015-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuhifadhi ‘Amali

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب المحافظة عَلَى الأعمال

15 - Mlango Wa Kuhifadhi ‘Amali

 

Alhidaaya.com

 

 قَالَ الله تَعَالَى:

 

أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّـهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ ﴿١٦﴾

Je, haujafika wakati kwa walioamini kwamba zinyenyekee nyoyo zao kwa ukumbusho wa Allaah na yale yaliyoteremka ya haki, na wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla, ukawatawilikia muda, kisha zikawa ngumu nyoyo zao? [Al-Hadiyd: 16]

 

وَقَفَّيْنَا بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ وَآتَيْنَاهُ الْإِنجِيلَ وَجَعَلْنَا فِي قُلُوبِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ رَأْفَةً وَرَحْمَةً وَرَهْبَانِيَّةً ابْتَدَعُوهَا مَا كَتَبْنَاهَا عَلَيْهِمْ إِلَّا ابْتِغَاءَ رِضْوَانِ اللَّـهِ فَمَا رَعَوْهَا حَقَّ رِعَايَتِهَا ﴿٢٧﴾

Na Tukamfuatisha ‘Iysaa mwana wa Maryam, na Tukampa Injiyl. Na Tukaweka katika nyoyo za wale waliomfuata upole na rahmah na uruhubani (maisha ya utawa); wameyaanzisha wao wenyewe Hatukuwaandikia hayo juu yao isipokuwa ni kutafuta radhi za Allaah. Lakini hawakuuchunga ipasavyo kuchungwa. [Al-Hadiyd: 27]

 

وَلَا تَكُونُوا كَالَّتِي نَقَضَتْ غَزْلَهَا مِن بَعْدِ قُوَّةٍ أَنكَاثًا ﴿٩٢﴾

Na wala msiwe kama yule mwanamke aliyezongoa uzi wake vipande vipande baada ya (kuusokota na) kuwa mgumu. [An-Nahl: 92]

 

وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ ﴿٩٩﴾

Na mwabudu Rabb wako mpaka ikufikie yakini (mauti). [Al-Hajr: 99]

 

 

Hadiyth – 1

وعن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ نَامَ عَنْ حِزْبهِ مِنَ اللَّيلِ، أَوْ عَنْ شَيءٍ مِنْهُ، فَقَرَأَهُ مَا بَيْنَ صَلاةِ الفَجْرِ وَصَلاةِ الظُّهْرِ، كُتِبَ لَهُ كَأَنَّمَا قَرَأَهُ مِنَ اللَّيلِ)). رواه مسلم

‘Umar bin Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayelala asisome hizbu (nyiradi) yake ya usiku au chochote katika hizbu yake ya usiku au chochote katika hizbu hiyo, halafu akaisoma baina ya Swalaah ya alfajiri na Swalaah ya adhuhuri, ataandikiwa kana kwamba ameisoma usiku.” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن عبد الله بن عَمْرو بن العاص رَضِيَ الله عنهما، قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((يَا عبدَ اللهِ، لا تَكُنْ مِثْلَ فُلان، كَانَ يَقُومُ اللَّيلَ فَتَرَكَ قِيَامَ اللَّيلِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

‘Abdullaah bin ‘Amruw bin Al-‘Aasw (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Aliniambia: “Ee ‘Abdullaah, usiwe kama fulani, alikuwa akiswali usiku na kuacha kuswali usiku.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن عائشة رضي الله عنها، قَالَتْ: كَانَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم إِذَا فَاتَتْهُ الصَّلاةُ مِنَ اللَّيلِ مِنْ وَجَعٍ أَوْ غَيرِهِ، صَلَّى مِنَ النَّهارِ ثنْتَيْ عَشرَةَ رَكْعَةً. رواه مسلم

‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapopitwa na Swalaah ya usiku kwa sababu ya maradhi au jambo lingine,  huswali wakati wa mchana, rakaa kumi na mbili.” [Muslim]

 

 

Share