014-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Iktisadi Katika Twaa-ah (‘Ibaadah)

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب الاقتصاد في الطَّاعَة

14 - Mlango Wa Iktisadi Katika Twaa-ah (‘Ibaadah)

 

Alhidaaya.com

 

 قَالَ الله تَعَالَى:

 

مَا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْقُرْآنَ لِتَشْقَىٰ ﴿٢﴾

Hatukukuteremshia Qur-aan ili upate mashaka. [Twaahaa: 2]

 

يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ ﴿١٨٥﴾

Allaah Anakutakieni mepesi na wala Hakutakieni magumu. [Al-Baqarah: 185]

 

 

Hadiyth – 1

عن عائشة رضي الله عنها: أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم دخل عَلَيْهَا وعِندها امرأةٌ، قَالَ: ((مَنْ هذِهِ؟)) قَالَتْ: هذِهِ فُلاَنَةٌ تَذْكُرُ مِنْ صَلاتِهَا. قَالَ: ((مهْ، عَلَيْكُمْ بِمَا تُطِيقُونَ، فَواللهِ لا يَمَلُّ اللهُ حَتَّى تَمَلُّوا، وكَانَ أَحَبُّ الدِّينِ إِلَيْهِ مَا دَاوَمَ صَاحِبُهُ عَلَيهِ)) مُتَّفَقٌ عَلَيه

Kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia kwake wakati alikuweko mwanamke. Akauliza: “Ni nani huyu?” Akamwambia: Huyu ni mtu fulani anayetajwa kusifiwa kwa Swalaah zake. Akasema: “Wacheni hayo! Fanyeni mnayoweza, wa-Allaahi, Allaah Hachoki kuwaandikia thawabu zenu mpaka mtakapochoka nyinyi wenyewe (kufanya ‘ibaadah). Na ‘amali bora kabisa mbele ya Allaah ni ile anayodumu nayo mwenye kuifanya.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أنس رضي الله عنه قَالَ: جَاءَ ثَلاثَةُ رَهْطٍ إِلَى بُيُوتِ أزْوَاجِ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، يَسْأَلُونَ عَنْ عِبَادَةِ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم فَلَمَّا أُخْبِروا كَأَنَّهُمْ تَقَالُّوهَا وَقَالُوا: أَيْنَ نَحْنُ مِنَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم قدْ غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ وَمَا تَأخَّرَ. قَالَ أحدُهُم: أمَّا أنا فَأُصَلِّي اللَّيلَ أبدًا. وَقالَ الآخَرُ: وَأَنَا أصُومُ الدَّهْرَ وَلا أُفْطِرُ. وَقالَ الآخر: وَأَنا أعْتَزِلُ النِّسَاءَ فَلا أتَزَوَّجُ أبَدًا. فجاء رسولُ الله صلى الله عليه وسلم إليهم، فَقَالَ: ((أنْتُمُ الَّذِينَ قُلْتُمْ كَذَا وَكَذَا؟ أَمَا واللهِ إنِّي لأخْشَاكُمْ للهِ، وَأَتْقَاكُمْ لَهُ، لَكِنِّي أصُومُ وَأُفْطِرُ، وأُصَلِّي وَأَرْقُدُ، وَأَتَزَوَّجُ النِّساءَ، فَمَنْ رَغِبَ عَنْ سُنَّتِي فَلَيْسَ مِنِّي)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Imepokelewa na Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba kundi la watu watatu lilikuja katika nyumba za wake wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakiuliza kuhusu ‘ibaadah za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Walipoelezwa waliziona kama ni kidogo, wakasema: Sisi hatuko sawa na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), yeye ameshaghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia na yatakayokuja. Mmoja wao akasema: Ama mimi, nitaswali daima usiku wote. Mwengine akasema: mimi nitafunga Swawm mwaka mzima. Mwengine akasema: Mimi nitawaepuka wanawake, sitaoa kamwe. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaendea na kuwauliza: “Ninyi ndio mliosema kadhaa na kadhaa? Ama wa-Allaahi mimi ninamkhofu Allaah zaidi ya nina taqwa zaidi kulikoni ninyi; lakini mimi ninafunga swawm na kufungua, ninaswali na ninalala, na pia ninaoa wake. Atakayekengeuka na Sunnah zangu basi si katika mimi.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن ابن مسعود رضي الله عنه: أنّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((هَلَكَ المُتَنَطِّعُونَ)). قالها ثَلاثًا. رواه مسلم

