Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Tofauti Baina Ya Rasuli Na Nabiy
Tofauti Baina Ya Rasuli Na Nabiy
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Je, kuna tofuati baina ya Rasuli na Nabiy?
JIBU:
Na’am. Wanavyuoni wanasema kwamba Nabiy ni Allaah Amemfunulia Wahyi wa shariy’ah lakini hakuamrishwa kubalighisha (kufikisha ulinganizi) kwa watu bali afanyie kazi mwenyewe bila ya kulazimika kubalighisha.
Na Rasuli ni ambaye Allaah Amemfunulia Wahyi wa shariy’ah na Akaamrishwa kubalighisha na kufanyia kazi.
Basi kila Rasuli ni Nabiy na si kila Nabiy ni Rasuli.
Na Manabii ni wengi kuliko Rusuli. Allaah Amewasimulia baadhi ya Rusuli katika Qur-aan na wengine hakuwasimulia. Anasema Allaah (Ta’aalaa):
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ مِنْهُم مَّن قَصَصْنَا عَلَيْكَ وَمِنْهُم مَّن لَّمْ نَقْصُصْ عَلَيْكَ ۗ وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأْتِيَ بِآيَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ
Na kwa yakini Tumewapeleka Rusuli kabla yako; miongoni mwao wako Tuliokusimulia na miongoni mwao wako ambao Hatukukusimulia. Na haiwi kwa Rasuli yeyote kuleta Aayah (au ishara) yoyote ile isipokuwa kwa idhini ya Allaah. [Ghaafir 40: 78]
Kutokana na Aayah hii, ni dhahiri kila aliyetajwa katika Qur-aan katika Nabiy basi ni Rasuli.
[Majmuw' Fataawaa wa Rasaail Imaam Muhammad bin Swaalih bin ‘Uthaymin, Mjalada Namba 1 Baab Ar-Rusul]