللهُ بِهِ الخَطَايَا وَيَرْفَعُ بِهِ الدَّرَجَاتِ؟)) قَالُوا: بَلَى، يَا رسولَ اللهِ، قَالَ: ((إِسْبَاغُ الوُضُوءِ عَلَى المَكَارِهِ، وَكَثْرَةُ الخُطَا إِلَى المَسَاجِدِ، وَانْتِظَارُ الصَّلاةِ بَعْدَ الصَّلاةِ فَذلِكُمُ الرِّبَاطُ)). رواه مسلم

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Jee, niwajulishe jambo ambalo Allaah Hufuta dhambi kwa sababu yake na Hupandisha daraja kwa sababu yake?” Wakasema: Tujulishe Ee Rasuli wa Allaah. Akawaambia: “Kutawadha vizuri wakati wa kuona karaha, kwenda hatua nyingi Masjid na kuingojea Swalaah baada ya Swalaah. Basi kufanya hayo ndio ar-ribaatwh (kujifunga katika njia ya Allaah).” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 16

 

عن أبي موسى الأشعرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ صَلَّى البَرْدَيْنِ دَخَلَ الجَنَّةَ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Abuu Muwsaa Al-Ash’ariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayeswali al-bardayni (Swalaah ya Al-Fajr na Al-‘Aswr) ataingia Jannah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 17

 

عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((إِذَا مَرِضَ العَبْدُ أَوْ سَافَرَ كُتِبَ لَهُ مِثْلُ مَا كَانَ يَعْمَلُ مُقِيمًا صَحِيحًا)). رواه البخاري

Abuu Muwsaa Al- Ash’ariy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mja atakapougua au akasafiri, ataandikiwa mfano wa aliyokuwa akiyatenda alipokuwa nyumbani na alipokuwa mzima.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 18

 

عن جَابرٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((كُلُّ مَعْرُوفٍ صَدَقَةٌ)) رواه البخاري، ورواه مسلم

Jaabir (Radhwiya Allaahhu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kila kitendo chema ni swadaqah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 19

 

عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَغْرِسُ غَرْسًا إلا كَانَ مَا أُكِلَ مِنْهُ لَهُ صَدَقَةً، وَمَا سُرِقَ مِنهُ لَهُ صَدَقَةً، وَلا يَرْزَؤُهُ أَحَدٌ إلا كَانَ لَهُ صَدَقَةً)). رواه مسلم

Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Muislamu yeyote atakayepandikiza mti basi chochote kitakacholiwa katika mti huo ni swadaqah yake, na kitakachoibiwa ni swadaqah yake, na chochote kitakachopunguza itakuwa ni swadaqah yake.” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 20

 

عَنْهُ، قَالَ: أراد بنو سَلِمَةَ أَن يَنتقِلوا قرب المسجِدِ فبلغ ذلِكَ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ لهم: ((إنَّهُ قَدْ بَلَغَني أنَّكُمْ تُرِيدُونَ أنْ تَنتَقِلُوا قُربَ المَسجِد؟)) فقالُوا: نَعَمْ، يَا رَسُول اللهِ قَدْ أَرَدْنَا ذلِكَ. فَقَالَ: ((بَنِي سَلِمَةَ، دِيَارَكُمْ تُكْتَبْ آثَارُكُمْ، ديَارَكُمْ تُكْتَبْ آثَارُكُمْ)). رواه مسلم

وفي روايةٍ: ((إنَّ بِكُلِّ خَطوَةٍ دَرَجَةً)). رواه مسلم

Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: Watu wa kabila la Banu Salamah walitaka kuhamia karibu na Masjid. Habari hiyo ilimfikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Akawauliza: “Nimesikia kuwa mnataka kuhamia karibu na Masjid.” Wakajibu: Ndio Ee Rasuli wa Allaah, tumetaka kufanya hivyo. Akawaambia: “Enyi Banu Salamah, kaeni huko huko majumbani mwenu (msihame), hatua zenu zinaandikwa, kaeni huko huko hatua zenu zinaandikwa.” [Muslim]

Riwaayah nyingine imesema: “Hakika katika kila hatua kuna daraja.” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 21

 

عن أبي المنذِر أُبيِّ بنِ كَعْب رضي الله عنه، قَالَ: كَانَ رَجُلٌ لا أعْلَمُ رَجلًا أبْعَدَ مِنَ المَسْجِدِ مِنْهُ، وَكَانَ لا تُخْطِئُهُ صَلاةٌ، فَقيلَ لَهُ أَوْ فَقُلْتُ لَهُ: لَوِ اشْتَرَيْتَ حِمَارًا تَرْكَبُهُ في الظَلْمَاء وفي الرَّمْضَاء؟ فَقَالَ: مَا يَسُرُّنِي أنَّ مَنْزِلي إِلَى جَنْبِ المَسْجِدِ إنِّي أريدُ أنْ يُكْتَبَ لِي مَمشَايَ إِلَى المَسْجِدِ وَرُجُوعِي إِذَا رَجَعْتُ إِلَى أهْلِي فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((قَدْ جَمَعَ اللهُ لَكَ ذلِكَ كُلَّهُ)). رواه مسلم

وفي رواية: ((إنَّ لَكَ مَا احْتَسَبْتَ))

Abuu Al-Mundhir, Ubayy bin Ka’b (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Alikuwepo mtu mmoja, sijui kama kuna mwengine aliyekuwa anaishi mbali zaidi na Masjid kulikoni mtu huyo, alikuwa hapitwi na Swalaah yoyote. Akaulizwa au nikamuuliza: Waonaje lau ungalinunua punda wakati wa giza na wakati mchanga ukiwa umepata joto? Akajibu: Sipendelei nyumba yangu iwepo karibu na Masjid, mimi nataka niandikiwe hatua zangu za kwenda Masjid na kurejea kwangu kwa familia yangu.” Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Allaah Ameshakujumuishia yote.” [Muslim]

Riwaayah nyingine imesema: “Umeshapata ulilotarajia.”