Imepokewa kutoka ‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Wameangamia wenye kushadidia mambo.” Amesema hivyo mara tatu. [Muslim]

 

 

Hadiyth – 4

 

عن أَبي هريرةَ رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إنَّ الدِّينَ يُسْرٌ، وَلَنْ يُشَادَّ الدِّيْنُ إلا غَلَبَهُ، فَسَدِّدُوا وَقَارِبُوا وَأبْشِرُوا، وَاسْتَعِينُوا بِالغَدْوَةِ وَالرَّوْحَةِ وَشَيءٍ مِنَ الدُّلْجَةِ)). رواه البخاري

وفي رواية لَهُ: ((سَدِّدُوا وَقَارِبُوا، وَاغْدُوا وَرُوحُوا، وَشَيءٌ مِنَ الدُّلْجَةِ، القَصْدَ القَصْدَ تَبْلُغُوا))

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika Dini ni nyepesi, wala hakuna atakayetia uzito katika Dini ispokuwa itamshinda, basi fanyeni kwa wastani, na karibieni  katika ukamilifu na toeni bishara njema na ombeni msaada katika nyakati za asubuhi na jioni na baadhi katika nyakati za usiku.” [Al-Bukhaariy]

Riwaayah nyingine ya Al-Bukhaariy imesema: “Karibieni katika ukamilifu, fanyeni wastani, na wahini  nyakati za asubuhi, jioni na baadhi ya nyakati za usiku kwa wastani wastani, mtafikia (malengo).” 

 

 

Hadiyth – 5

 

 وعن أنس رضي الله عنه قَالَ: دَخَلَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم المَسْجِدَ فَإِذَا حَبْلٌ مَمْدُودٌ بَيْنَ السَّارِيَتَيْنِ، فَقَالَ: ((مَا هَذَا الحَبْلُ؟)) قالُوا: هَذَا حَبْلٌ لِزَيْنَبَ، فَإِذَا فَتَرَتْ تَعَلَّقَتْ بِهِ. فَقَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم: ((حُلُّوهُ، لِيُصلِّ أَحَدُكُمْ نَشَاطَهُ فَإِذَا فَتَرَ فَلْيَرْقُدْ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Na amepokea Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia Masjid, akaona kamba imefungwa baina ya nguzo mbili. Akauliza: “Kamba hii ni ya nini?” Wakasema: Hii ni kamba ya Zaynab, anapochoka hujiegemeza kwayo. Basi Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Ifungueni na kila mmoja wenu aswali kwa nguvu zake, atakapochoka alale.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 6

 

وعن عائشة رضي الله عنها: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إِذَا نَعَسَ أَحَدُكُمْ وَهُوَ يُصَلِّي فَلْيَرْقُدْ حَتَّى يَذْهَبَ عَنْهُ النَّومُ، فإِنَّ أحدكم إِذَا صَلَّى وَهُوَ نَاعِسٌ لا يَدْرِي لَعَلَّهُ يَذْهَبُ يَسْتَغْفِرُ فَيَسُبُّ نَفْسَهُ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Na kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Anaposinzia mmoja wenu huku akiwa anaswali, basi alale mpaka usingizi utakapommalizikia kwani mmoja wenu atakaposwali na hali anasinzia, hatofahamu anayoyasema, hivyo huenda akawa anakusudia kuomba maghfirah kumbe anaitukana nafsi yake.” [Al-Bukhariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 7

 

وعن أَبي عبد الله جابر بن سمرة رضي الله عنهما، قَالَ: كُنْتُ أصَلِّي مَعَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم الصَّلَوَاتِ، فَكَانتْ صَلاتُهُ قَصْدًا وَخُطْبَتُهُ قَصْدًا. رواه مسلم

Abuu ‘Abdillaah, Jaabir bin Samurah (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Nilikuwa nikiswali pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baadhi ya Swalaah na ilikuwa Swalaah yake ni ya wastani na khutbah yake ilikuwa ni wastani.” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 8

 

