156-Aayah Na Mafunzo: Rahmah Za Allaah Ni Mia: Moja Duniani, Tisini Na Tisa Aakhirah
Aayah Na Mafunzo
Al-A’raaf 156
156-Rahmah Za Allaah Ni Mia: Moja Duniani, Tisini Na Tisa Aakhirah
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَاكْتُبْ لَنَا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ إِنَّا هُدْنَا إِلَيْكَ ۚ قَالَ عَذَابِي أُصِيبُ بِهِ مَنْ أَشَاءُ ۖ وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ فَسَأَكْتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالَّذِينَ هُم بِآيَاتِنَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٥٦﴾
Na Tuandikie katika dunia hii mazuri na katika Aakhirah. Hakika sisi tumerudi kutubu Kwako. (Allaah) Akasema: Adhabu Yangu Nitamsibu nayo Nimtakaye. Na Rahmah Yangu imeenea kila kitu. Basi Nitawaandikia wale wenye taqwa na wanaotoa Zakaah na ambao wao wanaziamini Aayaat (ishara, dalili) Zetu. [Al-A'raaf: 156]
Mafunzo:
Rahmah Za Allaah (سبحانه وتعالى) Ni Mia: Moja Duniani Na Rahmah Tisini Na Tisa Aakhirah:
Amesimulia Salmaan (رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah (عزّ وجلّ) Ana Rahmah mia. Katika hizo, Rahmah moja wanarehemiana viumbe baina yao, hata mnyama mwitu anakihurumia kizazi chake. Rahmah tisini na tisa Ameziweka kwa ajili ya Siku ya Qiyaamah.” [Ahmad]
Rejea Tanbihi Ya Al-Faatihah (1:1)