051-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 051: أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ وَالطَّاغُوتِ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
An-Nisaa 051-Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini itikadi potofu na twaghuti na ...
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ وَالطَّاغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا هَـٰؤُلَاءِ أَهْدَىٰ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا سَبِيلًا ﴿٥١﴾
Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini itikadi potofu na twaghuti na wanasema juu ya wale waliokufuru kuwa: Hawa wameongoka zaidi katika njia kuliko wale walioamini.
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ ۖ وَمَن يَلْعَنِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ نَصِيرًا ﴿٥٢﴾
Hao ndio wale Allaah Aliowalaani. Na ambaye Allaah Amemlaani basi hutamkuta kuwa na mtu wa kumsaidia. [An-Nisaa (4:51-52)
Sababun-Nuzwul:
Aayah hii imeteremshwa kama alivyohadithia ‘Ikrimah (رضي الله عنه) kwamba Huyay bin Akhtab na Ka’b Al-Ashraf (Wakuu wa ki-Yahudi) walikuja kwa watu wa Makkah (washirikina) wakawaambia: Nyinyi (Mayahudi) ni Ahlul-Kitaab na wenye ‘ilmu, hivyo basi tujulisheni (tofauti zetu) kuhusu sisi na kuhusu Muhammad. Wakasema: Jielezeni kuhusu nyinyi na kuhusu Muhammad. Wakasema: Sisi tunaunga ujamaa wa uhusiano wa damu, tunachinja ngamia (kwa ajili ya mafukara), tunasamehe madeni, tunawapa maji Mahujaji. Ama Muhammad, yeye hana watoto wa kiume, amekata ujamaa wa uhusiano wa damu, na wevi wa Mahujaji (kabila la) Ghifar wanamfuata. Basi je, sisi bora au yeye? Wakasema: Nyinyi bora zaidi na mlioongoka zaidi katika njia. Hapo Allaah Akateremsha:
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ وَالطَّاغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا هَـٰؤُلَاءِ أَهْدَىٰ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا سَبِيلًا ﴿٥١﴾
Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini itikadi potofu na twaghuti na wanasema juu ya wale waliokufuru kuwa: Hawa wameongoka zaidi katika njia kuliko wale walioamini.
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ ۖ وَمَن يَلْعَنِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ نَصِيرًا ﴿٥٢﴾
Hao ndio wale Allaah Aliowalaani. Na ambaye Allaah Amemlaani basi hutamkuta kuwa na mtu wa kumsaidia. [An-Nisaa (4:51-52)]