وعن أبي جُحَيْفَة وَهْب بنِ عبد اللهِ رضي الله عنه قَالَ: آخَى النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم بَيْنَ سَلْمَانَ وَأَبي الدَّرْداءِ، فَزارَ سَلْمَانُ أَبَا الدَّرداءِ فَرَأى أُمَّ الدَّرداءِ مُتَبَذِّلَةً، فَقَالَ: مَا شَأنُكِ؟ قَالَتْ: أخُوكَ أَبُو الدَّردَاءِ لَيْسَ لَهُ حَاجَةٌ في الدُّنْيَا، فَجاءَ أَبُو الدَّرْدَاءِ فَصَنَعَ لَهُ طَعَامًا، فَقَالَ لَهُ: كُلْ فَإِنِّي صَائِمٌ، قَالَ: مَا أنا بِآكِلٍ حَتَّى تَأكُلَ فأكل، فَلَمَّا كَانَ اللَّيلُ ذَهَبَ أَبُو الدَّردَاءِ يَقُومُ فَقَالَ لَهُ: نَمْ، فنام، ثُمَّ ذَهَبَ يَقُومُ فَقَالَ لَهُ: نَمْ. فَلَمَّا كَانَ من آخِر اللَّيلِ قَالَ سَلْمَانُ: قُم الآن، فَصَلَّيَا جَمِيعًا فَقَالَ لَهُ سَلْمَانُ: إنَّ لِرَبِّكَ عَلَيْكَ حَقًّا، وَإِنَّ لِنَفْسِكَ عَلَيكَ حَقًّا، وَلأَهْلِكَ عَلَيكَ حَقًّا، فَأعْطِ كُلَّ ذِي حَقٍّ حَقَّهُ، فَأَتَى النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم فَذَكَرَ ذلِكَ لَهُ فَقَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم: ((صَدَقَ سَلْمَانُ)). رواه البخاري

Abuu Juhayfah, Wahb bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alifunga undugu baina ya Salmaan na Abuu Dardaa. Salmaan akaenda kumtembelea Abuu Dardaa, akamuona mama Dardaa amevaa nguo iliyochakaa. Akamuuliza: Mbona upo hivyo? Akasema: Nduguyo Abuu Dardaa hana haja ya dunia (hataki wanawake). Abuu Dardaa akaja, akamtengenezea chakula nduguye (Salmaan) kisha akamwambia: Kula mimi nimefunga swawm. Salmaan akamwambia: Sitokula mpaka uanze wewe kula. Akala. Ulipofika usiku Abuu Dardaa akataka kuanza kuswali (Swalaah ya usiku). Salmaan akamwambia: Lala. Akalala. Ulipofika mwisho wa usiku Salmaan akamwambia sasa amka (uswali). Wakaswali wote. Kisha Salmaan akamwambia: Hakika Rabb wako Ana haki juu yako, na nafsi yako ina haki juu yako, na mkeo na familia yako wana haki juu yako. Kwa hiyo kila mmoja mpe haki yake.  Abuu Dardaa akamuendea Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatajiwa hayo, hapo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Salmaan amepatia” [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 9

 

وعن أَبي محمد عبدِ اللهِ بنِ عَمْرو بن العاصِ رضي الله عنهما، قَالَ: أُخْبرَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم أنِّي أقُولُ: وَاللهِ لأَصُومَنَّ النَّهَارَ، وَلأَقُومَنَّ اللَّيلَ مَا عِشْتُ. فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((أنتَ الَّذِي تَقُولُ ذلِكَ؟)) فَقُلْتُ لَهُ: قَدْ قُلْتُهُ بأبي أنْتَ وأمِّي يَا رسولَ الله. قَالَ: ((فَإِنَّكَ لا تَسْتَطِيعُ ذلِكَ فَصُمْ وَأَفْطِرْ، وَنَمْ وَقُمْ، وَصُمْ مِنَ الشَّهْرِ ثَلاثةَ أيَّامٍ، فإنَّ الحَسَنَةَ بِعَشْرِ أمْثَالِهَا وَذَلكَ مِثلُ صِيامِ الدَّهْرِ)) قُلْتُ: فَإِنِّي أُطيقُ أَفْضَلَ مِنْ ذلِكَ، قَالَ: ((فَصُمْ يَومًا وَأَفْطِرْ يَوْمَيْنِ)) قُلْتُ: فَإنِّي أُطِيقُ أفضَلَ مِنْ ذلِكَ، قَالَ: ((فَصُمْ يَومًا وَأفْطِرْ يَومًا فَذلِكَ صِيَامُ دَاوُد صلى الله عليه وسلم، وَهُوَ أعْدَلُ الصيامِ))

