Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kuchukua Vifaa Vya Hospitali Bila Kutambua Kuwa Ni Dhambi Je Arudishe?

Kuchukua Vifaa Vya Hospitali Bila Kutambua Kuwa Ni Dhambi; Je, Arudishe?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Mwanamke aliyelazwa hospitali masiku kadhaa - pindi alipotolewa hospitali alichukua vikombe (au gilasi) arubaini ambayo ni vya hospitali na hakutambua hukmu yake alipokuwa akichukua. Sasa amehamia mji mwengine; je, afanyeje? Arudishe (vikombe) alivyochukua hospitali au avitolee swadaqah kwa thamani yake?

 

 

JIBU:

 

Nataraji kuwa mwanamke huyu hatopata dhambi kwa kuchukua hivyo vikombe kwa vile alidhani hakuna madhara kuvichukua kwake. Lakini lazima avirudishe hospitali hata kama amehama mji. Hilo ni kwa sababu (vitu) hivyo ni haki ya mtu anayemiliki hiyo hospitali na ni wajibu kurejesha haki ya mtu au akaombe ruhusa kuvibakisha kwake. Kwa hiyo anatakiwa kurudisha hivyo vikombe alivyochukua hospitalini.

 

 

[Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb (As-Suaal 6291 (12/121)]

 

Share