Imaam Ibn Rajab: Kusherehekea Siku Ambazo Hazimo Katika Shariy’ah Ni Bid’ah
Kusherehekea Siku Ambazo Hazimo Katika Shariy’ah Ni Bid’ah
Imaam Ibn Rajab Al-Hanbaliy
Hakuna Shariy’ah kwa Waislamu kusherehekea siku yoyote ile isipokuwa ambayo imetajwa katika Shariy’ah kuwa ni siku za kusherehekewa.
Na siku ambazo zimewekewa Shariy’ah ni ‘Iydul-Fitwr, na ‘Iydul-Adhwhaa, na masiku ya Tashriyq, na siku ya Ijumaa.
Na ni bid’ah kufanya siku yoyote ile kuwa ni siku ya sherehe siku ambazo hakuna dalili katika Shariy’ah ya kufanya hayo.
[Latwaaif Al-Ma’aarif (228)]