  وفي رواية: ((هُوَ أفْضَلُ الصِّيامِ)) فَقُلْتُ: فَإِنِّي أُطيقُ أفْضَلَ مِنْ ذلِكَ، فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((لا أفضَلَ مِنْ ذلِكَ))، قال: وَلأنْ أكُونَ قَبِلْتُ الثَّلاثَةَ الأَيّامِ الَّتي قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم أحَبُّ إليَّ مِنْ أهْلي وَمَالي

وفي رواية: ((أَلَمْ أُخْبَرْ أنَّكَ تَصُومُ النَّهَارَ وتَقُومُ اللَّيلَ؟)) قُلْتُ: بَلَى، يَا رَسُول الله، قَالَ: ((فَلا تَفْعَلْ: صُمْ وَأَفْطِرْ، وَنَمْ وَقُمْ؛ فإنَّ لِجَسَدِكَ عَلَيْكَ حَقًّا، وَإِنَّ لِعَيْنَيكَ عَلَيْكَ حَقًّا، وَإِنَّ لِزَوْجِكَ عَلَيْكَ حَقًّا، وَإِنَّ لِزَوْرِكَ عَلَيْكَ حَقًّا، وَإنَّ بِحَسْبِكَ أنْ تَصُومَ في كُلِّ شَهْرٍ ثَلاثَةَ أيَّامٍ، فإنَّ لَكَ بِكُلِّ حَسَنَةٍ عَشْرَ أمْثَالِهَا، فَإِنَّ ذلِكَ صِيَامُ الدَّهْر)) فَشَدَّدْتُ فَشُدِّدَ عَلَيَّ، قُلْتُ: يَا رَسُول الله، إنِّي أجِدُ قُوَّةً، قَالَ: ((صُمْ صِيَامَ نَبيِّ الله دَاوُد وَلا تَزد عَلَيهِ)) قُلْتُ: وَمَا كَانَ صِيَامُ دَاوُد؟ قَالَ: ((نِصْفُ الدَّهْرِ)) فَكَانَ عَبدُ الله يقول بَعدَمَا كَبِرَ: يَا لَيتَنِي قَبِلْتُ رُخْصَة رَسُول الله صلى الله عليه وسلم.

   وفي رواية: ((أَلَمْ أُخْبَرْ أَنَّكَ تَصُومُ الدَّهرَ، وَتَقْرَأُ القُرآنَ كُلَّ لَيْلَة؟)) فقلت: بَلَى، يَا رَسُول الله، وَلَمْ أُرِدْ بذلِكَ إلا الخَيرَ، قَالَ: ((فَصُمْ صَومَ نَبيِّ اللهِ دَاوُد، فَإنَّهُ كَانَ أعْبَدَ النَّاسِ، وَاقْرَأ القُرْآنَ في كُلِّ شَهْر)) قُلْتُ: يَا نَبيَّ اللهِ، إنِّي أُطِيقُ أَفْضَلَ مِنْ ذلِكَ؟ قَالَ: ((فاقرأه في كل عشرين)) قُلْتُ: يَا نبي الله، إني أطيق أفضل من ذلِكَ؟ قَالَ: ((فَاقْرَأهُ في كُلِّ عَشْر)) قُلْتُ: يَا نبي اللهِ، إنِّي أُطيقُ أَفْضَلَ مِنْ ذلِكَ؟ قَالَ: ((فاقْرَأهُ في كُلِّ سَبْعٍ وَلا تَزِدْ عَلَى ذلِكَ)) فشدَّدْتُ فَشُدِّدَ عَلَيَّ وَقالَ لي النَّبيّ صلى الله عليه وسلم: ((إنَّكَ لا تَدرِي لَعَلَّكَ يَطُولُ بِكَ عُمُرٌ)) قَالَ: فَصِرْتُ إِلَى الَّذِي قَالَ لي النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم. فَلَمَّا كَبِرْتُ وَدِدْتُ أنِّي كُنْتُ قَبِلتُ رُخْصَةَ نَبيِّ الله صلى الله عليه وسلم.

