Kumwita Mtoto Jina La Balqiys Au Bilqiys
Kumwita Mtoto Jina La Balqiys Au Bilqiys
SWALI:
Assalaam alykum warahmatullaah wabakaatuh.
Sifa njema ni za Allaah, mola wa viumbe vyote. Sala na salaam zimwendee mtume wetu Muhammad Namshukuru Allaah aliyenijalia pamoja nanyi kuwa waislam.
Maelezo: Mke wangu ni mjamzito na anakaribia kujifungua. Jalia amejifungua mtoto wa kike. (Allah ndo anajua zaidi kilichokuwa tumboni mwake). Yeye anataka amuite Balqees ambalo lilkuwa jina la mfalme wa Sabaa ambaye hakuwa muislam kabla kuolewa na nabii Suleiman kwa ninavyojua na sijui kama aliitwa jina jingine baada ya kusilimishwa.
Swali: Je, hilo jina linafaa kumuita mtoto wa kike muislam?
JIBU:
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Wa ‘alaykumussalaam wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh
Wanavyuoni wameona kuwa hakuna dalili ya kukatazwa katika Shariy’ah ya Kiislamu kumpa mtoto wa kike jina hilo. Kwa hiyo unaweza kumpa. Na kwa taarifa yako, wengine wamesema kuwa inatamkwa Balqiys na wengine wamesema ni Bilqiys. Na hayo ni matamshi ya Kiswahili kulinganisha na matamshi ya kiarabu ukipenda kutumia hivyo badala ya Balqees au Bilqees vyovyote mpendavyo wenyewe.
Na Allaah Anajua zaidi .