020-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuhimiza Mema Na Kuwaita Watu Katika Uongofu Au Upotevu
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب في الدلالة عَلَى خير والدعاء إِلَى هدى أَوْ ضلالة
20 – Mlango Wa Kuhimiza Mema Na Kuwaita Watu Katika Uongofu Au Upotevu
قَالَ تَعَالَى:
وَادْعُ إِلَىٰ رَبِّكَ ۖ
Na lingania kwa Rabb wako… [Al-Qaswasw: 87]
ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ
Lingania katika njia ya Rabb wako kwa hikmah na mawaidha mazuri. [An-Nahl: 125]
وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ
Na shirikianeni katika wema na taqwa… [Al-Maaidah: 2]
وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ
Na watokeze kutoka kwenu umati wa watu unaolingania kheri… [Aal-‘Imraan: 104]
Hadiyth – 1
وعن أَبي مسعود عُقبةَ بنِ عمرو الأنصاري البدري رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ دَلَّ عَلَى خَيْرٍ فَلَهُ مِثْلُ أجْرِ فَاعِلِهِ)). رواه مسلم
Kutoka kwa Abuu Mas’uwd ‘Uqbah bin ‘Amru Al-Answaar Al-Badriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam): “Yeyote mwenye kumuelekeza mtu katika jambo jema atapata ujira wa mfano wa yule mwenye kufanya (hilo jambo jema).” [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((مَنْ دَعَا إِلَى هُدَىً، كَانَ لَهُ مِنَ الأَجْرِ مِثْلُ أجُورِ مَنْ تَبِعَه، لاَ يَنْقُصُ ذلِكَ مِنْ أجُورِهمْ شَيئًا، وَمَنْ دَعَا إِلَى ضَلاَلَةٍ، كَانَ عَلَيهِ مِنَ الإثْمِ مِثْلُ آثَامِ مَنْ تَبِعَهُ، لا يَنْقُصُ ذلِكَ مِنْ آثَامِهِمْ شَيئًا)). رواه مسلم
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: “Yeyote anayewaita wengine katika uongofu atapata thawabu mfano wa wale wenye kumfuata wala hilo haliwapunguzii thawabu zao hata kidogo. Na yeyote atakayewaita watu katika upotevu atapata madhambi mfano wa madhambi ya wale wenye kumfuata na wala hilo halitawapunguzia madhambi hata chembe.” [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أَبي العباس سهل بن سعد الساعدي رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ يوم خَيبَر: ((لأُعْطِيَنَّ الرَّايَةَ غَدًا رجلًا يَفْتَحُ الله عَلَى يَدَيهِ، يُحبُّ اللهَ وَرَسولَهُ، ويُحِبُّهُ اللهُ وَرَسُولُهُ))، فَبَاتَ النَّاسُ يَدُوكُونَ لَيْلَتَهُمْ أيُّهُمْ يُعْطَاهَا. فَلَمَّا أصْبَحَ النَّاسُ غَدَوْا عَلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم كُلُّهُمْ يَرْجُو أنْ يُعْطَاهَا. فَقَالَ: ((أينَ عَلِيُّ بنُ أَبي طالب؟)) فقيلَ: يَا رسولَ الله، هُوَ يَشْتَكي عَيْنَيهِ. قَالَ: ((فَأَرْسِلُوا إِلَيْه)) فَأُتِيَ بِهِ فَبَصَقَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم في عَيْنَيْهِ، وَدَعَا لَهُ فَبَرِئَ حَتَّى كأنْ لَمْ يكُن بِهِ وَجَعٌ، فأعْطاهُ الرَّايَةَ. فقَالَ عَليٌّ رضي الله عنه: يَا رَسُول اللهِ، أقاتِلُهمْ حَتَّى يَكُونُوا مِثْلَنَا؟ فَقَالَ: ((انْفُذْ عَلَى رِسْلِكَ حَتَّى تَنْزِلَ بسَاحَتهمْ، ثُمَّ ادْعُهُمْ إِلَى الإسْلاَمِ، وَأخْبِرْهُمْ بِمَا يَجِبُ عَلَيْهِمْ مِنْ حَقِّ اللهِ تَعَالَى فِيهِ، فَوَالله لأَنْ يَهْدِيَ اللهُ بِكَ رَجُلًا وَاحِدًا خَيرٌ لَكَ مِنْ حُمْرِ النَّعَم)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Kutoka kwa Abul-‘Abbaas Sahl bin Sa’d As-Saa’idiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alisema siku ya Khaybar: “Kesho nitampatia mtu bendera ambaye kwa mikono yake Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) atafungua (mji huu). Mtu huyo anampenda Allaah na Rasuli wake, basi Allaah na Rasuli wake wanampenda.” Watu wakakesha wakifikiria na kuzungumza juu ya nani atayepatiwa bendera hiyo. Kulipopambazuka watu wote walikwenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) kila mmoja anatarajia kuwa atapatiwa yeye jukumu hilo. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam): “Yuko wapi ‘Aliy bin Abiy Twaalib?” Wakasema: “Ee Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)! Yeye anaumwa macho.” Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam): “Mleteni kwangu.” Akaletwa kwake, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) akampaka mate yake katika macho na kumwombea kwa Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa). ‘Aliy akapona kabisa na ugonjwa huo (wa macho) mpaka ikaonekana kama kwamba hakuwa na tatizo lolote na hapo akapatiwa bendera. ‘Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) akasema: “Ee Mjumbe wa Allaah! Nipigane nao mpaka wawe kama sisi?” Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam): “Endelea kwenda kwa kasi yako ya kawaida mpaka ufike katika bonde lao na hapo muweke kambi yenu. Kisha waite katika Uislamu na uwapashe habari kuhusu wajibu wao na majukumu yao kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ndani yake. Naapa kwa Allaah! Allaah akimuongoa mtu mmoja kupitia kwako ni bora kuliko kundi la ngamia wekundu. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن أنس رضي الله عنه: أن فتىً مِنْ أسلم قَالَ: يَا رَسُول الله، إنِّي أُرِيدُ الغَزْوَ وَلَيْسَ معي مَا أتَجَهَّز بِهِ، قَالَ: ((ائتِ فُلاَنًا فإنَّهُ قَدْ كَانَ تَجَهَّزَ فَمَرِضَ)) فَأتَاهُ، فَقَالَ: إنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يُقْرِئُكَ السَّلامَ، وَيَقُولُ: أعْطني الَّذِي تَجَهَّزْتَ بِهِ، فَقَالَ: يَا فُلاَنَةُ، أعْطِيهِ الَّذِي تَجَهَّزْتُ بِهِ، وَلا تَحْبِسي مِنْهُ شَيئًا، فَواللهِ لا تَحْبِسِين مِنْهُ شَيئًا فَيُبَاركَ لَكِ فِيهِ. رواه مسلم
Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba kijana katika kabila la Aslam alikuja na kusema: “Ee Mjumbe wa Allaah! Mimi ninataka kushiriki katika vita, lakini sina chochote cha kujitayarisha kwayo?” Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam): “Nenda kwa Fulani kwani yeye amejitayarisha lakini akashikwa na maradhi.” Huyu kijana akaenda kwa huyo mtu na kumwambia: “Kwa hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) anakutolea salamu na anakwambia: Nipatie mimi vifaa ulivyovitayarisha ili kuvitumia katika vita.” Akasema yule Fulani: “Ewe mke wangu mpatie kila kitu nilichotayarisha wala usibakishe chochote. Naapa kwa Allaah, kisha ikiwa hutamnyima chochote katika vifaa nilivyotayarisha, Allaah atakubariki kwayo.” [Muslim]