018-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukataza Bid’ah Na Uzushi
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن البدع ومحدثات الأمور
018 - Mlango Wa Kukataza Bid’ah Na Uzushi
قَالَ تَعَالَى:
فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ ۖ
Na kuna nini baada ya haki ila upotofu? [Yuwnus: 32]
مَّا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِن شَيْءٍ ۚ
Hatukusuru katika Kitabu kitu chochote. [Al-An’aam: 38]
فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ
Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli. [An-Nisaa: 59]
وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ
Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake. [Al-An’aam: 153]
قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ
Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. [Aal-‘Imraan: 31]
Hadiyth – 1
عن عائشة رَضِي الله عنها، قَالَتْ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ أحْدَثَ في أمْرِنَا هَذَا مَا لَيْسَ مِنْهُ فَهُوَ رَدٌّ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
وفي رواية لمسلم: ((مَنْ عَمِلَ عَمَلًا لَيْسَ عَلَيهِ أمرُنا فَهُوَ رَدٌّ))
‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Mwenye kuzua katika jambo letu hili lisilokuwemo humo litakataliwa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riwaayah nyingine ya Muslim: “Mwenyekufanya amali isiyokuwa na hukmu yetu, itakataliwa.”
Hadiyth – 2
وعن جابر رضي الله عنه قَالَ: كَانَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم إِذَا خَطَبَ احْمَرَّتْ عَينَاهُ، وَعَلا صَوتُهُ، وَاشْتَدَّ غَضَبُهُ، حَتَّى كَأنَّهُ مُنْذِرُ جَيشٍ، يَقُولُ: ((صَبَّحَكُمْ وَمَسَّاكُمْ)) وَيَقُولُ: ((بُعِثتُ أنَا والسَّاعَةُ كَهَاتَينِ)) وَيَقْرِنُ بَيْنَ أُصبُعَيهِ السَّبَّابَةِ وَالوُسْطَى، وَيَقُولُ: ((أمَّا بَعْدُ، فَإنَّ خَيْرَ الحَديثِ كِتَابُ الله، وَخَيرَ الهَدْيِ هَدْيُ مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم، وَشَرَّ الأُمُورِ مُحْدَثَاتُهَا، وَكُلَّ بِدْعَة ضَلالَةٌ)) ثُمَّ يَقُولُ: ((أنَا أوْلَى بِكُلِّ مُؤمِنٍ مِنْ نَفسِهِ، مَنْ تَرَكَ مَالًا فَلأَهْلِهِ، وَمَنْ تَرَكَ دَيْنًا أَوْ ضَيَاعًا فَإلَيَّ وَعَلَيَّ)). رواه مسلم
وعن العرباض بن سَارية رضي الله عنه حدِيثه السابق في بابِ المحافظةِ عَلَى السنةِ
وفيه: ((فإنه من يعش منكم فسيرى اختلافًا كثيرًا فعليكم بسنَّتي...))
Kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba: Alipokuwa akikhutubia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) macho yake yalikuwa yakibadilika rangi na kuwa mekundu, na akinyanyua sauti yake na ghadhabu ilikuwa kali kana kwamba alikuwa akitutahadharisha na jeshi la adui. Alikuwa akisema: “Maadui watawashambulieni asubuhi na usiku.” Na pia akisema: “Nimetumwa mimi kuja siku mwisho kama hivi.” Na alikuwa anavishikanisha vidole vyake (kidole cha kati na cha shahada), na akisema tena: Ama baada (ya salamu): “Hakika mazungumzo bora ni maneno ya Allaah (Qur-aan) na uongofu bora ni uongofu wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam), na mambo yaliyomaovu ni yale yenyekuzuliwa na kila bid’ah ni upotevu.” [Muslim]
Kisha alikuwa akisema: “Mimi ni mwenyekumtakia kila Muumin masilahi yake kuliko anavyojitakia nafsi yake, hivyo yoyote atayeacha mali ni kwa watu wake, na yoyote atakayeacha deni au watoto na familia basi hayo yatakuwa juu yangu.”
Na imepokewa kwa ‘Irbaadhw bin Saariyah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Hadiyth iliyotangulia katika mlango wa: Amri ya kuhifadhi Sunnah na adabu zake: “Hakika atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona khitilafu nyingi.”