وفي رواية: ((وَإِنَّ لِوَلَدِكَ عَلَيْكَ حَقًّا))

وفي رواية: ((لا صَامَ مَنْ صَامَ الأَبَدَ)) ثلاثً

وفي رواية: ((أَحَبُّ الصِيَامِ إِلَى اللهِ تَعَالَى صِيَامُ دَاوُد، وَأَحَبُّ الصَّلاةِ إِلَى اللهِ تَعَالَى صَلاةُ دَاوُدَ: كَانَ ينام نصف الليل، ويقوم ثلثه، وينام سدسه، وكان يصوم يومًا ويفطر يومًا، وَلا يَفِرُّ إِذَا لاقَى))

وفي رواية قال: أنْكَحَني أَبي امرَأةً ذَاتَ حَسَبٍ وَكَانَ يَتَعَاهَدُ كنَّتَهُ-- أي: امْرَأَةَ وَلَدِهِ- فَيَسْأَلُهَا عَنْ بَعْلِهَا. فَتقُولُ لَهُ: نِعْمَ الرَّجُلُ مِنْ رَجُلٍ لَمْ يَطَأْ لَنَا فِرَاشًا، وَلَمْ يُفَتِّشْ لَنَا كَنَفًا مُنْذُ أتَيْنَاهُ. فَلَمَّا طَالَ ذلِكَ عَلَيهِ ذَكَرَ ذلك للنَّبيِّ صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ: ((القِنِي بِهِ)) فَلَقيتُهُ بَعد ذلك، فَقَالَ: ((كَيْفَ تَصُومُ؟)) قُلْتُ: كُلَّ يَومٍ، قَالَ: ((وَكَيْفَ تَخْتِمُ؟)) قُلْتُ: كُلَّ لَيْلَةٍ، وَذَكَرَ نَحْوَ مَا سَبَقَ، وَكَانَ يَقْرَأُ عَلَى بَعْضِ أهْلِهِ السُّبُعَ الَّذِي يَقْرَؤُهُ، يَعْرِضُهُ مِنَ النَّهَارِ ليَكُونَ أخفّ عَلَيهِ باللَّيلِ، وَإِذَا أَرَادَ أنْ يَتَقَوَّى أفْطَرَ أيَّامًا وَأحْصَى وَصَامَ مِثْلَهُنَّ كرَاهِيَةَ أنْ يَترُكَ شَيئًا فَارَقَ عَلَيهِ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم

 

Abuu Muhammad, ‘Abdillaah bin ‘Amruw bin Al-‘Aasw  (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliaambiwa kuwa mimi nasema: Wa-Allaahi nitafunga swawm mchana na nitaswali usiku maisha yangu yote. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaniuliza: “Wewe ndiye uliyesema hivyo?” Nikamjibu:  Ndiyo, hakika nimesema, nakutolee fidia baba yangu na mama yangu ee Rasuli wa Allaah. Akaniambia: “Wewe hutaweza kufanya hivyo, kwa hivyo funga swawm na ule, lala na uswali, na ufunge swawm siku tatu kila mwezi; kwani jema moja hulipwa kwa mema kumi mfano wake, na hiyo ni kama swiyaam ya dahari!” Nikamwambia: Mimi naweza kufanya zaidi ya hivyo. Akaniambia: “Basi funga swawm siku moja na ule siku mbili.” Nikamwambia: Mimi naweza zaidi ya hivyo. Akanambia: “Basi funga swawm siku moja na ule siku moja, hivyo ni swiyaam ya  Nabiy Daawuwd (‘Alayhis Salaam) nayo ndio Swawm ya wastani zaidi.”

Riwaayah nyingine imesema: “Hiyo ndiyo Swawm bora zaidi.” Nikamwambia: Mimi naweza zaidi ya hivyo. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: “Hakuna bora zaidi ya hivyo.” Kwa kweli lau ningelikubali zile siku tatu alizonipa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ingelipendeza kwangu zaidi kulikoni familia yangu na mali yangu.

Riwaayah nyingine imesema: “Si niliambiwa kuwa wewe unafunga swawm mchana na usiku wote unaswali?” Nikamjibu: Ndiyo ee Rasuli wa Allaah. Akaniambia: “Usifanye hivyo, funga swawm na ule, lala na uswali, hakika mwili wako una haki juu yako, na macho yako yana haki juu yako, na mkeo ana haki juu yako na mgeni wako ana haki juu yako, na hakika inakutosha ufunge swawm siku tatu kila mwezi; kwani katika kila jambo jema moja unapata mema kumi mfano wake; huko ndiyo swiyaam ya dahari!” Nikamkazania, nami nikakaziwa. Nikamwambia: Ee Rasuli wa Allaah, nina nguvu zaidi. Akanambia: “Funga Swawm ya Nabiy Daawuwd wala usizidishe juu ya hapo.” Nikamuuliza: Swawm ya Nabiy Daawuwd ilikuwaje? Akaniambia: “Nusu ya dahari.”

