Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Du'aa Ni ‘Ibaadah Hata Ikihusu Kuomba Mambo Ya Kidunia
Du'aa Ni ‘Ibaadah Hata Ikihusu Kuomba Mambo Ya Kidunia
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
“Hakuna ubaya kuomba jambo linalohusiana na mambo ya kidunia mfano mtu aseme: “Ee Allaah niruzuku nyumba pana”.
Au “Ee Allaah niruzuku mke mzuri”.
Au, “Ee Allaah, niruzuku mali nyingi”.
Au, “Ee Allaah niruzuku gari zuri”.
Hivyo kwa sababu du’aa ni ‘ibaadah hata kama ni kuhusu mambo ya dunia, kwani bin Aadam hana kimbilio isipokuwa kwa Allaah”.
[Ash-Sharh Al-Mumti’ (3/284)]