Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Haijuzu Kuswali Kwa Kumfuata Imaam Kupitia Redio Au Televisheni

 

Haijuzu Kuswali Kwa Kumfuata Imaam Kupitia Redio Au Televisheni

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Haijuzu mtu kumfuata Imaam kupitia redio au televisheni kwa sababu Swalaah ya Jamaa'ah inakusudiwa mkusanyiko, basi hakuna budi iwe katika sehemu moja au kuunganisha safu moja baada ya nyingine.

Wala Swalaah haijuzu kupitia viwili hivyo (redio na televisheni) kwa sababu ya kutopatikana malengo yake. 

Na tungelijuzisha hilo, basi kila mmoja angeliswali nyumbani kwake Swalaah zote tano pamoja na Swalaah ya Ijumaa pia. Na hili linakwenda kinyume na shariy’ah inayohusu Swalaah ya Ijumaa na ya jamaa'ah. 

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/213)]

 

 

Share