‘Abdullaah alipozeeka alikuwa akisema: Laiti kama ningelikubali ruhusa ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

Riwaayah nyingine imesema: “Si niliambiwa kuwa unafunga swawm dahari na unasoma Qur-aan yote kila usiku?” Nikamjibu: Ndiyo ee Rasuli wa Allaah, wala sijakusudia kufanya hivyo ila ni khayr tu. Akaniambia: “Funga Swawm ya Nabiy Daawuwd; kwani yeye aliwashinda watu kwa ‘ibaadah, na soma (ukhitimishe) Qur-aan kila mwezi.” Nikamwambia: Ee Rasuli wa Allaah, mimi naweza zaidi ya hivyo. Akaniambia: “Soma kwa siku ishirini.” Nikamwambia: Ee Nabiy wa Allaah, mimi naweza zaidi ya hivyo. Akaniambia: “Soma kwa siku kumi.” Nikamwambia: Ee Nabiy wa Allaah, mimi naweza zaidi ya hivyo. Akaniambia: “Soma umalize kila baada ya siku saba, wala usizidishe uchache wa hapo.” Nikatia mkazo nami nikakaziwa. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: “Huwezi kujua pengine unaweza kuwa na umri mrefu.” Na kweli nikawa kama alivyoniambia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

Riwaayah nyingine imesema: “Na hakika mwanao ana haki juu yako.”

Na Riwaayah nyengine: “Hana Swawm mwenye kufunga daima.” Alikariri mara tatu.

Riwaayah nyingine imesema: “Swawm ipendezayo zaidi kwa Allaah ni Swawm ya Nabiy Daawuwd. Na Swalaah ipendezayo zaidi kwa Allaah ni Swalaah ya Nabiy Daawuwd; alikuwa akilala nusu ya usiku, akiswali thuluthi yake, akilala sudusi yake, na alikuwa akifunga swawm siku moja na akila siku moja, wala hakimbii anapokutana na adaui (vitani).”

Riwaayah nyingine imesema: Baba yangu alinioza mke mwenye nasaba nzuri, na alikuwa akimjulia hali mkwewe, akamuuliza hali ya mumewe, naye akimwambia: Mtu mzuri miongoni mwa watu.  Kuanzia anioe, hakuja kulala na mimi wala kujamiiana nami. Hali hii ilipoendelea kwa muda mrefu, alitajiwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Akasema: “Nileteeni kwangu”. Nami nikamuendea. Akaniuliza: “Unafunga swawm vipi?”  Nikamjibu: Kila siku. Akaniuliza: “Unahitimisha vipi Qur-aan?” Nikamjibu: Kila usiku. Akataja Hadiyth ambayo imetangulia kuelezwa.  

‘Abdullaah alikuwa akisoma kwa baadhi ya familia yake subu’ anayoisoma (yaani alikuwa akihitimisha kwa siku saba), akiisoma mchana ili apate tahfifu wakati wa usiku. Na anapotaka tahfifu kwa kufunga swawm kila siku alikuwa anaacha kufunga swawm baadhi ya siku  na baadaye kuzilipa. Anafanya hivyo kwa kuchelea asije kuacha mazoea aliyokuwa nayo mpaka wakati Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anafariki. 

 

 

Hadiyth – 10

 

