Shaykh Fawzaan: Kunyoa Ndevu Kwa Hoja Ya Kwamba Makafiri Na Wao Wanafuga Ndevu
Kunyoa Ndevu Kwa Hoja Ya Kwamba Makafiri Na Wao Wanafuga Ndevu
Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Baadhi ya watu wanasema mayahudi au baadhi ya washirikiana wanafuga ndevu zao hivi sasa na sisi tumeamrishwa kwenda kinyume nao...
JIBU:
Hatukuamrishwa kwenda kinyume nao katika kufuga ndevu. Tumeamrishwa kwenda kinyume nao katika kunyoa.
Ama wakiachia ndevu zao basi wameafikiana na sisi. Kafiri ambaye amefuga ndevu zake ana sura bora kuliko kafiri ambaye ananyoa ndevu zake.
[Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan
http://www.alfawzan.af.org.sa/node/5570]