03-Aayah Na Mafunzo: Maana Ya Ar-Rahmaan Na Mwenye Kurehemu

Aayah Na Mafunzo

 

Al-Faatihah

 

Maana Ya Ar-Rahmaan, Mwenye Kurehemu

 

 

 Al-Faatihah Aayah 3:

 

 بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿١﴾

Kwa Jina la Allaah Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.

 

 الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٢﴾

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu.

 

الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿٣﴾

Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.

 

 

Mafunzo:

 

Ar-Rahmaan ni katika Jina la Allaah tukufu na Sifa ya Rahmaan  ni ambayo inawaenea viumbe Vyake vyote duniani; wana Aadam na majini, makafiri na Waumini na makafiri, wenye taqwa na wenye kumuasi, wanyama, mimea na kadhaalika. Hakuna kiumbe chochote isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amekiteremshia rahmah Yake. Amejiita Mwenyewe (Tabaaraka wa Ta’aalaa):

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥﴾

Ar-Rahmaan; Mwingi wa Rahmah juu ya ‘Arshi Istawaa (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah) [Twaahaa 5]

 Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

رَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ

Na rahmah Yangu imeenea kila kitu [Al-A’raaf: 156]

 

Na hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

عَنْ عَطَاءٍ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إِنَّ لِلَّهِ مِائَةَ رَحْمَةٍ أَنْزَلَ مِنْهَا رَحْمَةً وَاحِدَةً بَيْنَ الْجِنِّ وَالإِنْسِ وَالْبَهَائِمِ وَالْهَوَامِّ فَبِهَا يَتَعَاطَفُونَ وَبِهَا يَتَرَاحَمُونَ وَبِهَا تَعْطِفُ الْوَحْشُ عَلَى وَلَدِهَا وَأَخَّرَ اللَّهُ تِسْعًا وَتِسْعِينَ رَحْمَةً يَرْحَمُ بِهَا عِبَادَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ))     

Na pia imepokelewa kutoka kwa ‘Atwaa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah Ana rahmah mia, Ameiteresha moja kati ya majini na wana Aadam na wanyama na wadudu, ambao wanaoneana huruma na wanarehemeana, na hiyo hiyo mpaka mnyama mwitu anamhurumia mwanawe. Akazuia Allaah rahmah tisini na tisa Atawarehemu kwazo waja Wake Siku ya Qiyaamah)) [Muslim (6/98), Ahmad (2/434), Ibn Maajah (4293)]

 

Ama Rahiym ni Sifa inayowastahiki Waumini pekee. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا ﴿٤٣﴾

Naye kwa Waumini daima ni Mwenye kurehemu. [Al-Ahzaab: 43]

 

 Na waja Wake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) watakapoingia Jannah:

 

إِنَّ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ الْيَوْمَ فِي شُغُلٍ فَاكِهُونَ ﴿٥٥﴾

Hakika watu wa Jannah leo wamo katika kushughulika wakifurahi.

 

هُمْ وَأَزْوَاجُهُمْ فِي ظِلَالٍ عَلَى الْأَرَائِكِ مُتَّكِئُونَ ﴿٥٦﴾

Wao na wake zao, wakiwa katika vivuli, juu ya makochi ya fakhari wakiegemea.

 

لَهُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ وَلَهُم مَّا يَدَّعُونَ ﴿٥٧﴾

Watapata humo kila aina ya matunda, na watapata wanavyoomba.

 

سَلَامٌ قَوْلًا مِّن رَّبٍّ رَّحِيمٍ ﴿٥٨﴾

“Salaamun”; kauli kutoka kwa Rabb Mwenye kurehemu. [Yaasiyn: 55-58]

 

Rejea viungo viufatavyo upate faida zaidi:

 

004-Majina Ya Allaah Na Sifa Zake: AR-RAHMAAN

 

005-Majina Ya Allaah Na Sifa Zake: AR-RAHIYM

 

 

Share