وعن أبي رِبعِي حنظلة بنِ الربيعِ الأُسَيِّدِيِّ الكاتب أحدِ كتّاب رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: لَقِيَنِي أَبُو بَكر رضي الله عنه فَقَالَ: كَيْفَ أنْتَ يَا حنْظَلَةُ؟ قُلْتُ: نَافَقَ حَنْظَلَةُ! قَالَ: سُبْحَانَ الله مَا تَقُولُ؟! قُلْتُ: نَكُونُ عِنْدَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يُذَكِّرُنَا بالجَنَّةِ وَالنَّارِ كأنَّا رَأيَ عَيْنٍ فإِذَا خَرَجْنَا مِنْ عِنْدِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم عَافَسْنَا الأَزْواجَ وَالأَوْلاَدَ وَالضَّيْعَاتِ نَسينَا كَثِيرًا، قَالَ أَبُو بكر رضي الله عنه: فَوَالله إنَّا لَنَلْقَى مِثْلَ هَذَا، فانْطَلَقْتُ أَنَا وأبُو بَكْر حَتَّى دَخَلْنَا عَلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم. فقُلْتُ: نَافَقَ حَنْظَلَةُ يَا رَسُول اللهِ! فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((وَمَا ذَاكَ؟)) قُلْتُ: يَا رَسُول اللهِ، نَكُونُ عِنْدَكَ تُذَكِّرُنَا بِالنَّارِ والجَنَّةِ كأنَّا رَأيَ العَيْن فإِذَا خَرَجْنَا مِنْ عِنْدِكَ عَافَسْنَا الأَزْواجَ وَالأَوْلاَدَ وَالضَّيْعَاتِ نَسينَا كَثِيرًا. فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((وَالَّذِي نَفْسي بِيَدِهِ، لَوْ تَدُومُونَ عَلَى مَا تَكُونونَ عِنْدِي، وَفي الذِّكْر، لصَافَحَتْكُمُ الملائِكَةُ عَلَى فُرُشِكُمْ وَفي طُرُقِكُمْ، وَلَكِنْ يَا حَنْظَلَةُ سَاعَةً وسَاعَةً)) ثَلاَثَ مَرَات. رواه مسلم

Abuu Rabi’y, Handhwalah bin Ar-Rabiy’ Al-Usayyidiy ambaye ni mmoja katika waandishi wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesimulia: “Siku moja Abuu Bakr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alikutana nami, akaniuliza: Vipi hali ee Handhwalah? Nikamwambia: “Handhwalah anajikhofia unafiki! Akasema: Subhaana Allaah! Umesema nini? Nikamwambia: Sisi huwa tupo mbele ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akitukumbusha Jannah na moto kana kwamba huwa tukiziona. Lakini tunapoondoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hushughulika na wake zetu na watoto wetu na shughuli za kuendesha maisha yetu, hivyo hutufanya tusahau mengi. Abuu Bakr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akasema: Wa-Allaahi nasi pia hukutana na hali kama hii. Mimi na Abuu Bakr tukaenda kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nikamwambia: Handhwalah anajikhofia unafiki ee Rasuli wa Allaah, tunapokuwa kwako unatukumbusha moto na Jannah kana kwamba tunaziona kwa macho, tunapoondoka kwako, hushughulika na wake zetu na watoto wetu na shughuli za kuendesha maisha yetu, hivyo hutufanya tusahau mengi. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Naapa kwa Ambaye nasfi yangu ipo mikononi Mwake, lau mnadumu katika hali mnayokuwa nayo kwangu na katika kumdhukuru Allaah, basi Malaika wangewasalimia nyinyi mnapokuwa vitandani mwenu na njiani. Lakini ee Handhwalah, kuna wakati wa kutekeleza ‘ibaadah na kuna wakati wa kuangalia mambo ya maisha.” Alikariri hivyo mara tatu. [Muslim]

 

 

Hadiyth – 11

 

وعنِ ابن عباس رضي الله عنهما، قَالَ: بينما النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم يخطب إِذَا هُوَ برجلٍ قائم فسأل عَنْهُ، فقالوا: أَبُو إسْرَائيلَ نَذَرَ أنْ يَقُومَ في الشَّمْسِ وَلا يَقْعُدَ، وَلا يَسْتَظِل، وَلا يَتَكَلَّمَ، وَيَصُومَ، فَقَالَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم: ((مُرُوهُ، فَلْيَتَكَلَّمْ، وَلْيَسْتَظِلَّ، وَلْيَقْعُدْ، وَلْيُتِمَّ صَوْمَهُ)). رواه البخاري

‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa ana khutubia, mara akamuona mtu amesimama. Akauliza kuhusu mtu huyo. Akaambiwa kuwa huyo ni Abuu Israaiyl ambaye ameweka nadhiri atasimama katika jua wala hatoki, wala hatajikinga na kivuli, wala hatazungumza na atafunga swawm. Basi Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Mwambieni azungumze, akae kivulini, akae chini na atimize Swawm yake.” [Al-Bukhaariy]   

 

 

Share