 

 

Hadiyth – 22

 

عن أبي محمد عبدِ اللهِ بنِ عمرو بن العاصِ- رَضي الله عنهما، قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((أرْبَعُونَ خَصْلَةً: أعْلاَهَا مَنيحَةُ العَنْزِ، مَا مِنْ عَامِلٍ يَعْمَلُ بِخَصْلَة مِنْهَا؛ رَجَاءَ ثَوَابِهَا وتَصْدِيقَ مَوْعُودِهَا، إلا أدْخَلَهُ اللهُ بِهَا الجَنَّةَ)). رواه البخاري

Abuu Muhammad, ‘Abdullaah bin ‘Amruw bin ‘Aasw (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kuna mambo arubaini ya wema, la juu kabisa ni mtu akopeshe mbuzi wake. Hakuna yeyote atakayetenda mojawapo katika hayo kwa kutarajia thawabu zake na kusadikisha miadi yake, isipokuwa Allaah Atamuingiza Jannah.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 23

 

عن عَدِي بنِ حَاتمٍ رضي الله عنه قَالَ: سمعت النَّبيّ صلى الله عليه وسلم يقول: ((اتَّقُوا النَّارَ وَلَوْ بشقِّ تَمْرَةٍ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

وفي رواية لهما عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ إلا سَيُكَلِّمُهُ رَبُّهُ لَيْسَ بَينَهُ وَبَيْنَهُ تَرْجُمَانٌ، فَيَنْظُرُ أَيْمَنَ مِنْهُ فَلا يَرَى إلا مَا قَدَّمَ، وَيَنْظُرُ أَشْأَمَ مِنْهُ فَلا يَرى إلا مَا قَدَّمَ، وَيَنظُرُ بَيْنَ يَدَيهِ فَلا يَرَى إلا النَّار تِلقَاءَ وَجْهِهِ، فَاتَّقُوا النَّارَ وَلَو بِشِقِّ تَمْرَةٍ، فَمَنْ لَمْ يَجِدْ فَبِكَلِمَةٍ طَيِّبَةٍ))

Abuu ‘Adiyy bin Haatim (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nilimsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Jikingeni na moto japo kwa kutoa kipande cha tende.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine ya Al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwake (‘Adiyy) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kila mmoja wenu atazungumza na Rabb wake wala hakuna mwenye kutarjam baina yake na Rabb wake. Atatazama kuliani mwake, hataona ila alichotenda, atatazama kushotoni mwake, hataona ila alichotenda, atatazama mbele yake, hataona ila moto mbele yake. Basi ogopeni moto japo kwa kutoa kipande cha tende. Asiepata, azungumze neno jema.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 24

 

عن أنس رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((إنَّ اللهَ لَيَرْضَى عَنِ العَبْدِ أنْ يَأكُلَ الأَكْلَةَ، فَيَحمَدَهُ عَلَيْهَا، أَوْ يَشْرَبَ الشَّرْبَةَ، فَيَحْمَدَهُ عَلَيْهَا)). رواه مسلم

Anas (Radhwiya Allaahu ‘amhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Humridhia mja anapokula chakula kimoja, Humhimidi Allaah kwa kukila, au anapokunya funda moja la maji Humhimidi Allaah kwa kunywa hicho kinywaji.” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 25

 

عن أَبي موسى رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((عَلَى كلّ مُسْلِمٍ صَدَقَةٌ)) قَالَ: أرأيتَ إنْ لَمْ يَجِدْ؟ قَالَ: ((يَعْمَلُ بِيَدَيْهِ فَيَنْفَعُ نَفْسَهُ وَيَتَصَدَّقُ)) قَالَ: أرأيتَ إن لَمْ يَسْتَطِعْ؟ قَالَ: ((يُعِينُ ذَا الحَاجَةِ المَلْهُوفَ)) قَالَ: أرأيتَ إنْ لَمْ يَسْتَطِعْ، قَالَ: ((يَأمُرُ بِالمعْرُوفِ أوِ الخَيْرِ)) قَالَ: أرَأيْتَ إنْ لَمْ يَفْعَلْ؟ قَالَ: ((يُمْسِكُ عَنِ الشَّرِّ، فَإِنَّهَا صَدَقَةٌ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Abuu Muwsaa (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amepokea Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Kila Muislamu inampasa kutoa swadaqah.” Maswahaba wakamuuliza: Je itakuwaje asipopata cha kutoa? Akajibu: “Afanye kazi kwa mikono yake ajinufaishe na atoe swadaqah.” Akauliza: Jee, asipoweza? Akamwambia: “Atamsaidia mwenye haja anayesononeka.” Akamuuliza: Jee, asipoweza? Akajibu: “Ataamrisha wema.” Akauliza: Jee, asipofanya? Akamjibu: “Atajizuia kutenda shari, kwani huko pia ni kutoa swadaqah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Share