Shaykh Fawzaan: Ameacha Kuswali Baada Ya Kudhani Ni Hedhi Je Alipe Swalaah?
Ameacha Kuswali Baada Ya Kudhani Ni Hedhi Je Alipe Swalaah?
Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Je, mwanamke akiona damu kidogo akaacha kuswali, kisha damu ikasita siku hiyo (au ya pili yake), Je anatakiwa alipe Swalaah?
JIBU:
Ikiwa imemdhihirikia kwamba hiyo si damu ya hedhi basi ni wajibu kwake kulipa Swalaah hizo alizozikosa.
[Sharh ‘Umdatil-Fiqh Kanda Namba 7 Swali Namba 44]
