Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Sha'baan: Hukmu Ya Kisimamo Cha Usiku Wa Nusu Sha’baan
Hukmu Ya Kisimamo Cha Usiku Wa Nusu Sha’baan
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah) amejibu kuhusu Swali la maudhui ya kisimamo cha usiku wa Nusu Sha’baan:
“Kisimamo cha usiku wa Nusu Sha’baan kiko katika hali au hukmu tatu:
1-Iwe ni ada (desturi) ya mtu kuwa anafanya hivyo (kuamka kwa ajili ya ‘ibaadah) kwa hiyo hufanya hata siku hiyo ya usiku wa Nusu Sha’baan kama anavyofanya nyusiku nyenginezo bila ya kuufanya usiku huo kuwa ni makhsusi kwa kuzidisha ‘ibaadah. Jambo hili hakuna ubaya.
2- Kuswali usiku wa Nusu Sha’baan juu ya kuwa hakuwa mtu akifanya hivyo katika nyusiko nyenginezo. Hii ni bid’ah.
3-Kuswali usiku huo Swalaah zenye idadi maalumu, ambazo anakariri kila mwaka kuziswali. Hii ni bid’ah shadidi (ya nguvu) zaidi kuliko ya hali ya pili na iko mbali zaidi na Sunnah.”
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/28-30)]
