019-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Mwenye Kuzua Sunnah Nzuri Na Mbaya

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فيمن سن سنة حسنة أَوْ سيئة

019 – Mlango Wa Mwenye Kuzua Sunnah Nzuri Na Mbaya

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ تَعَالَى:

 

وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا ﴿٧٤﴾

Na wale wanaosema: “Rabb wetu! Tutunukie katika wake zetu na dhuria wetu viburudisho vya macho yetu, na Tujaalie kuwa waongozi kwa wenye taqwa. [Al-Furqaan: 74]

 

وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا

Na Tukawajaalia Maimaam wanaongoza kwa amri Yetu. [Al-Anbiyaa: 73]

 

 

Hadiyth - 1

عن أَبي عمرو جرير بن عبد الله رضي الله عنه قَالَ: كنا في صَدْرِ النَّهَارِ عِنْدَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم فَجَاءهُ قَومٌ عُرَاةٌ مُجْتَابي النِّمَار أَوْ العَبَاء، مُتَقَلِّدِي السُّيُوف، عَامَّتُهُمْ من مُضر، بَلْ كُلُّهُمْ مِنْ مُضَرَ، فَتَمَعَّرَ وَجْهُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم لما رَأَى بِهِمْ مِنَ الفَاقَة، فَدَخَلَ ثُمَّ خَرَجَ، فَأَمَرَ بِلالًا فَأَذَّنَ وَأَقَامَ، فصَلَّى ثُمَّ خَطَبَ، فَقَالَ: (({يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ نَفْسٍ وَاحِدَةٍ} إِلَى آخر الآية: {إِنَّ اللهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا}، والآية الأُخْرَى التي في آخر الحَشْرِ: {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللهَ وَلْتَنْظُرْ نَفْسٌ مَا قَدَّمَتْ لِغَدٍ} تَصَدَّقَ رَجُلٌ مِنْ دِينَارِهِ، مِنْ دِرهمِهِ، مِنْ ثَوبِهِ، مِنْ صَاعِ بُرِّهِ، مِنْ صَاعِ تَمْرِهِ- حَتَّى قَالَ: وَلَوْ بِشقِّ تَمرَةٍ)).

فَجَاءَ رَجُلٌ مِنَ الأَنْصَارِ بِصُرَّةٍ كَادَتْ كَفُّهُ تَعجَزُ عَنهَا، بَلْ قَدْ عَجَزَتْ، ثُمَّ تَتَابَعَ النَّاسُ حَتَّى رَأيْتُ كَومَيْنِ مِنْ طَعَامٍ وَثِيَابٍ، حَتَّى رَأيْتُ وَجْهَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يَتَهَلَّلُ كَأنَّهُ مُذْهَبَةٌ. فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ سَنَّ في الإسلامِ سنَّةً حَسَنَةً فَلَهُ أجْرُهَا، وَأجْرُ مَنْ عَمِلَ بِهَا مِنْ بَعْدَهُ، مِنْ غَيرِ أنْ يَنْقُصَ مِنْ أُجُورهمْ شَيءٌ، وَمَنْ سَنَّ في الإسْلامِ سُنَّةً سَيِّئَةً كَانَ عَلَيهِ وِزْرُهَا، وَوِزْرُ مَنْ عَمِلَ بِهَا مِنْ بَعْدِهِ، مِنْ غَيرِ أنْ يَنْقُصَ مِنْ أوْزَارِهمْ شَيءٌ)). رواه مسلم

Abuu ‘Amruw Jariyr bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba: Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) mchana na siku moja. Wakati huo mara wakaja watu waliokuwa hawakuvaa nguo bali nguo za magunia katika miili yao, na wengine walikuwa na kama majoho, panga zao zikiwa zinagusa chini. Takriban wote walikuwa wanatoka kabila ya Mudhar, bali wote walikuwa ni kutoka kabila la Mudhar. Uso wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) ulibadilika kwa kuwaona hawa watu katika hali hii ya shida na njaa. Akaingia nyumbani kwake kisha akatoka. Alimuamuru Bilaal (Radhwiya Allaahu 'anhu) aadhini kisha akimu, baada ya hapo aliswalisha na kuwahutubia watu baada ya Swalah, akasema: Enyi watu! Mcheni Rabb wenu Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja (Aadam) na Akaumba kutoka humo mke wake (Hawwaa) na Akaeneza kutoka hao wawili wanaume na wanawake wengi. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mnaombana (haki zenu kwa kuunga) undugu. Hakika Allaah ni Mwenye kuwachunga daima.”

 

”Kisha akasoma ile aayah nyingine ambayo ipo mwisho wa Suwratu Al-Hashr: Enyi walioamini! Mcheni Allaah, na nafsi itazame imetanguliza nini kwa ajili ya kesho, na mcheni Allaah.”

Baada ya hayo akawaomba watu watoe sadaka katika dinari zao, dirhamu, nguo, kipimo maalumu cha ngano na tende mpaka akasema: “Hata kama ni kipande cha tende.” Kusikia haya mtu mmoja wa ki Answaar alikuja na mzigo mkubwa, ambao ulimuelemea sana kuubeba. Wengine wakamfuata kwa kuleta sadaka zao mpaka nikaona milima miwili ya chakula na nguo. Hapo nikauona uso wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) unang’aa kama dhahabu. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alisema baada ya hayo: “Yeyote atakayezua katika Uislamu Sunnah nzuri atapata thawabu ya kitendo hicho na ujira (thawabu) za wenye kufanya kitendo hicho baada yake bila ya wale waliokuja baada yake kupunguziwa thawabu zao. Na yeyote atakayezua katika Uislamu Sunnah mbaya, atapata madhambi ya kufanya jambo hilo na madhambi ya wenye kumfuata yeye baada yake bila ya wao kupunguziwa chochote katika madhambi yao. [Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن ابنِ مسعود رضي الله عنه أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((لَيْسَ مِنْ نَفْسٍ تُقْتَلُ ظُلْمًا إلا كَانَ عَلَى ابْنِ آدَمَ الأوْلِ كِفْلٌ مِنْ دَمِهَا، لأَنَّهُ كَانَ أوَّلَ مَنْ سَنَّ القَتلَ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Kutoka kwa Ibn Mas’uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Hakuna nafsi yeyote inayouliwa kwa dhulma isipokuwa yule mwanadamu wa kwanza atapata sehemu yake ya madhambi (ya mauaji) kwani yeye ndiye wa mwanzo kuanzisha mauaji.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share