Imaam Al-Awzaaiy: Majuto Siku Ya Qiyaamah Kupoteza Muda Bila Kumdhukuru Allaah
Majuto Siku Ya Qiyaamah Kupoteza Muda Bila Kumdhukuru Allaah
Imaam Al-Awzaa’iy (Rahimahu-Allaah)
Imaam Al-Awzaa’iy (Rahimahu-Allaah) amesema:
“Hakuna saa katika saa za dunia isipokuwa itahudhurishwa mbele ya mja Siku ya Qiyaamah, siku na siku, saa na saa. Wala haipiti saa moja ambayo humo mtu hamdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) isipokuwa mtu ataijutia. Basi itakuwaje kwa ambaye yanampita masaa na masaa, siku na siku, usiku na usiku naye hamdhukuru Rabb wake?”
[Hilyatu Al-Awliyaa (6/142)]