Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Anapokukaribisha Chakula Mtu Kwa Kuona Hayaa, Usiitikie Mwaliko Huo

Anapokukaribisha Chakula Mtu Kwa Kuona Hayaa, Usiitikie Mwaliko Huo

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

“Atakapokaribishwa mtu kuingia kwenye nyumba kwa ajili ya chakula, naye anatambua kuwa kualikwa au kukaribishwa huko ni kwa sababu ya hayaa tu, basi asiitikie (wito, mwaliko huo). Na haijuzu kwake kuitikia (wito, mwaliko huo).

Na hili hutokea sana, (anaweza) akatoka mtu nyumbani kwake kwa ajili ya shughuli fulani, mara ghafla anakutana na rafiki yake mlangoni (kwake), anamwambia: karibu, kwa hayaa tu bila kukusudia kumkirimu; basi ni haramu kwake (huyo aliyekaribishwa) kuitikia (mwaliko huo) kwa sababu (aliyemkaribisha chakula) kafanya hivyo kwa kuona hayaa tu.”

 

 

[At-Ta’liyq ‘Alaa Kitaab Al-Qawaaid Wal-Uswuwl Al-Jaami’ah, uk. 42]

 

 

Share