Al-Lajnah Ad-Daaimah: Tafsiyr Ya Qur-aan Ya Muhammad Asad Imepigwa Marufuku
Tafsiyr Ya Qur-aan Ya Muhammad Asad Imepigwa Marufuku
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Ni kwanini tafsiyr iliyotajwa hapo juu imechapishwa ndani ya nchi ya Waislam ukiangalia kwamba Muhammad Asad – kwa ufahamu wangu – anaishi ndani ya Nchi ya Kifalme ya Morocco? Sioni chochote ndani ya Qur-aan au Sunnah kukubaliana na yale masuala yaliyoelezwa ndani yake. Nategemea kwamba Fatwa yako itakubaliana na mimi ili kuyaondosha mambo haya na kuzuia uchapishaji wa tafsiyr hii hapa nchini.
JIBU:
Tafsiry iliyotajwa ina makosa makubwa na itikadi batili zilizo wazi.
Kwa matokeo hayo, Baraza la Katiba la Umoja wa Waislam Duniani jijini Makkah imetoa amri kuzuia upigaji chapa na uchapishaji wa tafsiyr hii.
Allaah Atujaalie mafaniko! Swalah na Salaam ziwe juu ya Nabiy wetu Muhammad, familia yake, na Maswahaba zake.
Kamati ya Kudumu ya Utafiti wa Kielimu Na Utoaji Fatwa
`Abdul-`Aziyz bin `Abdillaah bin Baaz – Mwenyekiti
`Abdur-Razzaaq `Afifiy – Naibu Mwenyekiti
`Abdullaah bin Qa`uwd – Mjumbe
`Abdullaah bin Ghudayyaan – Mjumbe
[Kamati ya Kudumu ya Fatwa, Fungu La 1, Sura Ya 3: ‘Aqiydah 3, Mitume, ’Iysaa (‘Alayhis-Salaam), Tafsiyr Ya Qur-aan Tukufu Ya Muhammad Asad]