Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Mtake Msaada Allaah Katika Kila Kitu

 
Mtake Msaada Allaah Katika Kila Kitu
 
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
 
 
 
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
 
 
"Inampasa mwana Aadam amtake msaada Allaah Mwenye Nguvu, Aliyetukuka katika kila kitu, hata katika mambo madogo kama vile: unapokwenda mahali, unaporejea, unapokula, unapokunywa, unapovaa, hadi (mja) anakuwa ni mwenye kutambua mahitajio yake, na ayafanye hayo kwa lengo la 'Ibaadah kwa Mola wake, Mwenye Nguvu, Aliyetukuka.
 
Na mja anapomtaka msaada Mola wake, basi (Mola wake) Atamwepesishia yeye mambo, na Atamsahilishia juu yake."
 
 
 
[Ahkaam Minal-Qur-aan Al-Kariym, mj. 1, uk. 37]
 
Share